Emmanuel Shangai (CCM) Jimbo la Ngorongoro ashinda Uchaguzi. Ndiye mrithi wa William Tate Ole Nasha (RIP)

Emmanuel Shangai (CCM) Jimbo la Ngorongoro ashinda Uchaguzi. Ndiye mrithi wa William Tate Ole Nasha (RIP)

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2020
Posts
2,823
Reaction score
2,466
MATOKEO YA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA NGORONGORO

Jumla ya Wapigakura Waliojiandikisha mwaka 2020 walikuwa ni 115,538

Jumla ya wapigakura Waliopiga kura kwenye marudio ya Uchaguzi wa Jimbo la Ngorongoro wa tarehe 11|12|2021 ni 62,528

Jumla ya Kura halali ni 62,461 huku jumla ya kura 67 zikikataliwa.

MATOKEO KWA MUJIBU WA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI.

Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Emmanuel Shangai amepata jumla ya kura 62,017 sawa na 99.18% ya kura zote zilizopigwa.

Mwitikio wa wapigakura ni 54% ya wapigakura wote waliojiandikisha mwaka 2020.

Hakika Watanzania bado wanaimani kubwa sana na CCM-Tanzania.

=====

Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini leo Jumapil imemtangaza Bw. Emmanuel Lekishon Shangai wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa ndie Mshindi katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Ngorongoro kwa kupata kura 62,017 Kati ya kura halali 62,461. Uchaguzi ambao vyama vikuu vya Upinzani viliususia

Mgombea wq ACT Wazalendo kapata kura 170 na Saimon Ngilisho wa Demokrasia Makini kapata kura 105.

20211212_142102.jpg
20211212_142107.jpg
 
Kongole kwake komredi Emmanuel Shangai💪

Kila la heri kwake na wapiga kura wake ,aaamin🙏

#Kazi Inaendelea
#Taifa Kwanza
#Siempre CCM
 
MATOKEO YA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA NGORONGORO,

===
Jumla ya Wapigakura Waliojiandikisha mwaka 2020 walikuwa ni 115,538...
Wapinzani hawajaibiwa kura maana kila mda wwo ndo huibiwa kura yaan badala ya kuwekeza wao propaganda ndo kila kitu
 
Back
Top Bottom