Naunga mkono ateuliwe, apewe!View attachment 3575088
Emmanuela Mtatifikolo, ameonesha dhamira yake ya dhati ya kuwatumikia wananchi kwa kuchukua na kurejesha fomu ya kuwania nafasi ya ubunge katika Jimbo la Isimani.
Hatua hii inaakisi utayari wake wa kupeleka uzoefu wake mpana wa kiuongozi katika ngazi ya juu ya uwakilishi wa wananchi.
Akiwa ni kiongozi mahiri mwenye rekodi ya utendaji uliotukuka, Emmanuela amewahi kushika nafasi mbalimbali muhimu serikalini na katika taasisi za kitaifa na kimataifa.
View attachment 3575089
Kwa sasa anahudumu kama Mkuu wa Wilaya ya Babati (2024 – sasa), baada ya kuitumikia nchi kama Mkuu wa Wilaya ya Arumeru (2023 – 2024). Kabla ya hapo, alikuwa Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Jitegemee Holdings Co. Ltd (2021 – 2024), akionesha ubunifu na umahiri katika kuendesha miradi ya maendeleo. Aidha, aliwahi kuwa Mratibu wa Mradi katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (Kibaha), Afisa Mchambuzi wa Miradi katika UNFPA 2016 – 2017, pamoja na Programme Officer for Africa katika taasisi ya UEM, akiratibu miradi katika nchi mbalimbali za Afrika na Asia.
Kitaaluma, Emmanuela ana sifa madhubuti zinazomuimarisha katika uongozi na utumishi wa umma. Ana Shahada ya Uzamili ya Afya ya Jamii Master of Public Health kutoka Chuo Kikuu cha Jiji la New York (2014 – 2017), pamoja na Stashahada ya Afya ya Jamii kutoka chuo hicho hicho. Vilevile, ana Shahada ya Sanaa katika Mawasiliano ya Umma (Mass Communication) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Mwanza (2001 – 2004).
Mchanganyiko huu wa elimu na uzoefu unamfanya kuwa kiongozi mwenye maono, uthubutu, na uwezo wa kuleta mageuzi chanya kwa wananchi wa Isimani.
Aya nenda kachukue elfu 7 yako sasa kama malipo ya kumpigia chapuo..!View attachment 3575088

Hii ndio ile ukifa mkeo anaolewa utake usitakeNa huyu ndiye mbunge wa isimani. over!
Hakika maana huyo ndiye chagua hasa la kizimkazi na anabaraka zoteHii ndio ile ukifa mkeo anaolewa utake usitake
Sio yule mrembo wa vangimembe?Naunga mkono ateuliwe, apewe!
P
Atapambana na mtoto wa familia marehemu au ....this time sio nafasi za kifalme ?Naunga mkono ateuliwe, apewe!
P
Hakuna nafasi zozote za kifalme kwenye siasa za kidemokrasia, na huo ndio uzuri wa demokrasia, kama baba /mama ni mwanasiasa, mke na watoto wanalelewa kiuanasiasa, wanakulia kwenye siasa, baba akitoka anaingia mke, akitoka anaingia mtoto, inaruhusiwa as long as anasifa na kukidhi vigezo.Atapambana na mtoto wa familia marehemu au ....this time sio nafasi za kifalme ?
Hili sio swali!, kwa Tanzania hapa tulipo, tuna chama kimoja tuu cha siasa, chama kwa maana ya chama, ni kimoja tuu, the one and only!.Chama gani?
Indira Gandhi hakuwa mtoto wa Mahatma Gandhi bali mtoto wa Jawaharlal Nehru, jina la Gandhi ni kutoka kwa mme wake.Hakuna nafasi zozote za kifalme kwenye siasa za kidemokrasia, na huo ndio uzuri wa demokrasia, kama baba /mama ni mwanasiasa, mke na watoto wanalelewa kiuanasiasa, wanakulia kwenye siasa, baba akitoka anaingia mke, akitoka anaingia mtoto, inaruhusiwa as long as anasifa na kukidhi vigezo.
Hivyo ilivyo kwa India ya Mahatma Gandhi, akaja Indira Gandhi, akaja mwanae Ranjiv Gandhi, walipomuua, mkewe Sonia Gandhi akabeba mikoba!.
Hata US hii iko kwa Kenedies na Bush, alikuwa Bush baba, baadaye akaingia Bush mtoto. Jirani zetu Kenya Mzee Jomo Kenyetta na mwanae Uhuru Kenyetta, Mzee Jaramogi Oginga Odinga na Raila Omollo Odinga.
Tukija Tanzania, tulianzia Zanzibar kwa Abedi Amani Karume, akaja mwanae Amani Abedi Karume, kisha akaja Ali Hassan Mwinyi na Dr. Hussein Mwinyi, baada ya Jakaya Mrisho Kikwete, tuna Salma Kikwete na Riz1 Kikwete huku kwa Magufuli tuna Jesca.
That is democracy!.
P
Wewe mzee utakuwa sio wa kawaida. Huwa uko mbele sana ya muda. Ila kwanini huwa unashindwa kujua kuwa utapigwa chini kila unapoomba kupeperusha bendera ya CCM?Naunga mkono ateuliwe, apewe!
P
Nq amepewa kweli 😂😂😂Naunga mkono ateuliwe, apewe!
P
Mimi ni wale CCM wa Nyerere, ambao hatunaga issues za kujua mtu. au kunyoosha mkono!. Uteuzi huu ni dalili njema ya CCM kurejea kuwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi sio chama cha matajiri, hao matajiri, wekwende zao na mapesa yao wakaendelee na biashara zao, sisi watuachie chama chetu!.Wewe mzee utakuwa sio wa kawaida. Huwa uko mbele sana ya muda. Ila kwanini huwa unashindwa kujua kuwa utapigwa chini kila unapoomba kupeperusha bendera ya CCM?