DodomaTZ
Senior Member
- May 20, 2022
- 197
- 233
Hatua hii inaakisi utayari wake wa kupeleka uzoefu wake mpana wa kiuongozi katika ngazi ya juu ya uwakilishi wa wananchi.
Akiwa ni kiongozi mahiri mwenye rekodi ya utendaji uliotukuka, Emmanuela amewahi kushika nafasi mbalimbali muhimu serikalini na katika taasisi za kitaifa na kimataifa.
Kitaaluma, Emmanuela ana sifa madhubuti zinazomuimarisha katika uongozi na utumishi wa umma. Ana Shahada ya Uzamili ya Afya ya Jamii Master of Public Health kutoka Chuo Kikuu cha Jiji la New York (2014 – 2017), pamoja na Stashahada ya Afya ya Jamii kutoka chuo hicho hicho. Vilevile, ana Shahada ya Sanaa katika Mawasiliano ya Umma (Mass Communication) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Mwanza (2001 – 2004).
Mchanganyiko huu wa elimu na uzoefu unamfanya kuwa kiongozi mwenye maono, uthubutu, na uwezo wa kuleta mageuzi chanya kwa wananchi wa Isimani.
Pia soma:
~ Fred Vunja Bei aongoza kura za maoni matokeo ya awali kumrithi Lukuvi. Awatupa wenzake mbali kama mshale
~ CCM Iringa Vijijini yaanza Uchukuaji Fomu za Ubunge jimbo la Ismani kwa Lukuvi
~ TANZIA - Waziri William Lukuvi (na Mbunge wa Isimani) afariki Dunia