''Enchweke'': Sauti za waliokufa, inatokeaje mtu anaongea kwa niaba ya mfu?

mayenga

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2009
Posts
4,118
Reaction score
1,970
Wakuu,

Sina kiswahili sahihi cha neno ''enchweke'' ambalo kwa lugha yangu ya kihaya ni hali ya mzimu wa mtu aliyekufa kumwandama mtu aliye hai na kumfanya aongee kile anachokitaka. Mara nyingi marehemu hupenda kutoa wosia kwa waliobakia kupitia mtu huyo. Nimeishuhudia mjomba wangu alipofariki bibi yangu alisumbuliwa sana na mzimu wa mjomba.

Swali langu ni kwa jinsi gani inatokea mzimu wa mtu unamkalia mwingine na kutoa maagizo? Mara nyingi sauti na matendo ya mtu aliyekaliwa na mzimu huendana na kushahabiana kabisa na marehemu.

Wajuvi nijuzeni tafadhali.
 
Duh!,hii ndo mara ya kwanza mimi kuisikia;Mkuu wewe ni Mhaya wa wapi??.
 
Ni kweli hiki kitu kipo sana huko uhayani kwetu na imetokea pia kwenye ukoo wangu. Lakini sijui mpaka leo nini huwa kipo hapo? Na makuzi yangu pia nimekulia kwenye nyumba ya msonge nilikuwa nikiona wazee wakiweka vitu humo. Miaka ya karibuni nimekwenda hapo nilipolelewa msonge haupo tena isipokuwa kila mwanaukoo amejitengenezea msonge wake, na madhara niliyoyakuta ndani ya ukoo wangu ni wagonjwa mwenye kuugua magonjwa ya ajabu sana, hayaelezeki kwa kweli. Kama kuna mwana JF wa kabila hili tupe kidogo uzoefu. Si vibaya Mwl. asiye na makuu Mshana Jr na wenzeke tuongezeeni maarifa ya akili.
 
Kwa uelewa wangu wa harakaharaka hayo ni mapepo,ambayo kama unataka unaweza ukayaepuka kama utaamua kumgeukia Mungu wa kweli,kwani ninauhakika roho mtakatifu akishaingia hapo hakuna kitakochobakia CC: mshana jr Pasco Rakims wekeni ufafanuzi pale.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu,

Sina kiswahili sahihi cha neno ''enchweke'' ambalo kwa lugha yangu ya kihaya ni hali ya mzimu wa mtu aliyekufa kumwandama mtu aliye hai na kumfanya aongee kile anachokitaka. Mara nyingi marehemu hupenda kutoa wosia kwa waliobakia kupitia mtu huyo. Nimeishuhudia mjomba wangu alipofariki bibi yangu alisumbuliwa sana na mzimu wa mjomba.

Swali langu ni kwa jinsi gani inatokea mzimu wa mtu unamkalia mwingine na kutoa maagizo? Mara nyingi sauti na matendo ya mtu aliyekaliwa na mzimu huendana na kushahabiana kabisa na marehemu.

Wajuvi nijuzeni tafadhali.
Mkuu , kitu hicho kipo sana na sio kwa Wahaya tuu, bali kwa binadamu wote!.
Mizimu kwa lugha rahisi ni spirits, kuna Holly Spirit ambayo ni roho wa Mungu, kuna human spirits, ambazo ni roho za anadamu, kuna ghosts, kuna wondering spirits na kuna evil spirits ambazo zinaitwa mapepo au mashetani.

Ulimwengu una sehemu kuu mbili, ulimwengu wa miili, physical world na ulimwengu wa roho, spiritual world, na mwili wa binadamu una sehemu kuu mbili, physical body, mwili huu wa nyama na spiritual body, mwili wa kiroho. Mtu anapokufa, kinachokufa ni mwili wa nyama tuu, ukizika unaoza na biahara ya mili a nyama inaishia hapo!, lakini mwili wa roho haifi, huu unaishi milele!.

Zile roho za wafu ndizo zinazoitwa mizimu.

Unaweza kunisoma zaidi katika mada hizi.

Hizi nimezizungumza sana humu, kwenye mada ya
[h=3]Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. [/h][h=3]"Will Powers!", "Faith Healing!"-NgMiujiza Ya Uponyaji kwa Im[/h][h=3]Muda mfupi Kabla ya Kukata roho: NINI HUTOKEA?[/h] [h=3]Yahusu: Majini mahaba..[/h]Pasco
 
hayo ni mapepo yanajibadilisha kuwa kama marehemu ili myatimizie haja zao. aliyekufa kafa na hawezi kurudi ktk mfumo wowote ule
 
Wakuu,

Sina kiswahili sahihi cha neno ''enchweke'' ambalo kwa lugha yangu ya kihaya ni hali ya mzimu wa mtu aliyekufa kumwandama mtu aliye hai na kumfanya aongee kile anachokitaka. Mara nyingi marehemu hupenda kutoa wosia kwa waliobakia kupitia mtu huyo. Nimeishuhudia mjomba wangu alipofariki bibi yangu alisumbuliwa sana na mzimu wa mjomba.

Swali langu ni kwa jinsi gani inatokea mzimu wa mtu unamkalia mwingine na kutoa maagizo? Mara nyingi sauti na matendo ya mtu aliyekaliwa na mzimu huendana na kushahabiana kabisa na marehemu.

Wajuvi nijuzeni tafadhali.
Mkuu hakuna jambo kama hilo....kama wewe ni mkristo rejelea Biblia....kwa maana walio hai wanajua watakufa lakini wafu hawajui neno lolote anayeongea si-marehemu, mungu amemuita Ibilisi BABA WA UONGO kuwa makini.
 
Mkuu kuwepo lipo,sema tu ni ya kupuuzia,ila kujifunza na kujua ni muhimu.
 
niliwai soma kadea in late 80. kule kanyigo yapo sana. kuna rafki yangu alinipeleka kwao kwenye hatusi yakatokea. huwa yanasisitiza upendo na aman.kama kuna vurugu yakiongea yanatuliza
 
Wakuu,

Sina kiswahili sahihi cha neno ''enchweke'' ambalo kwa lugha yangu ya kihaya ni hali ya mzimu wa mtu aliyekufa kumwandama mtu aliye hai na kumfanya aongee kile anachokitaka. Mara nyingi marehemu hupenda kutoa wosia kwa waliobakia kupitia mtu huyo. Nimeishuhudia mjomba wangu alipofariki bibi yangu alisumbuliwa sana na mzimu wa mjomba.

Swali langu ni kwa jinsi gani inatokea mzimu wa mtu unamkalia mwingine na kutoa maagizo? Mara nyingi sauti na matendo ya mtu aliyekaliwa na mzimu huendana na kushahabiana kabisa na marehemu.

Wajuvi nijuzeni tafadhali.
Ni uhuni tu wala huwa hakuna kitu kama hicho! Mtu huwa najifanya hivyo ili atoe vitisho kusudi jambo fulani analotaka lifanyike. Watu wanaogopa kufa, wanaogopa maiti etc, hivyo ukiwatisha hivyo unalotaka litafanyika. Sasa hivi yameisha baada ya watu kuelimika!
 
tungepata anayesumbuliwa na hili jambo nadhan tungepata sehem nzuri ya kuanzia! siamin kama kuna kitu kama hiki but i am willing to learn and accept kama kuna ushahidi!!
 
Back
Top Bottom