bullet
JF-Expert Member
- Oct 31, 2009
- 1,047
- 543
"Enchweke" ni kitu ambacho kipo katika jamii hasa ya Wanyambo na Wahaya na labda katika jamii nyingine. Kwa ufupi, "enchweke" ni uingiliaji kati (intervention) wa mtu aliyekwishafariki katika jambo la uonevu au uvunjaji wa haki anaofanyiwa mtu mnyonge ambaye kwa unyonge wake hawezi kujitetea. Huenda ni yatima anadhulumiwa au ni mjane ananyanyaswa au ni fukara anaonewa na ndugu zake matajiri nk. Marehemu ambaye alikuwa labda ni mzazi au mume huingilia kati machozi ya mtu anayenyanyaswa kupitia "enchweke". Ni hali kama ya kumtokea au mdhulumiwa ama mdhulumaji, mtu huyu hupoteza fahamu na kisha sauti ya marehemu hukemea hali ya uvunjaji haki iliyopo mara nyingine hata kwa kutangaza adhabu kwa wadhulumu ama laana. Kisha mtu huzinduka na kwa vyovyote vile yeye husimuliwa kilichotokea na mashuhuda. Wakati mwingine huchukua muda mrefu kwa "nchweke" kumwachia mtokewa mpaka wadhulumu au ndugu wafanye malipizi ya dhuluma inayokuwa imefanyika. Inawezekana ni aina ya Illicination!