Wakuu,
Sina kiswahili sahihi cha neno ''enchweke'' ambalo kwa lugha yangu ya kihaya ni hali ya mzimu wa mtu aliyekufa kumwandama mtu aliye hai na kumfanya aongee kile anachokitaka. Mara nyingi marehemu hupenda kutoa wosia kwa waliobakia kupitia mtu huyo. Nimeishuhudia mjomba wangu alipofariki bibi yangu alisumbuliwa sana na mzimu wa mjomba.
Swali langu ni kwa jinsi gani inatokea mzimu wa mtu unamkalia mwingine na kutoa maagizo? Mara nyingi sauti na matendo ya mtu aliyekaliwa na mzimu huendana na kushahabiana kabisa na marehemu.
Wajuvi nijuzeni tafadhali.
Mkuu , kitu hicho kipo sana na sio kwa Wahaya tuu, bali kwa binadamu wote!.
Mizimu kwa lugha rahisi ni spirits, kuna Holly Spirit ambayo ni roho wa Mungu, kuna human spirits, ambazo ni roho za anadamu, kuna ghosts, kuna wondering spirits na kuna evil spirits ambazo zinaitwa mapepo au mashetani.
Ulimwengu una sehemu kuu mbili, ulimwengu wa miili, physical world na ulimwengu wa roho, spiritual world, na mwili wa binadamu una sehemu kuu mbili, physical body, mwili huu wa nyama na spiritual body, mwili wa kiroho. Mtu anapokufa, kinachokufa ni mwili wa nyama tuu, ukizika unaoza na biahara ya mili a nyama inaishia hapo!, lakini mwili wa roho haifi, huu unaishi milele!.
Zile roho za wafu ndizo zinazoitwa mizimu.
Unaweza kunisoma zaidi katika mada hizi.
Hizi nimezizungumza sana humu, kwenye mada ya
[h=3]
Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. [/h][h=3]
"Will Powers!", "Faith Healing!"-NgMiujiza Ya Uponyaji kwa Im[/h][h=3]
Muda mfupi Kabla ya Kukata roho: NINI HUTOKEA?[/h] [h=3]
Yahusu: Majini mahaba..[/h]Pasco