Kabla ya mwisho wa dunia kuna mambo meeengi saaana yametabiriwa kutokea kama dalili,watu kuzidisha uovu kupindukia,maarifa kuwa makubwa mno,Dini kuchafuliwa,njaa,vita,magonjwa,mipango ya kuanzisha serikali moja na dini moja duniani,matetemeko ya ardhi makubwa sana,ishara za ajabu angani,jua kuwa kali kupindukia,vimondo kuipiga dunia(mvua ya mawe ya moto),viumbe wa ajabu kuvamia na kutesa binadamu,mataifa makubwa duniani kuporomoka,mji mkubwa sana duniani kuangamia,taasisi kubwa sana ya kidini duniani kuanguka,jua na mwezi kutiwa giza na baada ya hapo sasa....nikae kimya maana ni rahisi kuyaongea haya lakini kiuhalisia kuna shida huko mbele maana hata bible yenyewe inasema watu watatafuta kifo lakini kitawakimbia!
Sasa hayo yote mmeshayaona hata mseme dec 21 ni mwisho wa dunia? Hii tabia ya kupanga tarehe ya mwisho wa dunia ni mpango wa kishetani ili kuwafanya watu wapuuzie maonyo ya siku za mwisho pale watakapoona mwisho hautokei kwa tarehe zinazosemwa. Matokeo yake baadae watu watapuuza unabii na maonyo yote kuhusu mwisho wa dunia kiasi kwamba mwisho halisi utakapokuwa unafika wengi hawataamini wala kujua.mwisho tutaujua kwa dalili na ishara tulizoambiwa na sio kwa hesabu za muda.
Tuepuke kutumia unabii wa muda utatupoteza!
NASEMA HIVII, KESHO SIO MWISHO WA DUNIA!