END OF THE YEAR GIVE AWAY

END OF THE YEAR GIVE AWAY

trudie

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
3,668
Reaction score
8,745
Habari za jumapili wanaJF,

Kwanza namshukuru mwenyezi Mungu kwa pumzi aliyotupatia mpaka tumefika mwisho wa mwaka kwa neema yake pia tutauona mwaka mpya.
Kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa yote aliyonitendea kwa mwaka mzima narudisha shukrani kwa jamii.Najitolea kumpa member mmoja kiasi cha shilingi 100,000/= kama shukrani..
Ili kupata pesa hii niambie unadhani ni kwanini unastahili kuipata na utaifanyia nini..nitasoma comment na mshindi nitamchagua 2/1/2018..Asanteni sana.
 
Nadhani ingekuwa vzr hiyo hela ungenunua hata madaftari upeleke kwny kituo cha yatima wafungue shule wakiwa na furaha
Vituo vya yatima huwa natembelea sana na nimeshatoa kwa kiasi chake....this time nimewiwa kutoa kwa mtu mwingine tofauti na vituoni...Asante sana
 
Mkuu mm nikiipata nitampatia ndugu yangu ambaye ni mgonjwa ili aweze kununulia madawa na kulipia ada ya kitanda hospitalini.
 
baada ya kusoma hili bandiko lako, umenifanya nikafikiria vitu vingi chanya ambavyo ningeweza kufanya kwa kutumia Tsh 100,000. Mwaka 2018 ntajitahidi niwe na matumizi mazuri ya fedha kwa kufanyia vitu sahihi. Ahsante sana kiongozi.
 
Nitaendelea kupitia comment tarehe 2 nitamchagua mmojawapo achukue 100,000/=
 
Habari mkuu..

Nina matatizo makubwa sana ya kifamilia, Mama yangu yupo polis mwezi unaisha huu sababu ya kupita eneo la shamba la mwekezaji wakati mimi nipo chuo na nimekosa mkopo mambo yameenda ndivyo sivyo..

Nimekosa hata nauli ya kwenda kumsabahi mama yangu likizo hii fupi..ingawaje wajomba zangu wanahangaikia atoke natumai watafanikiwa ,tatizo na wao mifuko imekauka..

Hali hii ilipelekeage niandike uzi huu

Ninahitaji mkopo wa Tsh 350,000 , dhamana vyeti vyangu vya elimu

Naomba msaada wako mkuu kama utaguswa ..nisingependa kushindanishwa ..
 
Tungeruhusiwa kupiga kura ningempigia huyu. By the way upo chuo gani.
 
ningelipa kodi ya nyumba niache kumkwepa mwenye nyumba wangu
 
baada ya kusoma hili bandiko lako, umenifanya nikafikiria vitu vingi chanya ambavyo ningeweza kufanya kwa kutumia Tsh 100,000. Mwaka 2018 ntajitahidi niwe na matumizi mazuri ya fedha kwa kufanyia vitu sahihi. Ahsante sana kiongozi.
shukrani kiongozi
 
Binafsi nimependa hili jambo na nina imani utatekeleza ulichoahidi.

Na hili likifanikiwa najua kuna wengi wataguswa na wakaiga mfano wako.

Kila la kheri
 
Nashukuru sana mkuu nitatekeleza nilichokiahidi hapa tarehe 2 kwa ushahidi kabisa
 
Because it is the end of the year give away, better you provide the amount before this year ends.

Otherwise, better you call it Begin of the year Give Away.
 
Habari mkuu..

Nina matatizo makubwa sana ya kifamilia, Mama yangu yupo polis mwezi unaisha huu sababu ya kupita eneo la shamba la mwekezaji wakati mimi nipo chuo na nimekosa mkopo mambo yameenda ndivyo sivyo..

Nimekosa hata nauli ya kwenda kumsabahi mama yangu likizo hii fupi..ingawaje wajomba zangu wanahangaikia atoke natumai watafanikiwa ,tatizo na wao mifuko imekauka..

Hali hii ilipelekeage niandike uzi huu

Ninahitaji mkopo wa Tsh 350,000 , dhamana vyeti vyangu vya elimu

Naomba msaada wako mkuu kama utaguswa ..nisingependa kushindanishwa ..
Pole sana mkuu, muombe Mungu atamsaidia bi mkubwa. trudie nadhani ukitoa msaada hapa Mungu atakubariki sana
 
Back
Top Bottom