Kikwete kukoseshwa nafasi ya kuwania urais mwaka 2010 ni vibaya kama vile ilivyo vibaya mtu yeyote, akiwamo Shibuda, kunyimwa nafasi ya kuwania urais.
Kwa "kukoseshwa nafasi ya kuwania urais" namaanisha kukoseshwa nafasi hiyo ndani ya CCM.Ushindi wa kweli dhidi ya Kikwete ni pale atakapopewa nafasi ndani ya CCM na kushindwa kupata wajumbe wa kutosha, au kupata wajumbe wa kutosha na kuiwakilisha CCM lakini kushindwa kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu.Ushindi mwingine wowote utakaohusisha kumkatalia kabisa Kikwete kushiriki katika mchakato huu utampa nafasi Kikwete kuweza kusema kuwa hakushindwa kihalali.
Swala kubwa ni kwamba, je, tumedhamiria kusimamia demokrasia kwa kiasi gani? Tukianza kuyumbishwa na hizi habari za "mgawanyiko" ndipo tunapoanza kufikiria kwamba "Watuhumiwa wa EPA hawashitakiki kwa maana wakishtakiwa nchi haitatawalika".
Utawala wa sheria, demokrasia na misingi ya utaifa visimame juu kuzidi kitu chochote, ukiwamo uoga wa kupandikizwa na wachache.
Waacheni CCM waamue kidemokrasia bila mizengwe, kama wanamtaka Kikwete sawa, kama wanamtaka Shibuda sawa, kama wanamtaka Lowassa sawa.Halafu wawaachie Watanzania wafanye uchaguzi, liwalo na liwe al muradi limekuwa kidemokrasia ya kweli.
Tusije kuwa kama Wamarekani ambao waliingia mashariki ya kati kwa mbiu ya kutaka kuleta demokrasia, sasa wanaona demokrasia kwa waarabu inaweza kumaanisha wananchi kuwachagua vyama vyenye mlengo wa kigaidi, wanaweza vizingiti katika demokrasia hiyo.
Bila kumuwekea njama Kikwete, tutake demokrasia ishinde.Kama kuna haja ya kuwaelimisha wananchi kuhusu uozo wa Kikwete na CCM na ufanyike kidemokrasia, kama kuna sababu ya kutotaka Kikwete asiwekewe njama za kumzuia kuwania urais, iwe ni kutokana na kusimamia demokrasia na haki ya Kikwete kuwania urais, siyo kwa sababu ya mbegu za uoga zinazopandikizwa na wasioweza kukubali ukweli na gharama ya kweli ya demokrasia, endapo tuna harara ya kumuonea imani Kikwete, basi imani hii itokane na sababu za msingi.