Elections 2010 Endapo Kampeni ya kumzuia JK kugombea 2010...

Elections 2010 Endapo Kampeni ya kumzuia JK kugombea 2010...

Kama ni hivyo ya nini kufanya uchaguzi nakupoteza mapesa ikiwa bila fulani ka nchi hakitawaliki?
 
Endapo kampeni ya kumzuia JK kuwa mgombea kwa tiketi ya CCM 2010 itafanikiwa Taifa letu litakuwa matatani kwani itakuwa ni mgawanyiko ambao Taifa haliwezi kustahimili. Kwa ajiili ya amani, umoja, na mshikamano vyovyote vile ni lazima Kikwete awe mgombea wa CCM. Nje ya hapo Nchi yetu itayumba.

Think you are doing that history paper ambapo uliulizwa "discuss how the British used indirect rule in colonial Africa compared to the system of assimilation used in French colonies".

Nina kupata kwa mbali, hebu fafanua kuwa kwa vipi nchi itayumba? inawezekana tupo pamoja.

Naomba FMES utoa comments zako na Mchungaji Modest atoe uchambuzi wa mafanikio and its qualities ya CCM nchi ya Kikwete against targets.
 
Endapo kampeni ya kumzuia JK kuwa mgombea kwa tiketi ya CCM 2010 itafanikiwa Taifa letu litakuwa matatani kwani itakuwa ni mgawanyiko ambao Taifa haliwezi kustahimili. Kwa ajiili ya amani, umoja, na mshikamano vyovyote vile ni lazima Kikwete awe mgombea wa CCM. Nje ya hapo Nchi yetu itayumba.

Think you are doing that history paper ambapo uliulizwa "discuss how the British used indirect rule in colonial Africa compared to the system of assimilation used in French colonies".

Huu ni uoga wa mabadiliko Mwanakijiji
 
Okay, tuje Marekani sasa na hii ya change change change.....zaidi ya kumchagua raisi chotara, ni change gani watu wanayotegemea? Kwamba serikali itaanza kulipia car note na mortgage note zao kila mwezi na kuwawezesha watu kubakiza hela nyingi za matumizi hence kuboresha maisha zao au?

Au ndio yale yale ya kuibuka na "vague statement" na kuchota akili za watu ili wakupigie kura uwe raisi? Ni change gani unapoajiri karibu robo tatu nzima ya timu yako kutoka katika utawala wa raisi mstaafu? Is that change we can believe in?

Can we take this to where it belongs na hapa tukaendelea na mambo ya JK?

Maana hata raisi hajaapishwa watu mmeanza criticism. Kumbuka during the camapain no one mentioned serikali itaanza kulipia car note na mortgage note zao kila mwezi na kuwawezesha watu kubakiza hela nyingi za matumizi hence kuboresha maisha zao au? Naona tuishie hapa au tukaendelee kule kule kwa siku zote.

JK hana mpya zaidi ya upopulist na kuzungukwa na watu wanaopenda kumsifia. I wonder if he do even care of his own legacy after retirement. Hivi huyu jamaa amewahi hata kuandika article gazetini? leave alone kitabu au kijimakala
 
Nijuavyo mimi ni kwamba lile kundi la mafisadi ndani ya CCM wanafurahia trend ya huu mjadala kweli kweli. Tunapojadili tukumbuke pia ndani ya CCM kuna ambao ni worse off 100x kuliko huyu JK na ndio hao wako nasi hapa JF kuhakikisha JK is finished b4 2010.

Ni kweli nchi haitayumba lakini JamiiForum itafungiwa, maandamano yote ya walimu, wanafunzi, wastaafu wa EAC, TRL, nk. yatapigwa marufuku. Waandishi watapewa kibano, magazeti yatafungiwa, viongozi wa upinzani wakipiga kelele watasweka rumande, wabunge wataambiwa wafunge midomo yao. Mashirika kama Hakielimu yatafungiwa. Kina mama Killango na timu yake wataambiwa either wabaki CCM au wafunge midomo.

Hapo sasa nchi itatulia kwani kutakuwa na amani na utulivu tunaopigania; hakutakuwa na migomo tena, wala uchochezi kutoka media, wala kuwachafulia waheshimiwa majina kwa kuwaita mafisadi, nk.

Viva demokrasia - ondoa Kikwete - viva Lowassa and company - Viva ufisadi! Vicious circle!!

Kikwete ni kweli ni failure lakini bado sijamkatia tamaa. Naona kama iko siku atakubali kuitikia sauti ya watu! bado nina matumaini kidogo japokuwa yanafifia kila kukicha!
 
Tuambieni RAIS wetu ni lipi limemshinda na lilitakiwa lifanyike vipi. Ni wapi ametoa maamuzi yanayokinzana na KATIBA yetu alooapa kuilinda?
 
Nijuavyo mimi ni kwamba lile kundi la mafisadi ndani ya CCM wanafurahia trend ya huu mjadala kweli kweli. Tunapojadili tukumbuke pia ndani ya CCM kuna ambao ni worse off 100x kuliko huyu JK na ndio hao wako nasi hapa JF kuhakikisha JK is finished b4 2010.

Ni kweli nchi haitayumba lakini JamiiForum itafungiwa, maandamano yote ya walimu, wanafunzi, wastaafu wa EAC, TRL, nk. yatapigwa marufuku. Waandishi watapewa kibano, magazeti yatafungiwa, viongozi wa upinzani wakipiga kelele watasweka rumande, wabunge wataambiwa wafunge midomo yao. Mashirika kama Hakielimu yatafungiwa. Kina mama Killango na timu yake wataambiwa either wabaki CCM au wafunge midomo.

Hapo sasa nchi itatulia kwani kutakuwa na amani na utulivu tunaopigania; hakutakuwa na migomo tena, wala uchochezi kutoka media, wala kuwachafulia waheshimiwa majina kwa kuwaita mafisadi, nk.

Viva demokrasia - ondoa Kikwete - viva Lowassa and company - Viva ufisadi! Vicious circle!!

Kikwete ni kweli ni failure lakini bado sijamkatia tamaa. Naona kama iko siku atakubali kuitikia sauti ya watu! bado nina matumaini kidogo japokuwa yanafifia kila kukicha!

anyways mi hata mngeniambia tusimpe tena kikwete kuongoza nchi KESHO ningeunga mkono maana hiyo miaka miwili naona kama jehanamu kila kitu vululuvululu, maisha magumu, migomo, siri za serikali njenje basi tabu tupu hii inaonyesha ile 80% ya watanzania imeshuka na kufikia 20% yes naishi na jamii na nimeliona hivyo hata vijijini, na siri kuvuja namna hiyo means hata watu wake hawamfagilii, na njia ni CCM kumuunga mkono ili arudi angalao kwenye 50% hapo wapambane nani mtu mzuri katika kuiba kura sasa kama KUNA wa CCM hawamtaki mi naona hana haja wa kujichosha atakufa tu kwa pressure kama sio kwa ndege kwa kusafiri kukimbia mijigomo na mijilalamiko au kesha tuzira maana siku hizi hakemei chochote yuko tuuuu
 
Jamani kama watanzania wangekuwa wameridhika na utendaji wake kusingekuwa na migomo lukuki namna hii na malalamiko mengi hivi. hali iliyopo sasa ni alama ya nyakati kwamba wananchi washamchoka wanataka mbadala hawana matumaini nae tena. akitaka aheshimiwe ni kuacha kugombea tena 2010
 
Endapo kampeni ya kumzuia JK kuwa mgombea kwa tiketi ya CCM 2010 itafanikiwa Taifa letu litakuwa matatani kwani itakuwa ni mgawanyiko ambao Taifa haliwezi kustahimili. Kwa ajiili ya amani, umoja, na mshikamano vyovyote vile ni lazima Kikwete awe mgombea wa CCM. Nje ya hapo Nchi yetu itayumba.

Think you are doing that history paper ambapo uliulizwa "discuss how the British used indirect rule in colonial Africa compared to the system of assimilation used in French colonies".

Mwanakijiji, mkataba wa ajira unaongezwa upon good performance sasa kama kama performance si nzuri halafu unaongeza muda wa muajiriwa huko ni kubahatisha na ikiwa mwajiriwa atavuruga zaidi baada ya kuongezewa mkataba aliyempa mkataba mpya ndiye alaumiwe.

Suala la Taifa kushindwa kuhimili halipo na halitakuwepo. Kama mataifa dhaifu ya Afrika yameweza kuvuka sisi kwa nini tusivuke? Vinginevyo ifanyike jitihada za makusudi za kutuvuruga. Mbona Afrika Kusini wameweza na wamevuka nao ni wajuzi0juzi tu, Kenya, Burundi, Liberia nk.

Kuna watu walituambia hivyo hivyo kwa habari ya kukamatwa kwa Mafisadi ati ooh, uchumi utayumba, ooh ... HAkuna kitu kama hicho ni vitisho tu. Sisi ni taifa na tukumbuke mabadiliko ni lazima kama haitatokea wakati huu itatokea wakati mwingine. CHANGES ARE INEVITABLE.

THE ONLY THING TO FEAR IS FEAR!
 
Watanzania wamechoka na slogans za kale. Kuna nyimbo nyingi SISIEMU inapenda kuimba sana hasa inapokaribia kipindi cha chaguzi zozote zile kama shina, kata, jimbo n.k nyimbo hizi huwa zinazungumzia AMANI na UTULIVU. Ni kweli watanzania tunapenda Amani na Utulivu, lakini si kweli kwamba amani itatoweka pale SISIEMU itakapotolewa madarakani. Hii imekuwa ni danganya toto tangu enzi hizo. Wananchi wanatakiwa kuamka kifikra, mawazo, kisiasa, kiuchumi, kielimu n.k Hatuwezi kudanganywa kama watoto kwa kutumia hizo nyimbo ili mradi SISIEMU iendelee kukaa madarakani.

Nakumbuka kipindi cha kampeni cha uchaguzi mkuu nchini Marekani. Chama tawala cha Republican wakiongozwa na John McCain walitumia mbinu hizi kama za SISIEMU kueneza propaganda za kijinga. Ooh Obama ni Socialist, muislam, ooh atapandisha kodi, ooh hataweza kupambana na magaidi. Chama pinzani cha DEMOCRATS kikiongozwa na Barack Obama kilizipangua propaganda hizo kwa kuwaelimisha wamarekani na kueleza ukweli dhidi ya hizo propaganda. Na wamarekani wadai kuwa Rais Mteule Obama aliendesha kampeni safi yenye heshima kuliko mgombea yeyote katika historia ya nchi hiyo. Lakini kuna sentensi moja muhimu aliwahi kuisema na ninanukuu "THE POWER WON'T CONCEDE WITHOUT FIERCE FIGHT"
Samahani kwa kutoka nje ya thread lakini Bold sentence ndiyo ya muhimu katika hii mada. SISIEMU haiwezi kukubali kuachia madaraka bila FIERCE FIGHT. Pamoja vitisho na propaganda za uongo za kuwagawa wamarekani katika uchaguzi wao still walimchagua Obama kuwa Rais wao. Nasi hatuna budi kutojali hizi propaganda na nyimbo nzee za CCM za kuwagawa watanzania.

Huu ni wakati wa mageuzi na kuna kila ishara inaonyesha hivyo. Ni vyema watanzania wapenda haki na maendeleo kutumia vyema mwanya huu. CCM imechoka na inahitaji ukarabati wa hali ya juu. Na fundi wa kufanya marekebisho hayo bado yuko chuo kikuu cha ufundi. Na kwa bahati mbaya chuo hicho ni mojawapo ya vyuo vilivyofungwa kutokana na migomo. Hivyo wanahitaji kukaa pembeni hadi huyo fundi atakapo-graduate.

SAA YA MAGEUZI NI SASA.
 
Endapo kampeni ya kumzuia JK kuwa mgombea kwa tiketi ya CCM 2010 itafanikiwa Taifa letu litakuwa matatani kwani itakuwa ni mgawanyiko ambao Taifa haliwezi kustahimili. Kwa ajiili ya amani, umoja, na mshikamano vyovyote vile ni lazima Kikwete awe mgombea wa CCM. Nje ya hapo Nchi yetu itayumba.

Think you are doing that history paper ambapo uliulizwa "discuss how the British used indirect rule in colonial Africa compared to the system of assimilation used in French colonies".

Mwanakijiji umekata tamaa. Hakuna litakalo tokea hayo mawazo ni mawazo ya walioshindwa kufikiri na kikomo cha fikra. kikwete au CCM sio muhimili wa amani tanzania, Tanzania ina amani na mambo yatakuwa shwari with/without kikwete na CCM. wao wakiamua (CCM) kugombana au kuleteana ufa hayo ni mambo ya chama chao.
Woga ni chanzo cha kushindwa.
kikwete kakumbatia wezi nchi inaangamia kuna ufa gani zaidi ya huu wa umasikini. Mwache atoke, wacha wachapane, wacha woga kuwa mpiganaji wa nchi yako na kizazi kijacho wa ukweli sio umbili mbili.
 
Tanzania bila CCM na isiyo na mafisadi inawezekana kabisa. Matatizo makubwa yanayoikabili nchi yetu sasa hivi mengi yamesababishwa na CCM na mafisadi wao waliojaa ndani ya chama na serikali. CCM kwa sasa haina tena uwezo wa kuiongoza Tanzania ni wababaishaji tu na wanahakikisha wanalinda maslahi yao ya kuendelea kuwa madarakani.
 
Tanzania ina matatizo makubwa sana, tena mengi mno. Tatizo nambari moja ni humu kwenye mtandao watu kujisahau na kudhani kila Mtanzania ana upeo wa kupambanua mambo kati walivyo wana JF. Ukweli ni kwamba "mindsets" za Watanzania bado ni za kizamani mno.

Na ndio maana hao viongozi wetu wala hawakosi usingizi eti kwa kuogopa hawatapigiwa tena kura. Watanzania wapiga kura wengi wao wako vijijini, na wale wa mijini wengi ni wale watu wa hali ya chini.

Jiulize kama kweli kuna mwamko kwa Wananchi, mbona majimbo yote ya uchaguzi ya Dar es Salaam yako mikononi mwa CCM? Na Dar es Salaam tunaamini ndiko kwenye watu walipevuka zaidi kisiasa? Tatizo liko wapi? Je ni wapinzani kutokuwa na nguvu za kutosha kuwashawawishi wananchi wawachague, au hawana pesa za kutosha kutoa rushwa na vitenge na khanga?

Watu wenye uelewa wa mambo wengi wao huwa hawaendi hata kupiga kura, wala hawahudhurii mikutano ya kampeni.
 
Kama kichwa cha habari cha thread ilivyo ndio madhumuni ya mjadala huu... basi sisi sio wana-demokrasia... huwezi kujadili kumzuia Raia wa Tanzania kutotekeleza haki yake ya kuchagua/kuchagulia kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi!

Dawa tafuta ya kushindana naye!
 
Well, angalau umejadili kichwa cha habari. Ndio maana imesemwa "Jadili".! Good job.
 
Kwa kweli miaka 3 ya awamu ya nne watu wengi hawajaridhika na uongozi. Jk asigombee tena watu watamheshimu kama muungwana na rais wa kwanza tz kukubali kushindwa.kuna watu wenye uwezo kuwa ma rais ila ccm ilivyo haitaruhusu wagombee.ccm itampitisha jk na kura zitaibiwa kama kawaida aendelee miaka mingine 5.naona maovu awamu hii ni mengi mno. Mungu atusaidie.
 
Kikwete hawezi kuondoka madarakani kwa kelele za JF wala chuki za kupandikizwa. Poleni sana!
 
Tanzania bila CCM na isiyo na mafisadi inawezekana kabisa. Matatizo makubwa yanayoikabili nchi yetu sasa hivi mengi yamesababishwa na CCM na mafisadi wao waliojaa ndani ya chama na serikali. CCM kwa sasa haina tena uwezo wa kuiongoza Tanzania ni wababaishaji tu na wanahakikisha wanalinda maslahi yao ya kuendelea kuwa madarakani.

Mimi nisingependa ku-single-out CCM... kwa kuwa kwa idadi ya wapiga kura waliwaweka viongozi madarakani kwa vipindi vyote... utagundua kwamba makosa ni yetu sote... maana kutoka wakati huo mpaka sasa CCM ndio jamii yenyewe...

Dawa sio kutafuta mchawi dawa ni kwamba jamii nzima ibadilike...

Ndio maana ya thread moja kwamba huwezi kubadilisha mifumo ya Tanzania kwa haraka kama hatutaomba CCM igawanyike vipande vipande ... bila hivyo ... haliwezi tokea lolote...

Kwa sasa CCM ndio yenye majority... na they only way kuondoka ni CCM yenyewe kuvunjia kama ANC... ikiwezekana.

Sasa kulia CCM CCM haisaidii hata kidogo...
 
yeye sio mungu na tanzania sio mali yake! Tanzania ilikuwepo kabla yake na itakuwepo baada yake. Tanzania sio ya mtu mmoja. Tanzania ni ya watu milioni 38-40. Hii dhana ya kumtegemea mtu mmoja na bila yeye hatuwezi ku survive ni dhana ya kichovu. Mimi sijali kama chama chake kitamteua kugombea tena au vipi. Kwanza sijui hata utaratibu wao wa kuchagua wagombea ukoje. Ninachojali mimi ni kupata mgombea mbadala ndani au nje ya ccm mwenye sifa za uongozi na aliye na rekodi ya utendaji wa kazi wenye matokeo mazuri. Hii sio guarantee kwamba mtu huyo atakuwa raisi bora (kuliko kikwete) lakini angalau tutakuwa na matumaini halisia kuwa anaweza kuja kufanya kazi nzuri.

Narudia tena. Tanzania sio mali ya mtu mmoja na haitegemei mtu mmoja kuiongoza. Kikwete na ccm ni binadamu kama sisi wengine na wala sio wateule wa mungu walioletwa kuja kuongoza tanzania (kuna baadhi ya watu wanaamini hivyo). Waondoke tu na sisi tutakuwa just fine.

wewe mpaka leo hujui kama tanzania ni mali ya watu ? Uko wapi wewe unataka kifanyike nini mwaka 2010 ndio uamini tanzania inamilikiwa na mtu na sio hao watu 40 unaowataja hapo ??
 
Back
Top Bottom