Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 59,045
- 94,974
Kwenye manunuzi huwa hatuangalii bei peke yake labda uwe mwehu wa kutupwa! Kuna factors nyingi zinakua considered na mara nyingi price inakua ndio ya mwisho, mnaweza mka-negotiage price.
Sasa, tunaambiwa kuwa Kivuko kipelekwa Kenya kwenye ukarabati kwa Bei ya 7.5B kwakua wale competitors wa ndani wao walikua na bei ya juu, japo binafsi sijasikia hio bei ya juu ilikua ngapi.
Kwa mtazamo wangu, ni wa kwangu siyo wako; Endapo kivuko kingekarabatiwa hapa hapa Bongo. Machache yafuatayo yangesaidia sana sana kuziba hio "Excess";
1. Hizi 7.5B au zaidi pengine 75% ingebaki ndani ya nchi na hivyo kuongeza mzunguko wa fedha.
2. Baadhi ya materials zingenunuliwa humu humu nchini na hivyo kuboresha mzunguko wa biashara na viwanda.
3. Vijana wetu na Mainjinia wetu wangepata fursa ya ku-practice kile walichosoma.
4. Ustawi wa jamii, hapa nazungumzia category mbili, ya kwanza niwaajiriwa ambao mishahara yao inapita kwenye mabenki na wangekatwa Kodi ambayo ingeinufaisha serikali na pili, ni wale Mama Ntilie wa eneo husika at least wangekua na uwezo wa kuendelea kuuza vyakula vyao.
5. Kampuni ambayo ingepewa tender hio ingelipa Kodi, Kodi ambayo ingeingia serikalini na kusaidia kwenye sector nyingine.
7. Usimamizi wake wakati wa Ukarabati ungekua rahisi na madhubuti kuliko itakavyokua huko Kenya ambako itabidi Kila wakati wasimamizi kutoka Tanzania wataenda, mnakumbuka kwenye Ndege? Kuna Watanzania wanaendaga huko majuu kukagua! Hili halikua na ulazima.
8. Kwa hali hii au Kwa kiswahili cha Kawaida ni kwamba, Tanzania imeipa Kenya 7.5b ambazo ingeweza kuzitumia yenyewe.
Ruksa kuongeza na wale wakosoaji karibuni.