Endapo Simba ingempata kiongozi kama Eng Hersi, Leo hii ingekuwa ni bingwa wa Africa

babu onyango

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2023
Posts
378
Reaction score
984
Kwa miaka mitano hii ya ushiriki wa Simba kwenye michuano ya kimataifa timu yetu ya ni kama haipigi hatua. Tunaishia pale ple tu ambapo tunaishia miaka ya nyuma.

Kwa mtazamo wangu kinachotuangusha ni kuwa na viongozi wasio waadilifu, wasio na upeo mpana na mpira na wengi wao ni wazee..

Mpira wa kisasa unaitaji viongozi wanaoingia field wenyewe kusaka wachezaji Bora ili kupunguza upigaji, viongozi wenye maono na wanaojua nini wanataka wa achieve.

Simba tumechagua viongozi wazee wasio elimi na uelewa wa kutosha na mpira.

Tutendelea kuwalaumu Caf wanawapendelea utopolo kwa kuwapangia timu vibonde huku utopolo wazidi kupanda viwango kila kukicha na sisi tumegota palepale.

Siku tukija kushituka tutawakuta utopolo ni mabingwa wa Africa

Nguvu moja[emoji123]
 
Umenena vyema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila Ni kweli....Mfano Kama Mangungu yaani hata sijui anakuwaje kiongozi wa football...anakuwa na mihemko Kama sisi mashbiki......Sasa kweli mwenyekiti anaweza kuongea ujinga eti wachezaji wanaumizwa kwa makusudi kweli....Pale angetoa darasa kwa wachezaji wote kwamba walindane,waamuzi watoe adhabu Kali kwenye matendo Kama Yale kwa mchezaji yeyote atakayekuwa anahatarisha usalama wa wenzie,mwisho tff na bodi ya ligi wareview matkio hayo ikiwezekana yaongezewe adhabu.....Mangungu Ni taktaka tu mi nikimwonaga naona Ni mtu hivyo sana
 
Simba inaendeshwa kwa akili za mtu mmoja tu. Na wakati Yanga inaendeshwa kama taasisi.
 
Una uhakika aliyesema Yale ni Mangungu? Inawezekana simu yake alichezea mjukuu!
 
Simba inaendeshwa kwa akili za mtu mmoja tu. Na wakati Yanga inaendeshwa kama taasisi.
Utopolo bhana[emoji1787][emoji1787][emoji1787] yaani mnajiona kama Al ahly.. mnajiona nyie ndio mmefanikiwa balaa kumbe haya ni mambo ya upepo tu..
 
Tabia ya kumpromote mtu moja wakati taasisi ni syndicate ya watu wengi ni ushenzi na ina shusha morale ya viongozi wengine. Uchawa umekuwa tatizo kwenye nchi yetu, yaani mtu mmoja anatazamwa kama mtenda muujiza what a stupid mind, simba anatengenezewa conspiracy kuwa sijui nini wala nn ujinga mtupu.
 
Eng. Hersi ni alama ya mapinduzi kwa viongozi katika soka la Bongo. Utendaji kazi wake na ushiriki wake kwa kila tukio linalohusu klabu ni chachu ya mafanikio yake.
Ni mechi gani ya Yanga usimuone Hersi?
Kuendesha klabu sio kukaa ofisini au kusafiri kila siku mara uko kwenye training gani huko na Wenger (Try again na wenzie)
Wakati mwingi yupo na kikosi kutoa hamasa, timu ikishinda au kushindwa yupo kuhamasisha!
Mafanikio hayaji kirahisi, Hersi ni mchapa kazi hodari. Anastahili sifa na pongezi.
 
Naunga mkono hoja
 
Kuna kitu unapaswa kujifunza kuhusu mpira wa miguu. Kwa maoni haya unaonekana hujui soka, japo ni shabiki wa mpira.

Zitazame timu zilizo kwenye super cup, halafu uone hatua iliyopigwa na Simba ndani ya miaka mitano.

Hatua ya robo fainali ya ACL huwa inachezwa na timu bora tupu, siyo Shirikisho ambako hata timu inayoshuka daraja inacheza.

Kwa hiyo Simba kucheza robo fainali sio hatua ndogo, na ni mchakato mzuri wa kuyaendea mafanikio makubwa.

Kwani Mamelody ana miaka mingapi bila kuwa bingwa ACL? Kutwaa ACL siyo suala la kulala na kuamka.

Huyo Hersi aliyeshindwa kununulia wachezaji wake viatu vya kuchezea kwenye mvua kwenye mechi ya fainali hadi wakafungwa ana lipi la maana kafanya hadi liitwe mafanikio makubwa?

Ova
 
Kumbe eng kazi yake nyingine ni kununulia wachezaji viatu ??? [emoji1787][emoji1787][emoji1787] kwahiyo pale simba nani anakazi ya kununulia viatu wachezaji MO au mangungu ??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…