Endeleeniu kuijadili Yanga badala ya kuboresha vikosi vyenu ila msije kusema GSM ananunua marefa

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Makolo wako busy kuijadili Yanga badala ya ku-focus madhaifu ya timu yao ambayo bado inaendelea kujitafuta na haina uhakika wa matokeo mazuri. Maneno ni mengi ila yote msingi wake ni kujifariji wakijiaminisha Yanga sasa basi na kwamba imeshuka kitu ambacho sio kweli.

Wakati wao wako busy kujijadili Yanga, Yanga wao wako busy kurekebisha makosa yao na baada ya muda matokeo yataonekana uwanjani na hii ni kanuni ya kawaida kabisa katika maisha.

Tukumbuke, hata msimu uliopita, Yanga alifungwa na Ihefu huku Yanga wakionekana kutocheza vizuri na hata baadhi ya mechi zingine walikuwa wanapata matokeo kwa taabu, ila hali hiyo haikuwa endelevu na baadae walifanya vizuri na ubingwa walibeba. Moja ya sababu ilikuwa ni kucheza mechi nyingi mfululizo zikiwemo za ndani na zile za kimataifa. Hivyo, leo hii hakuna kitu cha ajabu sana zaidi ya maneno ya ushabiki lakini wajue maneno hayachezi bali ni maandalizi kwa maana ya kujipanga upya.

Angalizo: Kwakuwa Yanga hawajatetereka na wanaendelea kujipanga huku nyie mmekali majungu na umbea, vipigo vya mfululizo vikiendelea, msije tena kuja kusema GSM ananunua marefa au sijui Yanga wana majini , n.k.

Time will tell.
 
Kweli tunakosea mkuu
 
Attachments

  • Screenshot_20241109-110340_1.jpg
    Screenshot_20241109-110340_1.jpg
    246.3 KB · Views: 4
Kushindwa na kushinda ni sehemu ya mchezo
 
Attachments

  • Screenshot_20241108-120224_1.jpg
    Screenshot_20241108-120224_1.jpg
    260.6 KB · Views: 6
Makolo wako busy kuijadili Yanga badala ya ku-focus madhaifu ya timu yao ambayo bado inaendelea kujitafuta
Kwa sasa timu inayojitafuta ni Yanga. Yanga inatakiwa kufocus madhaifu yake
 
Tabora Boys
Tabora boys yupo nafasi ya ngapi kwenye msimamo?

Yanga inayojitafuta hipo nafasi ya ngapi?

Yanga ni bingwa wa ngao ya jamii Tabora boys ni bingwa wa nini?

Ukiachilia mbali ligi kuu Yanga anashiriki klabu bingwa afrika,

Hao Tabora boys uliowataja wanashiriki kombe gani lingine ukiachilia mbali ligi kuu?

Nani kati ya hao wawili anajitafutia?
 
Ni lini Simba wamesitisha kufanya mazoezi kisa Uto imefungwa? Kwa hiyo sisi mashabiki unatuona kama ni benchi la ufundi la Simba . We kweli utopolo. Mnajidanganya kwamba nyinyi ndio mnaendelea kujiboresha halafu wengine wamebweteka. Yaani mnaleta mazoea sijui ya msimu uliopita. Uto ni timu ya kawaida kama zilivyo timu zingine na inaweza kufungwa muda wowote, mkiishi Kwa mazoea msimu huu uto itapigania nafasi ya tatu.
 
Ukiachilia mbali ligi kuu Yanga anashiriki klabu bingwa afrika,
Hao Tabora boys uliowataja wanashiriki kombe gani lingine ukiachilia mbali ligi kuu?
Hata Marumo Gallants walishiriki kombe la shirikisho, wakafika nusu fainali, lakini katika msimu husika wakashuka daraja
 
Makolo wako busy kuijadili Yanga badala ya ku-focus madhaifu ya timu yao ambayo bado inaendelea kujitafuta na haina uhakika wa matokeo mazuri. Maneno ni mengi ila yote msingi wake ni kujifariji wakijiaminisha Yanga sasa basi na kwamba imeshuka kitu ambacho sio kweli.

Wakati wao wako busy kujijadili Yanga, Yanga wao wako busy kurekebisha makosa yao na baada ya muda matokeo yataonekana uwanjani na hii ni kanuni ya kawaida kabisa katika maisha.

Tukumbuke, hata msimu uliopita, Yanga alifungwa na Ihefu huku Yanga wakionekana kutocheza vizuri na hata baadhi ya mechi zingine walikuwa wanapata matokeo kwa taabu, ila hali hiyo haikuwa endelevu na baadae walifanya vizuri na ubingwa walibeba. Moja ya sababu ilikuwa ni kucheza mechi nyingi mfululizo zikiwemo za ndani na zile za kimataifa. Hivyo, leo hii hakuna kitu cha ajabu sana zaidi ya maneno ya ushabiki lakini wajue maneno hayachezi bali ni maandalizi kwa maana ya kujipanga upya.

Angalizo: Kwakuwa Yanga hawajatetereka na wanaendelea kujipanga huku nyie mmekali majungu na umbea, vipigo vya mfululizo vikiendelea, msije tena kuja kusema GSM ananunua marefa au sijui Yanga wana majini , n.k.

Time will tell.
Kurekebisha makosa gani wakati huo huo unadai hawajaterereka?Msimu uliopita baada ya mechi 10 walikuwa na pointi 27 magoli 30 ya kufunga na 6 ya kufungwa.
Msimu huu baada ya mechi 10 wana pointi 24 magoli 14 ya kufunga na 4 ya kufungwa.Unaona wapo sawa na Msimu uliopita?
Wacha kuficha udhaifu wa timi yako kwa kujaribu kuwapa Simba nasaha.
Wachezaji muhimu wanakesha Kitambaa Cheupe Club na fomu na stamina imepungua.Visingizio havijengi.
Gamondi kaanza kufungua mdomo kwamba wachezaji maarufu wanalindwa na uongozi. Hata nidhamu uwanjani kadi 14 za njano na moja nyekundu kwenye mechi 10 sio takwimu nzuri za nidhamu.
 
Hata Marumo Gallants walishiriki kombe la shirikisho, wakafika nusu fainali, lakini katika msimu husika wakashuka daraja
Kwahiyo marumo gallants kushuka daraja ndio kombe analoshiriki Tabora boys ukitoa ligi kuu?
 
Hao wanao sherehekea kufungwa yanga, hawana uhusiano na benchi la ufundi la yanga!
 
Kuna vitu vitatu vya msingi wewe shabiki wa nyuma mwiko unatakiwa uvijue.

1.Simba ya msimu huu ni bora mara tano ya simba ya msimu uliopita kuanzia kwenye eneo la golikipa, safu ya ulinzi, safu ya kiungo na hata eneo la ushambuliaji.

Hadi sasa hivi simba haijafungwa goli kwenye open play.

Hadi sasa hivi simba inaongoza kwa kufunga magoli mengi kuliko timu yoyote, imefungwa magoli machache kuliko timu yoyote na imekusanya point nyingi kuliko timu yoyote na ndio maana inaongoza ligi.

2.Yanga ya msimu huu imeshuka kiwango ukilinganisha na yanga ya msimu uliopita. Unazikumbuka zile tano tano kila mechi? Sasa hivi ziko wapi? Aziz ki kiwango kimeshuka,dube hamna kitu,boka hamna kitu mbio tu kama swala,aucho kashuka kiwango umri umeenda.

3.huwezi kutumia mbinu zile zile kushinda vita kumbuka wapinzani wanakusoma na wanakutafutia njia bora ya kukudhibiti so usikariri eti kwakuwa yanga msimu uliopita alikuwa bingwa na msimu huu atakuwa bingwa.
 
Kwahiyo marumo gallants kushuka daraja ndio kombe analoshiriki Tabora boys ukitoa ligi kuu?
Nimekupa hiyo ili ujue kwamba timu kuwa bora msimu uliotangulia hakuweki guarantee kwamba itakuwa bora msimu uliopo, kwamba Gallants walikuwa bora kiasi cha kupata tiketi ya kuiwakilisha South Africa katika michuano ya Shirikisho, kwa lugha nyingine walikuwamo katika top four, lakini msimu uliofuata wakashuka daraja. So, Yanga kuwa mwakilishi wa Klabu Bingwa kwa tiketi ya mwaka jana hakugaratii kuwa bora msimu huu
 
Kurekebisha makosa gani wakati huo huo unadai hawajaterereka?Msimu uliopita baada ya mechi 10 walikuwa na pointi 27 magoli 30 ya kufunga na 6 ya kufungwa.
Msimu huu baada ya mechi 10 wana pointi 24 magoli 14 ya kufunga na 4 ya kufungwa.Unaona wapo sawa na Msimu uliopita?
Wacha kuficha udhaifu wa timi yako kwa kujaribu kuwapa Simba nasaha.
Wachezaji muhimu wanakesha Kitambaa Cheupe Club na fomu na stamina imepungua.Visingizio havijengi.
Gamondi kaanza kufungua mdomo kwamba wachezaji maarufu wanalindwa na uongozi. Hata nidhamu uwanjani kadi 14 za njano na moja nyekundu kwenye mechi 10 sio takwimu nzuri za nidhamu.
Timu yako ndio mbovu mpaka juzi mlikuwa hamna hata uhakika wa kushinda na mkifungwa nyie ni kawaida kabisa.
 
Back
Top Bottom