Strong ladg
Senior Member
- Jul 15, 2021
- 170
- 445
Jana, katika pitapita zangu nikifuatilia yanayoendelea Goma, nikakutana na maoni yenye kutaja kitabu kiitwacho Enduring Lies. Nikavutiwa nacho na nikaamua kukitafuta, bahati nzuri nikakipata.
Kulingana na waandishi wa kitabu hiki, kile tunachoambiwa kuhusu mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ni tofauti na ukweli wa kilichotokea. Wanadai kuwa propaganda zilitumika kusafisha jina la Paul Kagame, ili dunia iamini kuwa yeye hakuhusika katika mauaji hayo bali ni shujaa aliyeyakomesha na kuijenga Rwanda kutoka matopeni hadi mawinguni.
Sijamaliza kusoma kitabu hiki, lakini baadhi ya madai ambayo nimekutana nayo—ambayo sikuwahi kuyasikia kabla—ni haya yafuatayo (ingawa huenda kuna watu waliokuwa wakiyafahamu, nami nikiwa sijayafahamu):
Kulingana na Onana, uongo mkubwa zaidi wa karne ya 20 ni kudai kuwa mauaji ya kimbari yalipangwa na kuratibiwa na Wahutu pekee, na kwamba wao ndio wahusika wa pekee katika mauaji hayo.
Charles Onana pia ameandika vitabu mbalimbali kuhusu Rwanda na vita vinavyoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Je unakubalina na madai ya waandishi wa kitabu cha "ENDURING LIES"?.
Asante.

- Mauaji ya kimbari ya 1994 yalikuwa kilele cha matukio yaliyoanza miaka mingi nyuma. RPF na Kagame walijipanga kwa matukio haya kwa muda mrefu kwa kushirikiana na serikali ya Museveni, ilhali jeshi la serikali ya Rwanda lililokuwa likiongozwa na Habyarimana lilikutwa halijajiandaa.
- Kagame aliamuru kushambuliwa kwa ndege iliyokuwa imembeba Rais Habyarimana. Askari wa Kagame ndio walioshambulia ndege hiyo na kusababisha kifo cha Habyarimana, si Wahutu wenye msimamo mkali kama inavyodaiwa mara nyingi.
- Kagame alichukua uamuzi wa kumuua Rais Habyarimana kwa sababu aliona kuwa hiyo ndiyo njia pekee ya kuingia madarakani, kwani hakukuwa na uwezekano wa kushinda uchaguzi kwa njia ya kidemokrasia.
- Kagame alikuwa mtumishi mwaminifu wa mataifa ya Magharibi, ambayo yaliunga mkono harakati zake tangu alipokuwa Uganda. Vilevile, mataifa hayo yalihakikisha kuwa vipengele vya Mkataba wa Amani wa Arusha vilikuwa na faida zaidi kwa RPF, ili kuwawezesha kufanya shughuli zao kwa uhuru mjini Kigali.
- Mahakama ya kimataifa iliyoanzishwa kwa ajili ya kushughulikia washukiwa wa mauaji ya kimbari hutupilia mbali ushahidi wowote unaomhusisha Kagame na mauaji hayo. Mahakama hiyo ni mojawapo ya vyombo muhimu vilivyotumika kulisafisha jina lake.
- Wandani wa Kagame wanaofahamu jinsi alivyohusika katika mauaji ya kimbari huuawa au hunusurika kuuawa hata wakiwa uhamishoni. Mfano ni Colonel Theoneste Lizinde, aliyeuawa jijini Nairobi, na Kayumba Nyamwasa, ambaye amenusurika kuuawa zaidi ya mara moja akiwa Afrika Kusini. Wote wawili walikuwa na taarifa kuhusu ushiriki wa Kagame katika shambulio la ndege ya Habyarimana. Mwingine ni Patrick Karegeya, aliyeuawa akiwa Afrika Kusini.