Eneo la Stand ya mabasi la Magufuli pakijaa, watahamishia wapi tena? Kibaha?

Nina Akili Ndogo Sana

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2026
Posts
865
Reaction score
1,125
NB: Nina Akili Ndogo Sana.

Zamani stand ilikuwa kisutu. Palipokuwa mjini sana wakapeleka Ubungo kijijini. Ubungo palivyochangamka, wakapeleka Mbezi kwa Magufuli. Mbezi kwa Magufuli kukichangamka kama Kisutu na Ubungo, watahamishia wapi?? Mile Moja Kibaha?? Na hapo pakichangamka na kuwa mjini zaidi, watahamia wapi??

Stand ya Kisutu isingefutwa, bali wangepunguza idadi ya mabasi, at least bus moja au mbili kwa kila Mkoa. Hata Ubungo vile vile wasingepafunga moja kwa moja wangeacha stand Ndogo ya buses mbili mbili au moja moja kwa kila Mkoa. Hata stand ya Magufuli ikija kuhamishwa kama zile za Kisutu na Ubungo, isivunjwe moja kwa moja bali waache stand Ndogo ya buses kadhaa. Walikosea sana kuzivunja standa za Kisutu na Ubungo kwa 100%.

Unapokuwa kiongozi ni lazima uangalie miaka 50 mbele kwa watoto na wajukuu zako na sio wewe binafsi na maslahi yako. Tanzania salama na imara ni jukumu letu sote.

~ Nina Akili Ndogo Sana ~
 
Shida hatuna viongozi wanao waza miaka 100 ijayo.

Hatuna watu wanaofikiria kesho kutwa, wao ni Leo leo

Nchi inahitaji think tank wake na wasiwe viongozi wakubwa.

Leo hii wanawaza kama watu walio 1970 badala ya 2050
 
NB: Nina Akili Ndogo Sana.

Zamani stand ilikuwa kisutu. Palipokuwa mjini sana wakapeleka Ubungo kijijini. Ubungo palivyochangamka, wakapeleka Mbezi kwa Magufuli. Mbezi kwa Magufuli kukichangamka kama Kisutu na Ubungo, watahamishia wapi?? Mile Moja Kibaha?? Na hapo pakichangamka na kuwa mjini zaidi, watahamia wapi??

Stand ya Kisutu isingefutwa, bali wangepunguza idadi ya mabasi, at least bus moja au mbili kwa kila Mkoa. Hata Ubungo vile vile wasingepafunga moja kwa moja wangeacha stand Ndogo ya buses mbili mbili au moja moja kwa kila Mkoa. Hata stand ya Magufuli ikija kuhamishwa kama zile za Kisutu na Ubungo, isivunjwe moja kwa moja bali waache stand Ndogo ya buses kadhaa. Walikosea sana kuzivunja standa za Kisutu na Ubungo kwa 100%.

Unapokuwa kiongozi ni lazima uangalie miaka 50 mbele kwa watoto na wajukuu zako na sio wewe binafsi na maslahi yako. Tanzania salama na imara ni jukumu letu sote.

~ Nina Akili Ndogo Sana ~
Miaka 50 ijayo stendi zitasambazwa kila maneo kupeusha msongamano
 
Kitambo ijae kutakua na plan mpya.
For now inajitosheleza,miji hupanuka so wakati wa uhitaji ukifika jambo litafanyika before tatizo lianze.
 
Stand Moja kwenye jiji kubwa kabisa Tanzania na Afrika mashariki?

Hiyo Mwanza yenyewe tu ina stand tatu
Nyegezi, Nata na Nyamhongolo
Na hili ni jiji la pili kwa ukubwa.

Hawa ndio aina ya viongozi wetu wa Leo na kesho 😀😀😀👂
 
Back
Top Bottom