NB: Nina Akili Ndogo Sana.
Zamani stand ilikuwa kisutu. Palipokuwa mjini sana wakapeleka Ubungo kijijini. Ubungo palivyochangamka, wakapeleka Mbezi kwa Magufuli. Mbezi kwa Magufuli kukichangamka kama Kisutu na Ubungo, watahamishia wapi?? Mile Moja Kibaha?? Na hapo pakichangamka na kuwa mjini zaidi, watahamia wapi??
Stand ya Kisutu isingefutwa, bali wangepunguza idadi ya mabasi, at least bus moja au mbili kwa kila Mkoa. Hata Ubungo vile vile wasingepafunga moja kwa moja wangeacha stand Ndogo ya buses mbili mbili au moja moja kwa kila Mkoa. Hata stand ya Magufuli ikija kuhamishwa kama zile za Kisutu na Ubungo, isivunjwe moja kwa moja bali waache stand Ndogo ya buses kadhaa. Walikosea sana kuzivunja standa za Kisutu na Ubungo kwa 100%.
Unapokuwa kiongozi ni lazima uangalie miaka 50 mbele kwa watoto na wajukuu zako na sio wewe binafsi na maslahi yako. Tanzania salama na imara ni jukumu letu sote.
~ Nina Akili Ndogo Sana ~