Kwanza eneo hilo kuna umeme mkubwa umepita kwa juu ya kiwanja hivho, nimeweka picha na video kuonesha hizo waya zilivyopita hapo.
Kwa nini nasema ujenzi ni wa kimyakimya? Ni kwa kuwa kuna uzio wa mabati ambao umewekwa hapo kwa wiki kadhaa kumaanisha kuwa inawezekana ndani kuna kitu kinafanyika lakini hakuna bango lolote linaloonesha kuna nini kinachoendelea.
Kingine ni kuwa kama ni ujenzi, kwa ni i eneo hilo la wazi linajengwa? Kwa nini lijengwe kimyakimya? Vipi kuhusu nyaya za umeme zilizopo hapo?
Ni vema mamlaka za Shehiya zijitokeze na kutuambia Wananchi kuwa nini kinachoendelea hapo, ili baadaye wasianze mambo ya kuunda Tume ya Uchunguzi wakati wana nafasi ya kuweka wazi mapema
Miaka kadhaa nyuma kuna Watu waliofika na kuweka uzio wa mabati hapo lakini hakuna kilichofanyika kwa kuwa ilidaiwa eneo licha ya kuwa la wazi kuna mgogoro, sasa je kinachoendelea sasa kina Baraka za Serikali au kuna watu wanataka kufanya ujanja? Na vipi kuhusu usalama wa Watu wengine kutokana na uwepo wa miundombinu ya umeme iliyopo?