Eneo lenye hatua za miguu 250 kwa120 linaweza kutoa heka ngapi?

Hatua za miguu Mita ni vitu viwili tofauti
 
Endapo kipimo cha heka kikiwa 70*70 (hatua za miguu)
Lazima mmoja adhurumike tu, nashauri ukanunue measuring tape ni shs 10,000 tu uwe na kipimo cha uhakika, au tumia simu yako kama ni ya android au windows kuna app inapima urefu humo
 
Mimi nadhani asiwe mvivu anunue tape measure ya Mita Mia 100, apime urefu na upande, azidishe alafu atafute hizo ekari hata Kwa kipimo hicho hicho cha 70x70, atapata jubu
 
Lazima mmoja adhurumike tu, nashauri ukanunue measuring tape ni shs 10,000 tu uwe na kipimo cha uhakika, au tumia simu yako kama ni ya android au windows kuna app inapima urefu humo
Kama eneo Lina changamoto ya upana na Kona Kona atafute MTU mwenye GPS dakika chache Tu amepata majibu
 
Hivi toka lini ekari moja ikawa na 4,900 square metres yaani 70m kwa 70m?
 
Asante sana mkuu nilihangaika sana na hesabu nikapata 6 acres ngoja nisubiri hesabu zaidi
Hesabu zako ndiyo sahihi, ni ekari 6.1.

Yaani unaanza kwanza unatafuta ukubwa wa ekari 1 ambayo ni 70x70= 4,900 unaweka pembeni.

Unakuja kuangalia matokeo ya ukubwa wa 250×120 ambayo jibu lake ni 30,000.

Hiyo 30, 000 unaigawa kwa 4,900.

ie:3,0000÷4,900=6.1 simple like that.
 
Hivi toka lini ekari moja ikawa na 4,900 square metres yaani 70m kwa 70m?
Tuambie ekari moja huwa ina sqm ngapi mkuu? Tuambie mkuu kwa 70mx70m =4900sqm. Na 64mx64m=4096sqm.

Tupe jibu lako mkuu huwa ina ngapi sqm kwa ekari 1 bisha kwa hoja mkuu. No reason no right to speak.
 
Kwa kawaida ekari moja ni sawa na mita za eneo 4000m2. Kwa maana kwamba hekta moja =10000m2.Na katika Hekta moja kuna ekari 2.5.(mbili na nusu)

Hiyo ya 70 ×70 =4900m2 ni vipimo vya kikoloni walivyotumia kudhurumu watu ardhi au vibarua waliokuwa wakifanya kazi kwenye mashamba yao.
Changamoto ya eneo lako ni hapo ulipotumia hatua za miguu badala ya mita. Tafta "measuring tape" ili kuwa na uhakika zaida.
 
Vipimo vya miguu hutegemea na uwezo wa kutanua msamba kwa mtu.... Msamba wa mtoto na mtu mzima tofauti... Msamba wa mrefu na mfupi tofauti.....

Anyway kama eneo haliuzwi kwa sqm ni sawa kupima kwa misamba..... Ila kwenye ujenzi/kilimo utahitaji vipimo vya metric kujua una eneo kiasi gani ili ufahamu mahitaji na matokeo ya uwekezaji wako.

Weekend njema.
 
Habari Jf. Naomba msaada wa kimahesabu ili nipate data kamili.

Endapo kipimo cha heka kikiwa 70*70 (hatua za miguu)

Je eneo lenye hatua 250 kwa 120 litatoa ekari ngapi.

Karibuni
Acre mbili na robo..... am here just for the violence
 
hili la hatua moja = mita moja ni la kubahatisha sana......huyo mtu inabidi awe mrefu kweli kweli, km ni kambilikimo tu hilo haliwezekani
 
safi kabisa, nilikuwa sijaiona hii komenti ndo maana nami nimeongea kitu kinachofanana na hiki......kupima kwa hatua ni bahatisho la kienyeji sana
 
Mnaosema eka 6, 7 na 5 mnayapata wapi majibu!? Yaani 70x 70 ikupe eka Moja halafu 250x120 ikupe eka 6!?!??

Simple n Clear, katika hivyo vipimo vyako angalia zimo 140 ngapi itakayobaki ni eka 3 naa hiyo itakayobaki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…