TANZIA eng. Felix Mlima Ngoako, Meneja wa Tanroads Ruvuma afariki dunia akishiriki mbio za hisani

Mazoezi yakiwemo ya jogging yanahitaji mhusika awe na afya njema ya moyo, jogging huongeza mapigo ya moyo hivyo kama mhusika ana shida ya moyo anaweza kupata shambulio la moyo ghafla.

Usikurupuke kuanza mazoezi hasa yanayoendana na cardiovascular fitness bila kuwa na uelewa juu ya afya ya moyo wako.
 
Meneja wa TanRoads Mkoa wa Ruvuma mhandisi Ngaile amefariki ghafla baada ya kudondoka ghafla wakati akiwa kwenye mazoezi ya mbio za hisani zilizoandaliwa Mkoani humo.
---

Songea. Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Mlima Ngaile amefariki dunia leo asubuhi baada ya kudondoka wakati akishiriki mbio zilizoandaliwa na Wiloles Foundation Marathon.

Mhandisi Ngaile baada ya kudondoka inaelezwa akiishiwa pumzi akiwa eneo la Matalawe Manispaa ya Songea na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Songea (Homso) kwa matibabu, lakini alifariki dunia.

Mkuu wa Wilaya ya Songea, Wilman Ndile amesema leo Ijumaa Januari 12, 2024 kuwa daktari amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na mwili wa meneja huyo umehifadhiwa hospitalini hapo kusubiri taratibu za mazishi kuendelea kwa kushirikiana na Tanroads makao makuu.

Akisimulia jinsi walivyoshiriki mbio hizo, mkuu huyo wa wilaya (DC), amesema leo asubuhi kulikuwa na mbio za hisani za kuchangia fedha kwa ajili ya kununua vifaa vya kuokoa maisha ya watoto wachanga katika Hospitali ya Rufaa ya Songea.

Amesema meneja huyo alikimbia mbio za kilomita tano na katika kundi lake alikuwepo yeye (DC), Katibu Tawala Mkoa na Mganga Mkuu wa mkoa huo.

“Tulikuwa tunakimbia kwa mwendo wa kawaida, ila tulipofika kilima cha Bombambili tulishangaa akipanda kwa kasi sana na sio kawaida, kwani huwa tunakimbia kila mwisho wa mwezi na tukifika hapo huwa tunatembea.

"Kabda alipata shida kwenye moyo na alipofika Matarawe aliishiwa pumzi na mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Msigwa alipiga simu kuita gari la wagonjwa na walifanikiwa kumkimbuza hospitalini, lakini kwa bahati mbaya alifariki dunia akiwa katika jengo la dharura katika Hospitali ya Homso na mwili wake umehifadhiwa hapo," amesema DC Ndile.

Amesema tayari uongozi wa mkoa umewasiliana na Tanroads Makao Makuu na taratibu zinaendelea na mazishi zinaendelea.

Mkuu huyo wa mkoa ametoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu wakiwemo watumishi wenzake na amewataka waendele kuwa watulivu na kumuombea marehemu.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Songea, Dk Majura Magafu amesema taarifa zaidi ya tukio hilo atatoa baada ya kuwasiliana na daktari aliyekuwa akimuhudumia, kwani wakati tukio linatokea alikuwa Uwanja wa Majimaji kwenye mbio hizo.

My Take
Prof.Janabi aliwahi Kuonya Watu kushiriki jogging bila kupima Afya kwani ni hatari kwa Afya.
Kuna watu watasema karogwa.

RIP Meneja
 
What CPR means?

images

cardiopulmonary resuscitation

CPR stands for cardiopulmonary resuscitation. It can help save a life during cardiac arrest, when the heart stops beating or beats too ineffectively to circulate blood to the brain and other vital organs.

sijui kama waliokuwepo kwenye tukio walijaribu hii kabla ya kuita gari ya wagonjwa
 
sasa iwekwe sheria, kila mshiriki wa marathon apimwe afya kabla ya kuruhusiwa kukimbia, kuwe na wataalam wa afya wataotoa elimu za tahadhari na huduma ya kwanza kwa washiriki kabla mbio haijaanza... sasa DC anasema mahali pa kupanda taratibu ndo engineer akaongeza spid ili amalize kisima, yaan badala ya kupanda na namba moja akapanda na namba 5... hapo lazma alipata heart attack akaanguka na kuchelewa kupata huduma ya kwanza ikawa ngumu ku reverse.
 
.....RiP Meneja....mambo ni mengi ila pumzika kwa amani
 
Meneja wa TanRoads Mkoa wa Ruvuma mhandisi Ngaile amefariki ghafla baada ya kudondoka ghafla wakati akiwa kwenye mazoezi ya mbio za hisani zilizoandaliwa Mkoani humo.
---

Songea. Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Mlima Ngaile amefariki dunia leo asubuhi baada ya kudondoka wakati akishiriki mbio zilizoandaliwa na Wiloles Foundation Marathon.

Mhandisi Ngaile baada ya kudondoka inaelezwa akiishiwa pumzi akiwa eneo la Matalawe Manispaa ya Songea na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Songea (Homso) kwa matibabu, lakini alifariki dunia.

Mkuu wa Wilaya ya Songea, Wilman Ndile amesema leo Ijumaa Januari 12, 2024 kuwa daktari amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na mwili wa meneja huyo umehifadhiwa hospitalini hapo kusubiri taratibu za mazishi kuendelea kwa kushirikiana na Tanroads makao makuu.

Akisimulia jinsi walivyoshiriki mbio hizo, mkuu huyo wa wilaya (DC), amesema leo asubuhi kulikuwa na mbio za hisani za kuchangia fedha kwa ajili ya kununua vifaa vya kuokoa maisha ya watoto wachanga katika Hospitali ya Rufaa ya Songea.

Amesema meneja huyo alikimbia mbio za kilomita tano na katika kundi lake alikuwepo yeye (DC), Katibu Tawala Mkoa na Mganga Mkuu wa mkoa huo.

“Tulikuwa tunakimbia kwa mwendo wa kawaida, ila tulipofika kilima cha Bombambili tulishangaa akipanda kwa kasi sana na sio kawaida, kwani huwa tunakimbia kila mwisho wa mwezi na tukifika hapo huwa tunatembea.

"Kabda alipata shida kwenye moyo na alipofika Matarawe aliishiwa pumzi na mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Msigwa alipiga simu kuita gari la wagonjwa na walifanikiwa kumkimbuza hospitalini, lakini kwa bahati mbaya alifariki dunia akiwa katika jengo la dharura katika Hospitali ya Homso na mwili wake umehifadhiwa hapo," amesema DC Ndile.

Amesema tayari uongozi wa mkoa umewasiliana na Tanroads Makao Makuu na taratibu zinaendelea na mazishi zinaendelea.

Mkuu huyo wa mkoa ametoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu wakiwemo watumishi wenzake na amewataka waendele kuwa watulivu na kumuombea marehemu.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Songea, Dk Majura Magafu amesema taarifa zaidi ya tukio hilo atatoa baada ya kuwasiliana na daktari aliyekuwa akimuhudumia, kwani wakati tukio linatokea alikuwa Uwanja wa Majimaji kwenye mbio hizo.

My Take
Prof.Janabi aliwahi Kuonya Watu kushiriki jogging bila kupima Afya kwani ni hatari kwa Afya.
Kuna matukio pia mtu anadondoka akiwa amesimama na kufariki.
 
Hizi marathon siku hizi watu wanakurupuka tu

Ova
Jaribu siku moja ukimbie 21km bila mazoezi au 10km tu. Nakuhakikishia hufiki 3km hutaanguka kwa heart attack ila utasimama mwenyewe kwa uchovu tu.
Ninachotaka kukwambia heart attack inapata hata mtu yuko usingizini au kakaa ofisini sio lazima ukimbie.
Kwa mwaka watu zaidi ya 100,000 wanashirikia marathon hapa Tz mmesikia wangapi wamedondoka na kufa? Je huku mtaani kwa mwaka wanadondoka wangapi na kufa?
Tuacheni na mbio zetu nyinyi kunyweni bia tu kila mtu ashinde mechi zake.
#TukutaneKili
 
Mzee mm nko physic [emoji1]
Ndomana bia inashuka tu
Kukimbia kdg,pushups,pull ups
Tosha sahv
Soka siku moja moja linapigwa kama kawaida

Mpira bball nimeacha maanake sasa hivi nikitegua ankle inachukua muda mrefu sana kukaa sawa. Acha nifukuze upepo.
 
Binaadamu tuache maringo, tuache kuonea watu wengine kisa unacheo.
Tuwatendee mama walio chini kwani maisha haya ni mafupi hakuna atakaye ishi milele.
 
Una jambo,fafanua mkuu
 
Mpira bball nimeacha maanake sasa hivi nikitegua ankle inachukua muda mrefu sana kukaa sawa. Acha nifukuze upepo.
Kuna mtaalamu mmoja alisema jogging ni useless exercise, kama sijamnukuu vibaya inaharibu au inavuruga kazi za misuli muhimu.....ni metabolic interference ya hovyo kabisa katika mwili. Nafikiri njia sahihi ni kufanya mazoezi ya kutembea tu au kunyanyua vitu vizito kiasi kwa ajili ya misuli.​
 
Back
Top Bottom