Eng. Hersi 2021: Yanga inajiendesha kwa Hasara

Eng. Hersi 2021: Yanga inajiendesha kwa Hasara

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001

Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM Eng. Hersi Said amewashukia baadhi ya wadau wa soka nchini Tanzania walioibua hoja inayogusa udhamini wa kampuni hiyo kwenye klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Hoja hiyo imeibuka kufuatia Kampuni ya GSM kuwa mdhamini ya Young Africans, Namungo FC na Coastal Union, huku ikijaribu kuisafirisha Biashara Utd kwenda Libya (safari ambayo ilishindikana).

Wasiwasi uliopo ni kwamba kama kampuni ya GSM imewekeza kwenye klabu zaidi ya moja itakua na sababu ya kushawishi upangaji wa matokeo hasa kwa timu wanazozidhamini zitakapokutana.

Hersi ameandika kuwa: ”Timu hizi zinajiendesha kwa hasara kwa miaka mingi ndio maana zimekwama. Ukisema hivi mtu anaweza asikuelewe lakini ukitazama mapato ya klabu na matumizi ndio utajua kwanini zinajiendesha kwa hasara”

”Yanga inalipa mishahara yenyewe, ina mifumo yake ya kuajiri watu sisi tuna-support tu. Yanga ni timu kubwa huwezi kufananisha na hawa makolo. Huwezi kumleta mchezaji kama Bangala halafu hajui mshahara analipwa na nani”

”Hii ni klabu kubwa, tunafanya kazi ya kurejesha heshima yake, watu waipende tena. Mechi ya juzi Yanga inafungwa goli mashabiki wanapiga makofi, tunarudisha tunafunga la pili na la tatu na bado kuna dakika kama 900 za kucheza”

”Watu wanaleta siasa chafu na mimi nasema hizi ni takataka. Mbona kampuni kama Emirates inadhamini vilabu vingi tu vinacheza Champions League. Ina maana Arsenal wakicheza na AC Milan utasema mmoja amwachie mwenzake?”

My Take
Sina My Take yeyote
 
Teh kumbuka kuna mmoja kanunua timu na kuna mmoja kajiweka mdhamini kwa mapenzi yake mwenyewe....... Alienunua lazima asake faida maana kawekeza, huyu mwingine hata asipopata faida kazi ni kwake maana hajanunua timu
 
Teh kumbuka kuna mmoja kanunua timu na kuna mmoja kajiweka mdhamini kwa mapenzi yake mwenyewe. Alienunua lazima asake faida maana kawekeza, huyu mwingine hata asipopata faida kazi ni kwake maana hajanunua timu
Unaona hii ni hoja ya kuleta Mbele za watu?
 
Anaeona anapata hasara aachie timu OKW BOBAN SUNZU wewe chawa wa mhindi muulize huyo jamaa yako hasara kaanza kupata Simba vp African Lyon na Singida utd alikua anapata faida?

Unasema unapata hasara harafu hautaki kutoka ndio yale ya kiongozi mmoja alikua anajiliza eti kazi ya urais ni ngumu kwenye uchaguzi form inatoka moja na wizi wa kura juu
 
Anaeona anapata hasara aachie timu OKW BOBAN SUNZU wewe chawa wa mhindi muulize huyo jamaa yako hasara kaanza kupata Simba vp African Lyon na Singida utd alikua anapata faida? unasema unapata hasara harafu hautaki kutoka ndio yale ya kiongozi mmoja alikua anajiliza eti kazi ya urais ni ngumu kwenye uchaguzi form inatoka moja na wizi wa kura juu
Mwekezaji katoa taarifa ya uwekezaji wake. Upande wa pili kuna 51% ambako wewe upo. Tunaomba taarifa za 51% jinsi mlivyotengezena faida. Jadili ukiwa objective usilete ushabiki. Hapa hatutajadili mapenzi ya timu tunajadili biashara na uwekezaji. Msichanganye vitu tafadhali
 
51% ndio Simba yenyewe fan base, logo na assets za club ambavyo vipo yeye hio 20B yake kaiweka kwenye account gani? Kila siku kutusimanga kama biashara haimlipi anafanya nini si aondoke? ile michango ya uwanja na ahadi yake zipo wapi ? ni lini ametoa sheet za mapato na matumizi tuone hio hasara
 
Angalia huyu mfuasi mwingine wa zumaridi . Mambo ya Yanga yanawawashia nini ? Fanyeni mambo yenu achaneni na Yanga . Mwaka lazma muokote makopo . Kolo mwitu
Haha...hiyo profile picture yako sasa hadi nimecheka balaa [emoji1787]
 
Hata ukisikiliza kwenye Mkutano wa Simba mwaka huu, Mapato ya Simba ni Chini ya Bilioni 10 kwa Mwaka, ila Matumizi ni 12.7bil

Hizo za juu ndiyo MO hutoa

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Wakati imefika kwa wanachama wapewe club zao kusimamia kwa muda wa 6 months kwa kila kitu , salaries, kuscout na kununua wachezaji siyo kupiga kelele kila siku.
 
Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM Eng. Hersi Said amewashukia baadhi ya wadau wa soka nchini Tanzania walioibua hoja inayogusa udhamini wa kampuni hiyo kwenye klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Hoja hiyo imeibuka kufuatia Kampuni ya GSM kuwa mdhamini ya Young Africans, Namungo FC na Coastal Union, huku ikijaribu kuisafirisha Biashara Utd kwenda Libya (safari ambayo ilishindikana).

Wasiwasi uliopo ni kwamba kama kampuni ya GSM imewekeza kwenye klabu zaidi ya moja itakua na sababu ya kushawishi upangaji wa matokeo hasa kwa timu wanazozidhamini zitakapokutana.

Hersi ameandika kuwa: ”Timu hizi zinajiendesha kwa hasara kwa miaka mingi ndio maana zimekwama. Ukisema hivi mtu anaweza asikuelewe lakini ukitazama mapato ya klabu na matumizi ndio utajua kwanini zinajiendesha kwa hasara”

”Yanga inalipa mishahara yenyewe, ina mifumo yake ya kuajiri watu sisi tuna-support tu. Yanga ni timu kubwa huwezi kufananisha na hawa makolo. Huwezi kumleta mchezaji kama Bangala halafu hajui mshahara analipwa na nani”

”Hii ni klabu kubwa, tunafanya kazi ya kurejesha heshima yake, watu waipende tena. Mechi ya juzi Yanga inafungwa goli mashabiki wanapiga makofi, tunarudisha tunafunga la pili na la tatu na bado kuna dakika kama 900 za kucheza”

”Watu wanaleta siasa chafu na mimi nasema hizi ni takataka. Mbona kampuni kama Emirates inadhamini vilabu vingi tu vinacheza Champions League. Ina maana Arsenal wakicheza na AC Milan utasema mmoja amwachie mwenzake?”

My Take
Sina My Take yeyote
Kwahio hii habari ya mwaka 2021 umeileta hapa kubalance vilio vya mudi? nyie si mnasema ni wakubwa tujifunze kwenu tufundisheni jinsi ya kupata faida
 
Back
Top Bottom