Eng. Hersi 2021: Yanga inajiendesha kwa Hasara

Kuna tofauti kubwa kati ya Club kujiendesha kwa hasara na Club kumtia mtu hasara

Au tuiweke hivi;
1. "Hii Club inajiendesha kwa hasara, hii ni Club kubwa, yunafanya kazi ya kurudisha heshima yake"

2. "Hii Club inania hasara, natoa hela zangu kwa mapenzi tu wala hakuna numachokipata zaidi ya hasara. Gharama ninazotumia kwenye hii club kwenye hii club nimgeweza hata kununua ndege:

Tafakari
 
Uendeshaji wa klabu ni hasara katika taifa hili la TANZANIA na hata nchi nyingi za kiafrica.

Watu hawajiulizi tu Simba inatumia kiasi gani kulipa mishahara ya wachezaji, makocha na waajiriwa wengine kwa mwaka mzima,

Gharama za kuisafirisha timu, benchi la ufundi na viongozi kuzunguka Tanzania katika mechi 15 za msimu ni kiasi gani ? (NOTE: Usafiri wa ndege)

Gharama za kusafirisha timu na viongozi kwenda nje ya nchi kwa ajili ya mechi za kimataifa?

Gharama za hoteli!?

Gharama za posho, makazi ya wachezaji n.k

Gharama za usajili n.k

Ukishapiga hesabu haya njoo uangalie vyanzo vya mapato ya timu na kiasi cha pesa inayokusanywa! Mechi za taifa ukitoa big matches mahudhurio huwa ni hafifu licha ya kuwa viingilio huwekwa hadi 3000 na bado watu hawazidi hata 20000.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…