Eng. Hersi atoa tiketi za bure kwa watu wasioona

Eng. Hersi atoa tiketi za bure kwa watu wasioona

Mambo ya kunadi karanga za maziwa kwa wagonjwa ndani ya hospitali ya meno.
 
Is this supposed to be a Joke ?!!!!; Badala ya kuwapa hizo ticket hata angewapa / angechangia vitabu vya watu wasioona vyenye story za simba / au story nyingine lakini sponsored by Timu yake
 
Siyo wote wanaoingia viwanja vya mpira huwa wanaangalia mechi yenyewe, wapo wenye macho mazima kabisa lakini uwanjani haangalii hata Sekunde moja.
Huu ni ukweli wengine wanaingia uwanjani Ila wanakua na mishe zingine hawafocus na kuangalia mpira km umeenda uwanjani mara kwa mara lazima utakua umewaona
 
Wengi tunatoa maoni kana kwamba ni kazi bure kwa wasioona kwenda uwanjani kuangalia mpira.

Ninachoweza kusema ni kuwa wasioona wanatumia hisia zaidi kwa sababu ya kukosa macho.

Yaani kwa asiyeona anapata hisia zaidi akiwa yupo uwanjani panapachezwa mpira, kuliko wewe ukiwa hapo ukafumba macho huku mpira unachezwa.

Sasa hapa watu wanapinga kwa mtazamo wa mtu aliyefumba macho kushuhudia mpira huku akiwa na uwezo wa kuona.
Sasa yeye hana mbadala, hivyo anakuwa anashuhudia kwa hisia sana kwa sababu ubongo ameshautune kuwa hakuna namna nyingine anaweza kushuhudia.

Wasioona huwa wanakwenda misibani kuaga, kwenye harusi, kwenye starehe mfano show za wasanii nk. Wakati mwingine asiyeona anapiga vyombo vya muziki huku wanaoona wanacheza.

Hersi yupo sahihi, anachangia kutimiza hisia zao.
 
Watanzania likifika swala la Simba na Yanga akili hua zina waruka mbaya zaidi kitu kikifanywa upande wa pili ambao sio wako utakosoa tu hapo chini ni mashabiki wasio na uwezo wa kuona wapo uwanjani ila hapa kwetu itatafutwa sababu mpka ushirikina uhusishwe
C1WavXwWIAAiqiy.jpg
audio-described_commentary_for_blind_matchgoing_fan.jpg
0_Stephen-Garcia-and-Mike-Kearney.jpg
 
Back
Top Bottom