Wengi tunatoa maoni kana kwamba ni kazi bure kwa wasioona kwenda uwanjani kuangalia mpira.
Ninachoweza kusema ni kuwa wasioona wanatumia hisia zaidi kwa sababu ya kukosa macho.
Yaani kwa asiyeona anapata hisia zaidi akiwa yupo uwanjani panapachezwa mpira, kuliko wewe ukiwa hapo ukafumba macho huku mpira unachezwa.
Sasa hapa watu wanapinga kwa mtazamo wa mtu aliyefumba macho kushuhudia mpira huku akiwa na uwezo wa kuona.
Sasa yeye hana mbadala, hivyo anakuwa anashuhudia kwa hisia sana kwa sababu ubongo ameshautune kuwa hakuna namna nyingine anaweza kushuhudia.
Wasioona huwa wanakwenda misibani kuaga, kwenye harusi, kwenye starehe mfano show za wasanii nk. Wakati mwingine asiyeona anapiga vyombo vya muziki huku wanaoona wanacheza.
Hersi yupo sahihi, anachangia kutimiza hisia zao.