Eng. Hersi itafikia hatua mashabiki na wanachama watauvua uvumilivu wao kwako

Eng. Hersi itafikia hatua mashabiki na wanachama watauvua uvumilivu wao kwako

Yule Damaro ambaye alikuwa anacheza kama mchezaji wa ndani, sijui nini kiliwafanya wamrudishe kule Singida wakati alikuwa anaitumikia Yanga kwa mkopo. Hakuwa na ubora mkubwa ila alikuwa anasaidia kulingana na aina ya mechi. Halafu kwanzia aondoke Miloud Yanga haijafanikiwa kurejea katika ule ubora wake
na saiv ukiangalia kiungo cha yanga hasa kwenye namba 6 bado ni kweupe kabisa hasa kipindi hiki Abuya na Muda hawapo, walau angesaidia kiasi yule jamaa mana Aziz Andabwile yupo ila naona hawamuamini kabisa japo kuna kipindi alionesha kitu kwenye ile position kwenye mechi kadhaa mwanzoni mwa msimu ulopita wakati wa kocha Folz, yule Fred Ngoma ambae wao wanasema wamemsajili kama namba 6 lkn ukimuangalia anavyocheza ni namba 8 zaidi kuliko hiyo position ya namba 6

Kwa Kocha Miloud alichofanya hakuleta mambo mengi alitembea na blueprint ile ile ya kocha Gamondi ila yule Ramovic mimi sikuwahi kumuelewa kwakweli tena hasa ile mambo yake ya kumuweka kibwana na Israel Mwenda mmj winga mwingine beki kwenye ule upande wa kulia ndo nilikuwa simuelewi kabisa, timu ilikuwa inashinda sababu tu wachezaji tu wenyewe walikuwa wanafosi ila mpira mbovu kabisa tunacheza na ndo mana kwa ule mpira wake tukatupwa nje CAF mapema tu, tena hasa ile game ya mwisho na MC Alger Pacome akamuweka benchi kaenda kuanza na Musonda kama winga kama Pacome alikuwa na shida Chama si unae na yuko fit na ana experience nzuri tu na mzuri kwenye kutengeneza nafasi na kufunga pia kwanini usianze nae na ile mechi ilikuwa ni kushambulia mwanzo mwisho ilikuwa inatakiwa tuwe na viungo wengi wanaotengeneza nafasi na kufunga pia mana wale MC Alger wote tulikuwa tunajua wanakuja kupaki basi tu.
 
Depu na okello walipata ofa kubwa. Tunaona pesa waliyonunuliwa na mishahara wanayolipwa uko walipoenda ni pesa ndefu kwa level za timu zetu hapa bongo. Aucho alishafikia peak yake akua na maajabu tena zaidi ya alipofika pia alishaanza kuandamwa na majeruhi. Alipewa mkataba wa mwaka mmoja akakataa. Alitaka miaka mitatu.

Injia kama binadamu ana madhaifu yake lakini tusitoe mambo nje ya context kuhalalisha hisia zetu
Depu na Okello yanga wamewatimua wenyewe kama ishu ni ofa mbn Mzize na Pacome au hata Aziz Ki ule msimu anakuwa top scorer alipata ofa na yanga waliweza kumbakisha
 
Miloud Yanga walimtimua wao wenyewe, mfano wewe ndio kocha mkuu kwenye timu A then kabla hata msimu kuisha unaskia tetesi hiyo timu A inatafuta kocha mkuu, wewe kama kocha mkuu wa hiyo timu A kwa wakati huo unapata picha gani apo?? si maana ake wanakuona hutoshi

Na naamini hata kwa Aucho, Depu na Okello sio kweli kama sijui walipata ofa kubwa hamna lolote ni Yanga wenyewe chini ya Injinia wameondoa hizo quality kwa sababu ambazo hazina tija mwishoe wameenda kuokota viazi akina Toure , Selemani, Komaro sijui Zakwani, mfano kuna Timu kwa vipindi tofauti zilikuwa zinawahitaji Aziz Ki, Pacome na Mzize mbona kwa hao yanga waliweza kuwabakisha.

Ni kuna decisions za kiwaki saiv zinaendelea kwenye hii timu, af zigo la lawama anakuja kuaangushiwa kocha kila msimu.
Uko sahihi, Okello aliachwa kuondoka kisa shemeji wa Taifa kutaka kurudi utopoloni, wakaona wamuondoe Okello aje shemeji.
 
Kocha mmetimua kwa ku panic tu kwasababu mlifungwa na Simba.

Sasa kashinda mechi zote kasoro moja kafungwa na nyingine draw. Hizo ni sababu za kumtimua kocha ambaye amewavusha kwa kishindo kwenda CAF group stage na akiwa hana hata miezi minne tokea aanze kazi Wewe unaona hiyo ni akili timamu?

Hapo viongozi ndo hawataki wanyooshewe vidole wao, wanahamisha attention kwingine na siyo kwao.

Kumfukuza huyo kocha ni mambo ya kitopolo kabisa.
Maboga mabichi amefukuzwa kisa tu kufungwa na mnyama, wala hakuna sababu nyingine.
 
Maboga mabichi amefukuzwa kisa tu kufungwa na mnyama, wala hakuna sababu nyingine.
Sababu zipo tokea muda tu sema kusikia kwa kenge mpaka atoke damu. Mechi ya Yanga vs Gaborone na ile vs Geita Yanga iliomba refa amalize mpira. Ni ishara ya anguko, mechi Simba na TRA ikamalizia kabisa anguko la Yanga
 
Mkuu hizo stori za vijiweni, timu gani ya kuweza ku beat na Yanga unayoingolea hapo? Al Ismaily ndio impe Miloud ofa kubwa kuliko Yanga? Sio kila timu iliopo uarabuni basi ndio inapesa, hiyo timu imejichokea ndio maana hawana uwezo wa kufanya usajili wa maana na kuishia kuburuza mkia na kugombea nafasi za kushuka daraja.

Miloud hawezi kwenda kwenye timu inayoshuka daraja akaiacha timu inayoenda kucheza klabu bingwa. Mbona alihojiwa na kusema kuwa alikuwa anasubiria kupewa mkataba mpya baada ya kuisha mkataba wake ila kashangaa uongozi hawamuiti kuzungumzia mkataba mpya, ndipo akatafuta timu.

Kulikuwa na video humu humu JF ya mahojiano, sijui tu ni uzi upi.
Ni sahihi, jamaa alisema alitamani kuendelea ila viongozi wakamuweka pembeni.
 
Sababu zipo tokea muda tu sema kusikia kwa kenge mpaka atoke damu. Mechi ya Yanga vs Gaborone na ile vs Geita Yanga iliomba refa amalize mpira. Ni ishara ya anguko, mechi Simba na TRA ikamalizia kabisa anguko la Yanga
Mechi za Gaborone tulitafuta matokeo kwa shida, Simba sio wa kutuchezesha mpira mwingi kiasi kile na kutufunga. Manqoba aliishiwa mbinu aiseee.
 
na saiv ukiangalia kiungo cha yanga hasa kwenye namba 6 bado ni kweupe kabisa hasa kipindi hiki Abuya na Muda hawapo, walau angesaidia kiasi yule jamaa mana Aziz Andabwile yupo ila naona hawamuamini kabisa japo kuna kipindi alionesha kitu kwenye ile position kwenye mechi kadhaa mwanzoni mwa msimu ulopita wakati wa kocha Folz, yule Fred Ngoma ambae wao wanasema wamemsajili kama namba 6 lkn ukimuangalia anavyocheza ni namba 8 zaidi kuliko hiyo position ya namba 6

Kwa Kocha Miloud alichofanya hakuleta mambo mengi alitembea na blueprint ile ile ya kocha Gamondi ila yule Ramovic mimi sikuwahi kumuelewa kwakweli tena hasa ile mambo yake ya kumuweka kibwana na Israel Mwenda mmj winga mwingine beki kwenye ule upande wa kulia ndo nilikuwa simuelewi kabisa, timu ilikuwa inashinda sababu tu wachezaji tu wenyewe walikuwa wanafosi ila mpira mbovu kabisa tunacheza na ndo mana kwa ule mpira wake tukatupwa nje CAF mapema tu, tena hasa ile game ya mwisho na MC Alger Pacome akamuweka benchi kaenda kuanza na Musonda kama winga kama Pacome alikuwa na shida Chama si unae na yuko fit na ana experience nzuri tu na mzuri kwenye kutengeneza nafasi na kufunga pia kwanini usianze nae na ile mechi ilikuwa ni kushambulia mwanzo mwisho ilikuwa inatakiwa tuwe na viungo wengi wanaotengeneza nafasi na kufunga pia mana wale MC Alger wote tulikuwa tunajua wanakuja kupaki basi tu.
Tukumbuke pia kuwa kocha Miloud ni kwa hisani Singida. Hivyo Hersi akataka sifa aonekane anajicho la kutafuta makocha wazuri. Akampotezea Miloud na kumleta Folz
 
Back
Top Bottom