Eng. Hersi itafikia hatua mashabiki na wanachama watauvua uvumilivu wao kwako

na saiv ukiangalia kiungo cha yanga hasa kwenye namba 6 bado ni kweupe kabisa hasa kipindi hiki Abuya na Muda hawapo, walau angesaidia kiasi yule jamaa mana Aziz Andabwile yupo ila naona hawamuamini kabisa japo kuna kipindi alionesha kitu kwenye ile position kwenye mechi kadhaa mwanzoni mwa msimu ulopita wakati wa kocha Folz, yule Fred Ngoma ambae wao wanasema wamemsajili kama namba 6 lkn ukimuangalia anavyocheza ni namba 8 zaidi kuliko hiyo position ya namba 6

Kwa Kocha Miloud alichofanya hakuleta mambo mengi alitembea na blueprint ile ile ya kocha Gamondi ila yule Ramovic mimi sikuwahi kumuelewa kwakweli tena hasa ile mambo yake ya kumuweka kibwana na Israel Mwenda mmj winga mwingine beki kwenye ule upande wa kulia ndo nilikuwa simuelewi kabisa, timu ilikuwa inashinda sababu tu wachezaji tu wenyewe walikuwa wanafosi ila mpira mbovu kabisa tunacheza na ndo mana kwa ule mpira wake tukatupwa nje CAF mapema tu, tena hasa ile game ya mwisho na MC Alger Pacome akamuweka benchi kaenda kuanza na Musonda kama winga kama Pacome alikuwa na shida Chama si unae na yuko fit na ana experience nzuri tu na mzuri kwenye kutengeneza nafasi na kufunga pia kwanini usianze nae na ile mechi ilikuwa ni kushambulia mwanzo mwisho ilikuwa inatakiwa tuwe na viungo wengi wanaotengeneza nafasi na kufunga pia mana wale MC Alger wote tulikuwa tunajua wanakuja kupaki basi tu.
 
Depu na Okello yanga wamewatimua wenyewe kama ishu ni ofa mbn Mzize na Pacome au hata Aziz Ki ule msimu anakuwa top scorer alipata ofa na yanga waliweza kumbakisha
 
Uko sahihi, Okello aliachwa kuondoka kisa shemeji wa Taifa kutaka kurudi utopoloni, wakaona wamuondoe Okello aje shemeji.
 
Shalulilekashachukua makombe yote makubwa Hana uchu WA mafanikio tena ,unamsanili Yanga unategemea nini wanashindwa kuchukua Amina girumugisha wanasajili garasa πŸ˜‚πŸ˜‚
Yanga, ni team ya wachezaji kula pension,
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Maboga mabichi amefukuzwa kisa tu kufungwa na mnyama, wala hakuna sababu nyingine.
 
Maboga mabichi amefukuzwa kisa tu kufungwa na mnyama, wala hakuna sababu nyingine.
Sababu zipo tokea muda tu sema kusikia kwa kenge mpaka atoke damu. Mechi ya Yanga vs Gaborone na ile vs Geita Yanga iliomba refa amalize mpira. Ni ishara ya anguko, mechi Simba na TRA ikamalizia kabisa anguko la Yanga
 
Ni sahihi, jamaa alisema alitamani kuendelea ila viongozi wakamuweka pembeni.
 
Sababu zipo tokea muda tu sema kusikia kwa kenge mpaka atoke damu. Mechi ya Yanga vs Gaborone na ile vs Geita Yanga iliomba refa amalize mpira. Ni ishara ya anguko, mechi Simba na TRA ikamalizia kabisa anguko la Yanga
Mechi za Gaborone tulitafuta matokeo kwa shida, Simba sio wa kutuchezesha mpira mwingi kiasi kile na kutufunga. Manqoba aliishiwa mbinu aiseee.
 
Tukumbuke pia kuwa kocha Miloud ni kwa hisani Singida. Hivyo Hersi akataka sifa aonekane anajicho la kutafuta makocha wazuri. Akampotezea Miloud na kumleta Folz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…