Titicomb
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 12,823
- 21,210
Pesa ndogo sana hiyo.Acheni kujipa jukumu la kuwa mshauri wa mchezaji kwa maslahi yenu binafsi. Wachezaji wana meneja na wakala, suala la kumzuia mchezaji fulani kisa mnahisi timu inayomtaka ni ndogo halikuhusu wewe kama mshabiki au hata kiongozi wa timu ni kazi ya wale wanaomsimamia mchezaji mwenyewe.
Eti Wydad ni timu ndogo? Unajua exposure ya Club World Cup wewe? Umeona uwekezaji wanaoufanya sasa kwa kuanzia kwa benchi la ufundi? Kaizer Chiefs ingekuwa timu ndogo mngeshangilia kama wehu baada ya kuwafunga katika mechi ya kirafiki?
Huu mnaofanya ndiyo tunaita ushabiki maandazi, kutetea uovu kisa timu yako imeweka msimamo fulani.
Nani kaongelea pesa ndogo? Kwani dola 100K ni pesa ndogo? Yaani unataka kusema Mzize ana thamani kubwa kuliko kikosi kizima cha Yanga? Mnachekesha sana nyie watu.
Uzeni wachezaji wenu sisi Young African hatuuzi hiyo bei.