Eng. Hersi Said acha kuwa na kiburi

Eng. Hersi Said acha kuwa na kiburi

Bigirimana hakuna wa kumfikia hapa Bongo, tatizo mmezoea kutumia nguvu nyingi bila akili.
Mkuu Kwa bigirimana pale tumepigwa.. ukisema wachezaji wanaotumia akili hapo huwezi kumtaja bigirimana ukawaacha kina Chama, Saido.. Yaani yule ni mchezaji wa daraja la chini sana kwa Sasa ambae hana msaada Kwa timu yetu.
 
Mimi ni mwanachama wa Yanga mwenye kadi kabisa ya uwanachama.

Watu wengi wanajiunga na kujiandikisha kama wanachama wa Yanga kwa sababu wanaona timu inavyopata matokeo.

Timu kwa Sasa imekuwa popular kwa sababu ya kuongeza fan base kwa sababu ya matokeo..

Sasa eng anaona kama timu yeye ndiye anaisaidia Sana lakini aelewi kwamba timu kufanya vizuri ni mchanganyiko wa mambo mengi yaani Benchi bora la ufundi, dua za wadau, Uwekezaji kwenye kununua wachezaji bora wa aina zote kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi.

Kwanza makosa makubwa yaanza kufanywa pale yanga ya kufukuza fukuza wachezaji na kujifanya yanga ni kubwa kuliko wachezaji!!

Hii sio kweli wote tunategemeana yanga ni timu ya umma sio ya GSM kwamba ataamua kila kitu tu yeye Bila kuulizwa lazima tuhoji kwa sababu Harsi mimi ni moja ya watu ambao nilikuchagua acha kuwa na kiburi .

Acha kuingizwa king na majasusi na kujifanya unajua kila kitu .

Mpe fei toto mkataba mpe hiyo milion 16 kwani pesa kitu gani bwana si wanacha si tunatoa ?

Mpe dickson job mkataba mrefu hata miaka 5 yule yupo yupo Sana Sana mpe hiyo milion 10 anayotaka.

Yanga kwa Sasa ina wanachama 50000×29000 unapata 1,450,000,000 hii pesa inatosha kulipa mishahara ya mwaka mzima ya wachezaji!!.

Hivi unapata kiasi gani kama shukrani kutoka kwa wachezaji wabovu kama Bigrimana na Kisinda takataka zile?

Eng acha kiburi kubali kwamba kwa Kisinda na Bigrimana tulipigwa achana nao kabisa tumefanya makosa kwa saido alitakiwa kupewa mkataba mpya mapema Sana sasahivi tunakuwa na kiburi..

Tutapoteza wachezaji vijana kama feisal na Dickson job tena wazawa kwa sababu ya milion 26 upuuzi kama timu haina pesa semini tuchangie..

Yanga ni brand kubwa kwa Sasa na timu yeyote kama inapata matokeo na kulinda maslahi ya wachezaji wetu hakuna mtu ataiangusha hii club.

Mnahangaika na wachezaji ambao hawajaprove na kuchezea shilling kwa wachezaji ambao tayari walishaprove.

Eng acha kiburi kuwa makini Sana Linda wachezaji wetu ambao waliipambania timu hata kabla ya timu kuwa na chochote!!!.

Happy new year!!
Pita kule mwenye kiburi ni Eng au Fei toto kafanya utoto?
 
Usidanganyike ni kitu kinaitwa "fan base" kwa hizi timu kubwa, hao jamaa wanachojua ni kupiga kelele tu za ushabiki, lakini ukitaka kujua walivyo wasumbufu waambie tu walipie kadi zao za uanachama, hapo ndipo utaiona rangi yao halisi, ni wagumu kutoa wanaopenda sana kulalamika mambo ya timu yakienda kombo, kuna uswahili mwingi sana.
Umesema jambo zuri sana mkuu. Umeongea ukweli kabisa. Na ndo ninachokiona hata humu JF wengi ni wapiga kelele wasio na msaada kwa Simba na Yanga.
 
Soma namba 5 uone michango ya wanachama Kwa mwaka 2020.

Wanachama walichangia milion 6 kwenye Ada za uanachama.

Hiyo ni taarifa ya mapato na matumizi ya Yanga kwenye mkutano mkuu WA timu mwaka 2020.

Sasa wewe endelea kujidanganya na hizo bilion za wanachama
View attachment 2464737
Unaletq mambo ya 2019 wakati tupo 2023 tafuta takwimu za wanachama wa Yanga December 2022 baada ya transformation
 
Unaletq mambo ya 2019 wakati tupo 2023 tafuta takwimu za wanachama wa Yanga December 2022 baada ya transformation
We mpuuzi hujui taarifa za fedha za mwaka 2022 za Yanga zinatoka mwaka 2023.

Nyie ndio Aina ya mashabiki kichwani hamna akili.

Nimekuwekea ripoti ya 2020 ambayo ilitoka 2021.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom