Feisal hana bifu na Yanga bali ana bifu binafsi na kiongozi wa Yanga (Eng Hers).
Je Umechukua mchumba wake (mpenzi) wake?
Nini umemfanya kijana huyu mpaka kuamua kabisa bora aachane na mpira lakini siyo kufanya kazi na wewe?
NALIA NGWENA nimeweka pembeni ushabiki nimejiuliza sana haya maswali kwa jicho la tatu bila shaka kuna kitu kikubwa nyuma ya pazia na bwana mdogo Feisal Salumu anafukia (anaficha) hataki kuweka wazi.
NALIA NGWENA nitafurahi sana kama Eng HersI utakuja hadharani kuzungumza nini ulichomfanya Feisal lakini usipojibu mashabiki tutabaki na mashaka makubwa na kuwa wachezaji wetu huko avic town Kuna Mambo ya ajabu wanafanyiwa.
Nawasilisha hoja.