Eng Hersi Said Simamia Misingi ya Kanuni na Sheria za Mpira. Mshauri Rais Samia asivuke Mipaka

Mtu anatoa ombi halafu anataka na mrejesho wa mtakapofikia kama una akili timamu lazima ujiongeze.

Huyo mpemba akisaini Simba hii dinner watailaani sana waliokuwa wamedhamiria kumkomoa.

Halafu tuhuma zake alizotoa juzi hazitojibiwa tena hivyo kuaminika ni za kweli.
 
Wewe ndio yule wanaemuita HAJI ?
 
Wamuache aende kwan wachezaji si wapo Duniani kote shida ni nini ? Au ndio roho za kichawi kuwangiana na kuwekeana kauzibe ?
 
Hili liwe fundisho kwa mawakala wa wachezaji.
Lazima kuwa na kipengele katika mkataba kinachoonesha.

1. Timu ikitaka kuvunja mkataba wa mchezaji muda wowote ifate kanuni gani.
Kuna wakati mchezaji anabadilikia kutabia au anaisaliti timu na anatakiwa kuachwa lazima kuwa na kipengele cha namna ya kumwacha.

2. Mchezaji akitaka kuvunja mkataba wake na timu kama Dejeni wa Simba.
Kuna wakati mchezaji anataka kuiacha timu yake na kuondoka kama kafanyiwa hujuma flani au kudharauliwa au kuvunjiwa heshima kama Fei toto.
Lazima kuwe na kipengele cha namna ya kuachana na timu yake.

Kucheza mpira ni ajira kama ajira nyingine.
Mchezaji kama amepoteza imani na timu yake na anataka kuondoka kumkatalia ni hakuna tija kwake na wala kwa timu.
Sheria lazima ziongee kwa mambo kama haya.
 
Wasomali na mambo ya kanuni sijui sheria wapi na wapi?
 
Ombi la Rais wa Nchi akimaliza,kulitamka linageuka kuwa amri ambayo lazima itekelezwe. Na wako watakaofuatilia kuhakikisha inatekelezwa ima unapenda au la.

Mchezaji huyu hawezi kucheza yanga tena labda Rais wa yanga asiwepo.

Hivyo yanga itangaze kumuuza. Kama hatokei wa kumnunua basi imdai fidia kama kipengele hiko kiko kwenye mkataba. Ama imsamehe bure aende zake akasajiliwe na timu nyingine. Liwe jua ama mvua amri ya mkuu wa nchi lazima itekelezwe na ioonekane imetekelezwa. Hiyo ndio gharama yanga wamelipia kwa kwenda ikulu kula dinner bila ya Feisali kuwa sehemu ya wahudhuriaji. Na kaalikwa nyumbani kwenda kusema yuko huru mgogoro ukisha tatuliwa.
 
Huu ni wakati wa Eng Hersi Said kuonyesha kwanini alichaguliwa na WANANCHi kusimamia maslahi ya Klabu Kubwa.
Hakuna mkate mgumu mbele ya chai!! Hpo injinia kashapigiwa cm na GSM kuwa hebu muacheni FEI aendezake.. gharama ya kupambna na serikali ni kubwa sana.. Dogo kashaachiwa tayrii na mrejessho unasubiriwa
 
Hii ngoma inamalizikia pale TFF, I mean, Karia ndo atakuwa mbuzi wa kafara.

Ile kesi ambayo Yanga wamepeleka TFF itatoka ruling kuwa Fei toto ana haki ya kuvunja mkataba.

Fa masihara nini! Mpewe hadi eneo la kujenga uwanja af muanze kubinya binya wapemba wakat mama yupo! Bangladesh
 
Biriani, Pilau, Sharubati Zimeishia Kooni Wameshindwa Kumeza Kwa Uchungu Mwingi Hasa Rais Alipogonga Kisu Cha Uchungu Kuhusu Feitoto
Aachwe Aende Atakapo Bila Sharti, FIFA Wanawazoom Wanasiasa Tanzania
 
Ombi la Rais popote duniani ni amri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…