Eng Hersi Said Simamia Misingi ya Kanuni na Sheria za Mpira. Mshauri Rais Samia asivuke Mipaka

Habari wanajamvi.

Leo amesikika Rais wa Tanzania Akimdadavulia Rais wa Yanga SC Bw Eng Hersi Said kwa lengo la
kumuhimiza ahakikishe Mchezaji Feisal Salum anapata haki yake.

Ninacho fahamu kuwa Mama Samia hana ufahamu sahihi wa kinacho endelea baina ya mgogoro uliopo kati ya Yanga SC na Mchezaji husika. Hisia zake kama Mzanzibar ndizo zimempelekea kusukumwa kutoa mapendekezo yake pasi na kuhitaji kulifahamu zaidi swala hilo.

Ndugu Hersi Said, unapaswa kucheza karata zako makini mno kwenye hilo. Kumbuka Mama Samia ametumia gharama kiduchu sana kwenye kampeni ya zawadi za kila goli, Dinner la Ikulu pampja na usafiri wa ndege. Kumbuka hajafanya haya si kwa mapenzi ya dhati na masuala ya michezo, bali alilenga zaidi kuilaghai taasisi ya michezo ili iache kusimamia misingi ya kisheria na kikanuni ya michezo.

Kwa kawaida, ni muhimu kwa Rais wa nchi kuzingatia majukumu yake kikatiba na kutofautisha majukumu ya mamlaka nyingine za kiserikali na taasisi mbalimbali. Mgogoro kati ya klabu na mchezaji ni suala la kisheria ambalo linapaswa kusuluhishwa na mamlaka husika za sheria na kanuni za michezo.

Rais Samia Anahitaji Elimu zaidi.

Kwa hiyo Rais wa nchi kuingilia kati ktk mgogoro kama huo unaweza kusababisha mchanganyiko wa majukumu na kuingilia uhuru wa mamlaka nyingine. Ni muhimu kwamba kila mamlaka ifanye kazi yake. Kitendo cha Rais kuwapa Incentives mbalimbali basi isiwe sababu ya kuhalalisha kuingiliana ki mamlaka katika mihimili inayo jitegemea kiutendaji.

Rais Samia anahitaji mrejesho, Basi ni wasaa sahihi kuhakikisha anaandikiwa mrejesho wa kumuelimisha kuwa masuala ya migogoro ya kisoka/kimpira yana namna yake ya kutatuliwa. Muelewesheni kuwa zipo sababu za msingi kwanini hili suala linakawia kufikiwa tamati.

Ni vyema akafahamu kuwa uvunjwaji wa taratibu na mchezaji yeyote wa klabu ni lazima kuadhibiwe pasi na kujali kama huyu ni mchezaji wa kizanzibar, wa bara au wa kimataifa. Na hukumu kwa mchezaji wa namna hiyo hautotokwa kwa upendelea wa kibusara eti kwa kisingizio kuwa mchezaji ni mzawa au la.

Mshaurini Rais kuwa licha ya kuyafurahia mafanikio haya madogo ya klabu, kuna watu nyuma ya pazia ambao wanawekeza pesa zao na wasingependa kuona wanapata hasara ktk biashara ya mauzo ya wachezaji. Tukiruhusu kuingilia maamuzi ya taasisi huru ambazo zina sheria zake za usuluhishi basi tunajiweka katika nafasi ya kuwafukuza wawekezaji aina ya wakina GSM na Mo Dewji katika mpira wa Tanzania.

Kuna madhara makubwa sana endapo klabu kama klabu itashindwa kusimamia misingi ya taratibu zake na kusuluhisha migogoro na kesi za kimpira kwa kutumia tu mapendekezo ya wana siasa. Je Mama Samia anatoa ushauri kama nani? Je ni kama mtu mwenye ufahamu wa kanuni na taratibu za uendeshaji wa mpira? au Kama
rais katoa ombi hajaelekeza wala kulazimisha,yanga watamwita fei na waongee ili wamuuze au alipe gharama za kuvunja mkataba
 
Rais Samia amesema "ANAOMBA" wakalimalize swala la Feisal, hapendezwi na ugomvi. Hajasema kama kuwalazimisha au kama amri. Ni "OMBI" ametoa ambalo linaweza likakubaliwa au kukataliwa na hao viongozi wa yanga!!!

Kosa lake ni nini hapo? Mipaka gani achunge?
Ilo sio ombi ni agizo mkuu kauli ya Raisi wa nchi ni agizo

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Ombi la Rais wa Nchi akimaliza,kulitamka linageuka kuwa amri ambayo lazima itekelezwe. Na wako watakafuatilia kuhakikisha inatekelezwa ima unapenda au la.

Mchezaji huyu hawezi kucheza yanga tena labda Rais wa yanga asiwepo.

Hivyo yanga itangaze kumuuza. Kama hatokei wa kumnunua basi imdai fidia kama kipengele hiko kiko kwenye mkataba. Ama imsamehe bure aende akasajiliwe na timu nyingine. Liwe jua ama mvua amri ya mkuu wa nchi lazima iyekelezwe na ioonekane imetekelezwa. Hiyo ndio gharama yanga wamelipia kwa kwenda ikulu kula dinner bila ya Feisali kuwa sehemu ya wahudhuriaji. Na kaalikwa nyumbani kwenda kusema yuko huru mgogoro ukisha tatuliwa.
Hapo ni kumwuliza Fei anataka nini kufanyike na mwenyewe ndio aamue cha kufanya.
Unamlazimisha kulipa faini akigoma utaendelea kumshikilia ?

Ajira za wachezaji mpira ni lazima ziwe sasa na vipengele vitakavyo mruhusu mchezaji kuondoka muda wowote na pia kuruhusu vilabu kumwacha mchezaji muda wowote pale utakapo onekana inafaa.

Ajira za kulazimishana na kung'ang'aniana zimepitwa na wakati.

Unasaini mkataba wa kazi wa miaka mwili.
Ukitaka kuondoka fanya hili na hili.
Tukitaka kukuondoa tutafanya hili na hili.
Full stop.
 
Bwana mdogo ulikua hujui kwamba Rais wa Nchi hii ni Alpha na Omega?

Usijichoshe kubonyeza Keyboard hapa ukidhani kuna chochote kitabadilika zaidi ya agizo la Rais ni amri.

Bear in mind hata boss wenu GSM kaahidiwa kutobinywa binywa katika biashara zake. Sijui wewe una uwezo wa kuwa mwekezaji ili GSM akuachie timu?

Eng. Hersi na cabinet yake usiku huu wameshajadiri namna ya kumrelease dogo, sasa tunatarajia wewe na jamaa zako muandamane kumpinga Hersi.

Goodnight.
Week hii hii feitoto anakuwa mchezaji Huru tayari kuungana na Mnyama mkali
 
"Sweet command" ni pale mkubwa anaposema NAOMBA.
GSM ni mfanyabiashara anaelewa madhara ya siasa.... Alietoka kauli ni mwanasiasa na mkuu wa nchi... Kukaza shingo Kwa GSM ni kujitia kitanzi kibiashara
Nakumbuka ile kauli ya "GHALIB WEWE FANYA BIASHARA MIMI SITAKUBANA" [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Rais Samia amesema "ANAOMBA" wakalimalize swala la Feisal, hapendezwi na ugomvi. Hajasema kama kuwalazimisha au kama amri. Ni "OMBI" ametoa ambalo linaweza likakubaliwa au kukataliwa na hao viongozi wa yanga!!!

Kosa lake ni nini hapo? Mipaka gani achunge?
Uliwahi kuona mtu aliemkatalia rais kitu maisha yake kwenye jamii yanakuaje?
 
Halafu wanakimbilia kuandika uzi mrefu kama gazeti, tena kwa kujitutumua kweli!!! Rais Samia katoa "OMBI", ombi ambalo linaweza likapokelewa au likakataliwa na viongozi wa yangu! Hayo ni maamuzi yao sasa!
Hakunaga ombi la rais linalokataliwa...kama umewahi ona mtu aliekataa ombi la rais tupe jina..na baada ya kukataa ameishije...
 
Mualiko wa ikulu umekua mchunguu, pilau limegeuka boko boko.

Sahivi ndo mnajua serikali haitakiwi kujihusisha na masuala ya soka? Alipokua anatoa ndege ya serikali buree? Na gharama zote zile? Mbna mlikua hamu muambii hilo??

Tulieni dawa iwaingie vizuriii, na ameshasema hivyoo, kinachotakiwa ni utekelezaji tyuuh.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] patamu hapoooo.
Wanataka kumponza Eng.wao yaani aanze kubishana na mamlaka ! Hilo swala la Fei hata mwezi hautaisha tutasikia limefika tamati
 
Habari wanajamvi.

Leo amesikika Rais wa Tanzania Akimdadavulia Rais wa Yanga SC Bw Eng Hersi Said kwa lengo la
kumuhimiza ahakikishe Mchezaji Feisal Salum anapata haki yake.

Ninacho fahamu kuwa Mama Samia hana ufahamu sahihi wa kinacho endelea baina ya mgogoro uliopo kati ya Yanga SC na Mchezaji husika. Hisia zake kama Mzanzibar ndizo zimempelekea kusukumwa kutoa mapendekezo yake pasi na kuhitaji kulifahamu zaidi swala hilo.

Ndugu Hersi Said, unapaswa kucheza karata zako makini mno kwenye hilo. Kumbuka Mama Samia ametumia gharama kiduchu sana kwenye kampeni ya zawadi za kila goli, Dinner la Ikulu pampja na usafiri wa ndege. Kumbuka hajafanya haya si kwa mapenzi ya dhati na masuala ya michezo, bali alilenga zaidi kuilaghai taasisi ya michezo ili iache kusimamia misingi ya kisheria na kikanuni ya michezo.

Kwa kawaida, ni muhimu kwa Rais wa nchi kuzingatia majukumu yake kikatiba na kutofautisha majukumu ya mamlaka nyingine za kiserikali na taasisi mbalimbali. Mgogoro kati ya klabu na mchezaji ni suala la kisheria ambalo linapaswa kusuluhishwa na mamlaka husika za sheria na kanuni za michezo.

Rais Samia Anahitaji Elimu zaidi.

Kwa hiyo Rais wa nchi kuingilia kati ktk mgogoro kama huo unaweza kusababisha mchanganyiko wa majukumu na kuingilia uhuru wa mamlaka nyingine. Ni muhimu kwamba kila mamlaka ifanye kazi yake. Kitendo cha Rais kuwapa Incentives mbalimbali basi isiwe sababu ya kuhalalisha kuingiliana ki mamlaka katika mihimili inayo jitegemea kiutendaji.

Rais Samia anahitaji mrejesho, Basi ni wasaa sahihi kuhakikisha anaandikiwa mrejesho wa kumuelimisha kuwa masuala ya migogoro ya kisoka/kimpira yana namna yake ya kutatuliwa. Muelewesheni kuwa zipo sababu za msingi kwanini hili suala linakawia kufikiwa tamati.

Ni vyema akafahamu kuwa uvunjwaji wa taratibu na mchezaji yeyote wa klabu ni lazima kuadhibiwe pasi na kujali kama huyu ni mchezaji wa kizanzibar, wa bara au wa kimataifa. Na hukumu kwa mchezaji wa namna hiyo hautotokwa kwa upendelea wa kibusara eti kwa kisingizio kuwa mchezaji ni mzawa au la.

Mshaurini Rais kuwa licha ya kuyafurahia mafanikio haya madogo ya klabu, kuna watu nyuma ya pazia ambao wanawekeza pesa zao na wasingependa kuona wanapata hasara ktk biashara ya mauzo ya wachezaji. Tukiruhusu kuingilia maamuzi ya taasisi huru ambazo zina sheria zake za usuluhishi basi tunajiweka katika nafasi ya kuwafukuza wawekezaji aina ya wakina GSM na Mo Dewji katika mpira wa Tanzania.

Kuna madhara makubwa sana endapo klabu kama klabu itashindwa kusimamia misingi ya taratibu zake na kusuluhisha migogoro na kesi za kimpira kwa kutumia tu mapendekezo ya wana siasa. Je Mama Samia anatoa ushauri kama nani? Je ni kama mtu mwenye ufahamu wa kanuni na taratibu za uendeshaji wa mpira? au Kama

Amshauri nani🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kuingilia mambo ya kisoko Ni ujinga endapo sheria zitakanyagwa mm nitaiandikia caf barua kulalamika serekali ya Tanzania kuingilia mambo ya mpira
Wakati Serikali ya Tanzania inaingilia mambo ya mpira kwa kununua magoli haukuandika barua CAF,wakati Serikali inaingilia mambo ya mpira kwa kutoa ndege kwenda Algeria haukuandika barua CAF,wakati Serikali inatoa dinner Ikulu haukuandika barua CAF,Leo hii uje uandike barua CAF kwa ugonvi kati ya Fei toto dhidi ya Eng. Hersi ? Kuwa serious
Pilau ya Ikulu imegeuka shubiri
 
Bwana mdogo ulikua hujui kwamba Rais wa Nchi hii ni Alpha na Omega?

Usijichoshe kubonyeza Keyboard hapa ukidhani kuna chochote kitabadilika zaidi ya agizo la Rais ni amri.

Bear in mind hata boss wenu GSM kaahidiwa kutobinywa binywa katika biashara zake. Sijui wewe una uwezo wa kuwa mwekezaji ili GSM akuachie timu?

Eng. Hersi na cabinet yake usiku huu wameshajadiri namna ya kumrelease dogo, sasa tunatarajia wewe na jamaa zako muandamane kumpinga Hersi.

Goodnight.
Na kumrelease ni lazima maana kijana ataihujumu timu..ref: Sir A Fergason na M. United, alikua akikuona tuu hata umeanza kususa mazoez anakupga bench akiona una akili mbili anakuuza
 
Kuingilia mambo ya kisoko Ni ujinga endapo sheria zitakanyagwa mm nitaiandikia caf barua kulalamika serekali ya Tanzania kuingilia mambo ya mpira
Kwahiyo wewe unataka Fei toto achezee Yanga hata kama hataki? Akiwafungisha kwenye mechi mtamlaumu?
 
Habari wanajamvi.

Leo amesikika Rais wa Tanzania Akimdadavulia Rais wa Yanga SC Bw Eng Hersi Said kwa lengo la
kumuhimiza ahakikishe Mchezaji Feisal Salum anapata haki yake.

Ninacho fahamu kuwa Mama Samia hana ufahamu sahihi wa kinacho endelea baina ya mgogoro uliopo kati ya Yanga SC na Mchezaji husika. Hisia zake kama Mzanzibar ndizo zimempelekea kusukumwa kutoa mapendekezo yake pasi na kuhitaji kulifahamu zaidi swala hilo.

Ndugu Hersi Said, unapaswa kucheza karata zako makini mno kwenye hilo. Kumbuka Mama Samia ametumia gharama kiduchu sana kwenye kampeni ya zawadi za kila goli, Dinner la Ikulu pampja na usafiri wa ndege. Kumbuka hajafanya haya si kwa mapenzi ya dhati na masuala ya michezo, bali alilenga zaidi kuilaghai taasisi ya michezo ili iache kusimamia misingi ya kisheria na kikanuni ya michezo.

Kwa kawaida, ni muhimu kwa Rais wa nchi kuzingatia majukumu yake kikatiba na kutofautisha majukumu ya mamlaka nyingine za kiserikali na taasisi mbalimbali. Mgogoro kati ya klabu na mchezaji ni suala la kisheria ambalo linapaswa kusuluhishwa na mamlaka husika za sheria na kanuni za michezo.

Rais Samia Anahitaji Elimu zaidi.

Kwa hiyo Rais wa nchi kuingilia kati ktk mgogoro kama huo unaweza kusababisha mchanganyiko wa majukumu na kuingilia uhuru wa mamlaka nyingine. Ni muhimu kwamba kila mamlaka ifanye kazi yake. Kitendo cha Rais kuwapa Incentives mbalimbali basi isiwe sababu ya kuhalalisha kuingiliana ki mamlaka katika mihimili inayo jitegemea kiutendaji.

Rais Samia anahitaji mrejesho, Basi ni wasaa sahihi kuhakikisha anaandikiwa mrejesho wa kumuelimisha kuwa masuala ya migogoro ya kisoka/kimpira yana namna yake ya kutatuliwa. Muelewesheni kuwa zipo sababu za msingi kwanini hili suala linakawia kufikiwa tamati.

Ni vyema akafahamu kuwa uvunjwaji wa taratibu na mchezaji yeyote wa klabu ni lazima kuadhibiwe pasi na kujali kama huyu ni mchezaji wa kizanzibar, wa bara au wa kimataifa. Na hukumu kwa mchezaji wa namna hiyo hautotokwa kwa upendelea wa kibusara eti kwa kisingizio kuwa mchezaji ni mzawa au la.

Mshaurini Rais kuwa licha ya kuyafurahia mafanikio haya madogo ya klabu, kuna watu nyuma ya pazia ambao wanawekeza pesa zao na wasingependa kuona wanapata hasara ktk biashara ya mauzo ya wachezaji. Tukiruhusu kuingilia maamuzi ya taasisi huru ambazo zina sheria zake za usuluhishi basi tunajiweka katika nafasi ya kuwafukuza wawekezaji aina ya wakina GSM na Mo Dewji katika mpira wa Tanzania.

Kuna madhara makubwa sana endapo klabu kama klabu itashindwa kusimamia misingi ya taratibu zake na kusuluhisha migogoro na kesi za kimpira kwa kutumia tu mapendekezo ya wana siasa. Je Mama Samia anatoa ushauri kama nani? Je ni kama mtu mwenye ufahamu wa kanuni na taratibu za uendeshaji wa mpira? au Kama
(Kwa kawaida, ni muhimu kwa Rais wa nchi kuzingatia majukumu yake kikatiba na kutofautisha majukumu ya mamlaka nyingine za kiserikali na taasisi mbalimbali. Mgogoro kati ya klabu na mchezaji ni suala la kisheria ambalo linapaswa kusuluhishwa na mamlaka husika za sheria na kanuni za michezo.)

[emoji867]Raisi katoa ombi hakulazimisha
kuomba kuna mwili kukubaliwa au kutakatiwa
hajalazimisha kuvuja sheria
 
Wakati Serikali ya Tanzania inaingilia mambo ya mpira kwa kununua magoli haukuandika barua CAF,wakati Serikali inaingilia mambo ya mpira kwa kutoa ndege kwenda Algeria haukuandika barua CAF,wakati Serikali inatoa dinner Ikulu haukuandika barua CAF,Leo hii uje uandike barua CAF kwa ugonvi kati ya Fei toto dhidi ya Eng. Hersi ? Kuwa serious
Pilau ya Ikulu imegeuka shubiri
🫱🏼‍🫲🏽🫱🏼‍🫲🏽🫱🏼‍🫲🏽🫱🏼‍🫲🏽🫱🏼‍🫲🏽 kuna mijitu mijinga sana muulize gharama ya ndege kwenda Algeria na kurudivna kwenda Mbeya apige hesabu ya nauli ya watu 250×2 Tz -Algeria
 
Back
Top Bottom