Eng. Hersi, Senzo na Kocha Nabi tunaomba mtuachie klabu yetu!

Eng. Hersi, Senzo na Kocha Nabi tunaomba mtuachie klabu yetu!

Kama shabiki hajui mtendaji mkuu wa klabu kwa sasa ni nani, basi manara alikuwa sahihi kusema pale wenye akili ni wawil tu.
Mbona sijakuelewa, mimi ni yanga mwwnzako mkuu
 
Kipindi hao uliowataja hawapo team ilikuwa na mafanikio gani kimataifa??
 
Ina maana simba iko vizuri kuzidi Yanga!!? Mbona wao wanafanya vizuri kila kukicha!!??
Mbona huwa tunawafunga sana!!??

Simba kwa mkapA hatoki mtu,lakini hao wengine hawalijui hilo
 
Mleta mada wewe ni kolo tafadhali sana usiingilie timu yetu unashindwa nini kumpa mbinu Mgunda na Barbara ili mshinde huko Angola. Kudhihilisha wewe ni kolo na hujui kinachoendelea timu ya wananchi unadhani Senzo bado anafanya kazi Yanga sc.
 
Yanga hawezi kufungwa na Al hilal, Yanga anaingia Makundi kibabe.
 
Huyu naye atakuwa shabiki wa Simba aliyevaa jezi ya Yanga
 
Hakuna siku nimeaibika kama leo mashabiki tunapewa hamasa za kipumbavu tunaenda uwanjani tunarudi na aibu.

Leo nimetamba mtaani nikaja hapa jf nimetamba sana kwenye nyuzi mbalimbali kule Twitter ndo usiseme .
Lakini timu imecheza ovyo imenifanya napita mtaani kwa kujificha kama panya bana.

Kiukweli huyu kocha aache kukariri kikosi ni lazima sasa bangala acheze namba 6 na mmoja kati ya Feisal au Aziz ki aanzie bench.
 
Habarini Wanajangwani wenzangu.

Tunajenga kikosi cha aina gani!?
Kwanini kimataifa kila siku iwe kilio kwetu!?

Hapana. Tunahitaji mabadiliko ndani ya klabu yetu, kuanzia uongozi, wachezaji mpaka benchi la ufundi. Tunahitaji kikosi kitakachotoa upinzani kwa timu za kimataifa na si kutamba Ligi Kuu peke yake.

Kuna muda najisikia wivu ninavyoona wenzetu Simba wanavyotinga mpaka hatua za robo fainali michuano ya Africa, lakini nabaki sina namna kwa sababu Yanga niliirithi mwenyewe kwa baba angu.

Ila ni mpaka lini tutaitwa majina ya kukera na wapinzani huko mitaani kama wamatopeni, utopolo, chura fc, wazee miamala n.k? Yaani kila siku yanga ndiyo iwe timu ya kubinuliwa na wapinzani kimataifa. Hapana, imetosha sasa!

Naanza kuamini viongozi mnafanya tabia chafu za kununua mechi za Ligi Kuu, maana haiwezekani michuano ya nje ndiyo tushindwe ila ya ndani tumudu.

Kwa pamoja tushirikiane kuutoa huu uongozi madarakani, ikiwezekana Wanajangwani tusiende uwanjani, maana ndiyo kunapowapa viburi.

Tunaomba mtuachie timu yetu,
Daima mbele nyuma mwiko
Sijasoma chochote! This is what you deserve. 🚮

Maana hakuna shabiki wa Yanga anaweza kuja kuandika uvundo kama huu wa kwako. Na ukome kujifanya mwananchi. Baki huko huko na tabia zako za kimbumbumbu.


Na kudhihirisha wewe ni bongotole! Eti umemtaja mpaka SENZO, akuachie timu yako!!
 
Sasa ukitakua kujua kuwa kila shabik wa utopolo ni kocha ndo kipnd hiki sas...mara nabi hajui kupanga kikosi....bangala anatakiwa acheze namba 6..yaan ni kelele tu huko mtandaon...kiuhalisia yanga kikosi chao c kizuri kimataifa kama wanavyoaminishwa mashabik..imefika sehem mashabik wa yanga wanaona kwao kutoa sare si haki achilia mbali kufungwa....
 
Sasa ukitakua kujua kuwa kila shabik wa utopolo ni kocha ndo kipnd hiki sas...mara nabi hajui kupanga kikosi....bangala anatakiwa acheze namba 6..yaan ni kelele tu huko mtandaon...kiuhalisia yanga kikosi chao c kizuri kimataifa kama wanavyoaminishwa mashabik..imefika sehem mashabik wa yanga wanaona kwao kutoa sare si haki achilia mbali kufungwa....
Sisi mashabiki wa Yanga tuna imani na timu yetu! Ishinde, itoe sare! Ifuzu! Ishindwe kufuzu! Bado Tutaiunga mkono mwanzo mwisho! Na wala hatushwi na kelele kutoka kwa mashabiki wa timu nyingine, na wasio jitambua.
 
Back
Top Bottom