Manara pale bado yupo sana sidhani hizi fujo na maneno ya wanasimba yatamuondoa
Just kwa kudeclare interest, mimi ni mnyama. Lakini naomba nisaidie kuhusu hili la wanaomuunga mkono na wanaompinga Manara kwa mujibu wa observation yangu:
WANA YANGA
1. Wapo wana Yanga ambao wanaounga mkono uwepo wa Manara pale Yanga kwa kuwa wanaamini anasaidia kuwakera Simba
2. Wapo wana Yanga ambao wanaounga mkono uwepo wa Manara pale Yanga kwa kuwa viongozi (na mdhamini) wa Yanga ametaka awepo pale
3. Wapo wana Yanga ambao wanapinga uwepo wa Manara pale Yanga kwa kuwa alishawahi kuwanyanyasa kwa maneno alipokuwa Simba
4. Wapo wana Yanga ambao wanapinga uwepo wa Manara pale Yanga kwa kuwa anaondoa utulivu kwa idara ya habari na baadhi ya watumishi wa hiyo idara wanaoaminiwa
WANA SIMBA
1. Wapo wana Simba ambao wanapiga vita uwepo wa Manara pale Yanga kwa kuwa wanaamini anatoa maneno ya kuwakera (Simba)
2. Wapo wana Simba ambao wanaounga mkono uwepo wa Manara pale Yanga kwa kuwa wanaamini anasaidia kuondoa utulivu pale Yanga
WACHAMBUZI NA WANA HABARI ZA MICHEZO
Pia lipo kundi dogo la Wana Habari na Wachambuzi wa michezo (bila kujali ushabiki wao kwa Simba na Yanga) linaloangukia katika either kumpiga vita au kumuunga mkono Manara. Hawa wana sababu kubwa mbili, kulinda heshima zao na kulinda maslahi yao
Kwa hiyo si sahihi sana kutoa hukumu moja kwa moja kuwa ni wana Simba ndio wanaotoa maneno ya kumchallenge Injinia na JiiEsiEm kwa kitendo cha kumlea Manara pale Yanga