Poker
JF-Expert Member
- Oct 7, 2016
- 5,445
- 14,828
Raisi wetu wa klabu pendwa ya kihistoria hapa nchini na Africa mashariki. Yanga ni klabu kubwa yenye historia nzuri na Pana, hata pepe kalle aliwahi kuimba kuhusu ubora wa yanga.
Kuwa wa Rais wa klabu kama yanga yenye mashabiki lukuki ndani ya nchi na nje ya nchi si kitu kidogo wala cha mzaha mzaha. Ulituahidi wanayanga tutaingia makundi huu mwaka, lakini mpaka sasa hatuoni hiyo dalili na mbaya zaidi tukihoji ni kwanini hatufuzu makundi na huku kwenye ligi tukiwa unbeaten mpaka sasa unatuita wala mihogo.
Kiufupi hutaki mashabiki wa yanga wahoji chochote kuhusu matokeo? Kisa ni unbeaten ya kwenye ligi ambayo haina mashiko kama klabu itakuwa haifanyi vizuri kimataifa ili kuakisi yale maneno ya Young Africans mabingwa wa Tanzania na Africa.
Jwaneng Galaxy ilimtoa simba tena kwa mkapa lupaso na hawakuwa na uzoefu wa aina yoyote na hayo mashindano Yanga ya Eng. Hersi inataka uzoefu gani? Vipers ya Uganda imemtoa TP Mazembe je vipers ilikuwa na uzoefu gani?
Eng. Hersi Yanga tunamafanikio sana kwa Tanzania na malengo yetu ni kuhakikisha tunaitawala Africa ili kuakisi jina letu. Hivyo basi kwakuwa ulituahidi makundi na tulipohoji juu ya uwezo wa timu kimataifa ukatuita wala mihogo, endapo hatutofikia lengo hilo kuwa muungwana kama raisi ukubali lawama na ujiuzulu nafasi yako, ili upishe wengine waje ambao wataweza kutuvusha.
Na endapo tutafuzu makundi pia ujiuzulu nafasi yako maana bado ulitutukana na huenda ukatutukana zaidi huko mbeleni kwasababu huna busara hata kidogo.
#enghersiout