KERO Eng. Kundo, nusuru maisha ya Wananchi na Watumishi Kata ya BUNAMHALA

KERO Eng. Kundo, nusuru maisha ya Wananchi na Watumishi Kata ya BUNAMHALA

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ni jambo la kusikitisha na linaloumiza moyo kuona hali ya miundombinu ya barabara na daraja katika Kata ya Bunamhala, iliyopo Wilaya ya Bariadi Mjini. Mbunge wetu, Mhe. Kundo Andrea Mathew, tunaomba utupie macho hali hii inayotishia uhai wetu.

Kama unavyoona kwenye picha na video, hapa ndipo mahali ambapo:
  • Watumishi wa umma hulazimika kupita kila siku kwenda kutoa huduma kwa jamii.
  • Wanafunzi na wagonjwa (ikiwemo akina mama wajawazito) wanahatarisha maisha yao kuvuka maji haya ya kasi.
  • Wananchi na watumishi wenzetu wamepoteza maisha kwa kusombwa na maji wakijaribu kutafuta riziki na kulitumikia taifa.
Hatuwezi kuendelea kupoteza nguvu kazi ya taifa na wapendwa wetu kwa sababu ya daraja na barabara isiyopitika wakati wa mvua.

Tunaiomba mamlaka husika (TARURA) na uongozi wa wilaya ya Bariadi Mjini kuchukua hatua za haraka kabla maisha mengine hayajapotea.

Screenshot_2026-03-23-09-20-33-64_f2cb81fb7cf38af7978f186f2a61634a.jpg
IMG_20260323_092734.jpg
 
Back
Top Bottom