Engine Oil imejaa juu ya Maximum limit

Engine Oil imejaa juu ya Maximum limit

WENYELE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,433
Reaction score
1,442
Wakuu gari iliwekewa engine oil ikawa juu ya maximum leo.

Gari ilikua na sign ya kuvujisha oil ndo maana ikawekewa nyingi lakini sasa inaonekana oil haipunguzi.

Je, hii inaweza ilaleta madhara gani kwenye engine?
 
Tegemea gari kuwa zembe zembe,chukulia picha wewe ukiwa umeshiba ndindindi
 
Hapa shida itakuwa pistons na vitu vingine kwenye engine vitakuwa havifiki chini au juu sababu vitakuwa vinaelea.
 
Pressure itakuja kuwa kubwa hapo baadae na kisha kupelekea sehemu ambazo ni dhaifu kupenyeza oil.

Leakage ya oil haitatuliwi kwa kuzidisha kiwango cha oil.

Angalia sehemu ilipokuwa inavuja hapo awali kisha ureplace hizo seals.

Na kutokuvuja kwa gari yako huenda uliweka oil ambayo ni nzito.

Nb: mimi siyo technician wala Engineer
 
Wakuu gari iliwekewa engine oil ikawa juu ya maximum leo.
Gari ilikua na sign ya kuvujisha oil ndo maana ikawekewa nyingi lakini sasa inaonekana oil haipunguzi.
Je, hii inaweza ilaleta madhara gani kwenye engine?
Kapunguze hio oil haraka vinginevyo itatafuta pa kutokea na itatoka.
Ni afadhali uweke oil pungufu (bila taa kuwaka) kuliko kuzidisha oil.
 
Hii si kweli hata kidogo, mimi nasema afadhali oil kuzidi kuliko kupungua

Madhara ya oil kuzidi hayalingani na madhara ya oil kupungua hata kidogo
 
Kiasi cha oil kinachozidi kwenye injini kinapunguza nafasi wazi iliokusudiwa kwa ajili ya hewa na mzunguko wa cranshaft kwa wepesi (injini inakuwa zito)

Kuna uwezekano mkubwa gari yako imewekewa oil nzito zaidi ya inayotumia ndio maana haivujishi kama mwanzo. Au wameweka STP.

Madhara yake ni kwa muda mrefu.
Piston rings zitazidiwa na uchafu zitashindwa kujitanua itaanza kuchelewa kuwaka na moshi.

Pia vitu vidogo vidogo kama oil prs switch itachelewa kuzima, nk.

Ni diesel au petrol?
 
Asante sana kwa majibu mazuri mkuu ni petrol
 
Wakuu gari iliwekewa engine oil ikawa juu ya maximum leo.

Gari ilikua na sign ya kuvujisha oil ndo maana ikawekewa nyingi lakini sasa inaonekana oil haipunguzi.

Je, hii inaweza ilaleta madhara gani kwenye engine?
Mkuu ndinga haina miezi ushaanza majaribio na mafundi?
 
Uko sahihi mashine yoyote inayotumia oil kwenye sehemu ya kuweka kile kizibo ki a nafasi ya upenyo wa sindano ambayo kazi yake n kutema hewa inayozalishwa kwenye engine wakati wa mchakato pia oil ikizidi hutokea hapo hapo. Na itatema hadi itakapokaa sawa mm nafikiri pengine jamaa mashine yake haitemi kiasi kilichozidi.

Back
Top Bottom