Siku nyingine ukipata matatizo ya namna hii usikimbilie kufanya engine overhaul kwani mara nyingi huwa siyo yalazima kabisa. Injini ikipitia kwenye computer scanning ikaonekana kuwa na misfirire, ni rahisi fundi asiye na uzoefu wa kutosha kucheki spark plugs tu, na au ignition coils; akikuta zote ziko sawa basi ata kuambia engine Overhaul kwa kuhisi kuwa kuwa Piston ni mbaya. Lakini mara nyingi misfire hutokana pia na ama na valve kutofunguka vizuri au timing belt kuchakaa, mambo ambayo mafundi wengi huwa hawaangalii kabisa. Uzoefu wangu kwenye engine za magari tena makuukuu sana yenye maili nyingi hata zaidi 200,000 (km300,0000) (nina autoshop yangu ya binafsi huko mitaani) ni kuwa kuna kitu kinaitwa valve lifters (tappets), ambazo huchakaa na kushindwa kusukuma valves na kusababisha misfire. Hii hutokea iwapo hauko makini kubadilisha oil wakati unaotakiwa; ukiendesha gari kwa muda mrefu na oil chafu unaweza kuharibu hizo valve lifters. Gharama yake (US Prices) kwa seti ni kati ya $40 hadi $80 kulingana na aina ya injini na wingi wake; injini moja inaweza kuwa nazo 8 (4 cylinder) mpaka 16 (8 cylinder). Halafu, kama injini yako inatumia timing belt, basi hiyo inatakiwa ibadilishwe pia kila baada ya maili 100,000 (km 150,000) kulingana na aina ya gari. Kila unapobadilisha timing belt, ni muhimu ubadilishe pia water pump, idler pulley, tensioner pulley, na vile vile air conditioning clutch. Hata kama gari yako inatumia timing chain (siyo belt), bado unatakiwa ubadilishe water-pump, idler pulley, tensioner pulley na A/C clutch kwani bearings zake hufa baada ya muda wa km150,000. Kubadilisha kwa pipes huwa siyo jambo la kawaida ila labda kama fundi afanye makosa na kuvunja pipe hiyo wakati wa kufungua kwani huwa haziharibiki kabisa..
Oil pump inatumia umeme na iko chini ya engine unaweza kuibadilisha wakati wowote bila kuangusha injini, nayo pia hufa kutokana na kutobadilisha oil kwa wakati unaotakiwa. Fuel pump imo ndani ya tanki la mafuta, ambayo pia hufa baada ya muda fulani na inaweza kubadilishwa bila kuangusha engine.
Matengezo yote hayo ni ya kawaida kwenye gari yoyote na huanza baada ya gari kufikisha maili 100000 (km150,000); hayahitaji injini kuangusha na kufanya overhaul. Engine overhaul hufanyika tu iwapo umetumia gari vibaya bila oil na kusababisha Crackshaft bearings kuungua au valves kuvunjika. Ina maana injini iangushwe chini, halafu isukwe tena upya. Matatizo yatokanayo na overhaul yoyote ni kuwa huwa inadhoofisha ubora wa injini kabisa, yaani injini haiwezi kuwa kama awali tena; zile genuine parts za piston, piston rings, na bearings za ndani ya injini unaziondoa na kuweka OEM ambazo huwa siyo nzuri kama genuine parts zilizokuwamo mwanzo. Piston unazoweka huwa hazina uzito sawa na piston ulizoondoa, na ndiyo maana engine baada ya overhauli haiwezi kufanya kama ile original.