changaule
JF-Expert Member
- Jan 10, 2020
- 6,039
- 10,151
Ni kweli timu haijakamilika lakini kuna kitu kikubwa sana kimeonekana kuliko hata watu walivyotegemea.Ila bado timu haijaimarika vya kutosha. Juzi kwenye ushindi wa goli 5 kulikuwa na makosa mengi sana ya kiufundi yaliyochangia uchache wa magoli. Eng Hersi ahakikishe timu kupitia kocha inaondoa makosa yaliyojitokeza ili kwenye mzunguko wa pili tupate magoli mengi zaidi dhidi ya Simba.
Timu imendokewa na benchi zima la ufundi lakini Eng Hersi ameweza kufanya replacement katika eneo gumu sana, vipi kuna pengo la Nabi mtu kaliona?
Kuna pengo la kocha wa viungo likionekana?
Kuna pengo la kocha wa makipa limeonekana?
Wameondoka wachezaji na wamekuja wacheza moto sana
Max, Pacome na Yao Kwasi ni kazi nzuri sana la jicho la mpira.
Mpaka hapa tutoe credit hakuna aliyetegemea timu itafikia hapa ilipo, kwavile kocha yupo na Eng. Hersi ni mtu wa mpira, bila shaka dirisha dogo litatumika kwaajili ya kurekebisha mapengo mapengo yaliyojitokeza.