Engineer Hersi Saidi ni nani haswa?

Hata Vita na Mazembe wana sajili wachezaji grade C tena kutoka Tanzania, tena wazee, waliochoka, na wameshindwa kuongezewa mikataba, kwa taarifa tu mwaka jana Vita imesajili mchezaji aliye achwa na Simba Zana Coulibaly, na mwaka huu wamesajili mchezaji aliyeachwa na Simba Deo Kanda. Hao Mazembe mwaka jana wamesajili mchezaji aliyeachwa na Azam Hamisi Singano (Mesi)
 
Nami hapa nina hoja kidogo. tuchukulie mfano mauzo ya jezi za timu kwa msimu ni laki tano (500,000/=). Kwa bei ya sasa jezi moja ni wastani wa elfu thelasini (30,000/=). jumla ya pesa ya mauzo ya jezi ni 500,000 x 30,000=15,000,000,000/=. Uwekezaji wa MO kwa mwaka ni bilioni 3 na mauzo ya jezi kwa msimu mmoja ni bilioni 15.
Wajanja wameona fursa za kupiga pesa kwenye industry ya mpira,cha msingi mashabiki tupate raha tu.
 

Maana wewe umejibu hoja aliyopaswa kujibu niliyemquote... inabidi nikuulize.. wapi nimekataa kwamba timu kubwa hazina wachezaji wa grade za chini?
 
Kwa kuongezea, pale DIT idara ya Building &Civil/Highway Engineering alikua mchezaji tegemeo idarani. Mpambano ulikua mkali kati ya Idara ya Ujenzi na Umeme!
 
Hapana haiko hivyo, mfano yanga jezi ilikuwa inauzwa elfu 35 na Gsm ndio watengenezaji na ni wasambazaji, kwa hiyo kwenye hiyo elfu 35 yanga km yanga walikuwa wanapata karibia elfu 5[na haiwezi kuzid hiyo elfu 5 kwa jezi] sina wakika vzr maana nilishasahu, ukifatilia vzr kwenye huu uzwaji wa jezi vilabu vinapata hela ndogo sana ila viongozi waliosuka ilo dili ndio wanapiga hela
 
Usipende kufuatilia mpira vibanda umiza.
Horoya ni timu kubwa kuliko Simba, jua hilo sasa.
Huyo jamaa ni mtupu alafu anajidai mjuaji, Horoya imeanzishwa 1975, Simba imeanzishwa miaka ya 1930,
Horoya ina vikombe zaidi ya 30 tokae ianzishwe, na imechukua Africa cup 1978, Horoya ina uwanja wake wenye capacity 25,000.
Hakuna cha Simba wala Yanga wa kuifananisha na Horoya, tuache ushabiki wa kitoto.
 
Hahahaha
 
Asipokuelewa na hapa tafadhaaali sana naomba umuache.
 
Kumbe muda wote nilikuwa naongea na linyani uneducated ndio sababu mgumu kuelewa
 
2011 kama sio 2012 Chelsea ananyanyua ndoo ya UEFA kwa kumuangusha Barca na hatimaye Bayern, kumbuka Bayern na Barca ndo zilikuwa kwenye peak ya hali ya juu saaana.

Hakuna wakati Chelsea ilikuwa weak kama wakati ule, cha ajabu wakanyanyua ndoo.

Kuna mwaka Dortumund alimchapaga Real Madrid 4, Madrid ikiwa imeshiba kabisa kuanzia first eleven mpaka sub.

Madrid alishawahi kulala 6 pale Bernabeu, Madrid akiwa na Ronaldo De Lima, Zinedin Zidane, Figo, Robert Carlos, Iker Cassilas n.k

Kwenye soka nakubaliana na wewe bahati ipo, unaweza ukawa na kikosi bora ila ukapigwa.

Na unaweza kikosi weak lakini ikatoka na matokeo mazuri.

Msimu uloisha tulishuhudia Yanga ikitoa Sare ya 2-2 na Simba, Yanga walikuwa na kikosi gani cha kuto ile draw? Kumbuka hakukuwa na akina Ditrum wala Morrison.
 
Hizi fedha wanazotumia kusajilia wachezaji, kuandaa siku kama ya kesho, mishahara n.k unataka GSM irudishe kwa namna ipi?
 
Tumekuwa ni wepesi wa kulalamika ila huenda tukawa hatuna elimu ya biashara kwa ujumla.

Kuendesha club kama simba au yanga au azam usifikiri ni fedha ndogo ndugu.

Hapo umetamka habari ya jezi tu, unazungumza vipi kuhusu mambo haya?

1. Kusajili wachezaji eneo la kuvunja mikataba, vilabu vyetu vina fedha ya kufanya hizi sajili?

2. Mishahara ya hawa wachezaji wa kigeni, vyanzo vya mapato vya club vinaweza kulipa mishahara hii?

3. Mishahara ya wafanyakazi je? Hapa kuanzia Administration, Management, Department n.k

4. Hujazungumzia operation costs mbalimbali ndan ya Taasisi, mafuta ya gari, kurepair majengo na vifaa n.k

Kama kuna faida wanapata hawa watu basi tambua kuwa sio kubwa sana kifedha zaidi ya wao wenyewe kujitengenezea jina tu.

TP Mazembe Mose Katumbi angebaki na utajiri wake wa madini miaka ya karibuni wala asingekuwa tishio la siasa Congo.

Ila Brand alotengeneza ndani ya Congo kupitia Club ya TP Mazembe ndio ilimpa umaarufu zaidi.

Manji akaja akawa kiongozi Mbagala. Ushawahi kujiuliza kwanini watu kama Kimei wa CRDB licha ya fedha zote walizonazo lakini wanagombea Ubunge?

Matajiri wangapi wanajiingiza ktk siasa? Sitaki nitoe mifano ya mbali, mtazame Mheshimiwa Abood, Aboos ana shida gani na ela za ubunge? Kila baada ya lisaa limoja gari moja inatoka Dar kwenda Moro, na Moro kwenda Dar.

Kuna Shabiby, kuna akina Nimrod Mkono, Andy Chenge n.k hawa wote wana fedha chafu ila unawaona wanataka nafasi tu ili kujijengea heshima ndani ya jamii au kujibrand mwenyewe na kujitengenezea CV.

Hata huyo Abramovic wa Chelsea, wale Maboss wa Man City, PSG hizi club haziwaingizii fedha nyingi saaaana ila tu wameamua kuwekeza kwa ajili ya kutengeneza nafasi ktk jamii.
 
Hizi fedha wanazotumia kusajilia wachezaji, kuandaa siku kama ya kesho, mishahara n.k unataka GSM irudishe kwa namna ipi?
Nilikuwa namjibu jamaa pale juu kuwa hela yote ya jezi inaenda club, kumbe sio kweli,
 
Kwenye mpira bahati ni asilimia 2 tu.. Vingine vyote ni uwezo. Hao Betis pamoja na kumfunga Madrid Je alichukua kombe la Ligi??

Alafu hao Horoya una hakika hawana wachezaji wazuri?? Makambo si alienda huko?? Makambo na Kagere wana tofauti gani??
 
Mpira unachezwa uwanjani ilikuwaje simba iliwatoa timu ya afrika kusini iliyokuwa na kipa aliyecheza world cup, ikawatoa zamalek waliokuwa mabingwa watetezi wa afrika, al ahly ya misri walifungwa taifa wakiwa na wachezaji wanaocheza kwa mkopo to EPL
Hujui unachozungumzs, uwekezaji na thamani ya ligi ya nchi ulizozitaja unaweza kufananisha na ligi ya Tanzania? Atakua mwekezaji mwendawazu anunue mchezaji wa bl.2 amlipe mshahara wa ml.60 kwa mwezi alafu aje kucheza ligi ya Tanzania na asububiri mechi nne za ligi ya mabingwa.
 
Siasa tu zile upewe 1.2B ukatae
While waweza tafuta mchezaji mzuri kwa 300m..
Sasa mfano kimataifa ile beki ya wawa na onyango..
Kipa manula
Striker ilamfya na magulu???

Maana kagere na boko jua lishazama kimataifa.
Mkuu, Dewj ana utajiri wa karibu Trilion 4 huko , billion moja kwake sii kitu kabisa, hapo simba kwa mwaka anatoa pesa yake mfukoni bil 3 kuendesha club,
club yeyote inayotaka kupiga hatua haiwez simama kwa kuuza wachezaj wake muhimu

na kama unadhani ni jambo jepesi kuwapata watu kama Konde boy.. waambie hao waliotoa hiyo bil wawatafute, watawapata watatu

TP Mazembe yenyewe kuuza mchezaj tegemeo ni mziki mzito
 
Hivi unaelewa ulichozungumza au umeandika ili mradi uonekane umeandika
 
Siasa tu zile upewe 1.2B ukatae
While waweza tafuta mchezaji mzuri kwa 300m..
Sasa mfano kimataifa ile beki ya wawa na onyango..
Kipa manula
Striker ilamfya na magulu???

Maana kagere na boko jua lishazama kimataifa.
Onyango anatoka kenya anakuja kama akiwa Mchezaji MVP wa kenya premier league.. Ametoka Gor Mahia sio Ndanda

Huyo mkongoman ndani ya msimu mitatu ana goli 44.. hapo hapo amepata injuries ndefu sana, na kufungiwa juu, na sawa tuseme kapata hizo goli kwenye misimu 2, nitafutie wachezaj wenye hizo data hapa Africa wako wangapi.. usipayuke tu
 
Mamelodi kama wangeona hafai wasingeenda FIFA kudai Mchezaji wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…