Nami hapa nina hoja kidogo. tuchukulie mfano mauzo ya jezi za timu kwa msimu ni laki tano (500,000/=). Kwa bei ya sasa jezi moja ni wastani wa elfu thelasini (30,000/=). jumla ya pesa ya mauzo ya jezi ni 500,000 x 30,000=15,000,000,000/=. Uwekezaji wa MO kwa mwaka ni bilioni 3 na mauzo ya jezi kwa msimu mmoja ni bilioni 15.
Wajanja wameona fursa za kupiga pesa kwenye industry ya mpira,cha msingi mashabiki tupate raha tu.
Tumekuwa ni wepesi wa kulalamika ila huenda tukawa hatuna elimu ya biashara kwa ujumla.
Kuendesha club kama simba au yanga au azam usifikiri ni fedha ndogo ndugu.
Hapo umetamka habari ya jezi tu, unazungumza vipi kuhusu mambo haya?
1. Kusajili wachezaji eneo la kuvunja mikataba, vilabu vyetu vina fedha ya kufanya hizi sajili?
2. Mishahara ya hawa wachezaji wa kigeni, vyanzo vya mapato vya club vinaweza kulipa mishahara hii?
3. Mishahara ya wafanyakazi je? Hapa kuanzia Administration, Management, Department n.k
4. Hujazungumzia operation costs mbalimbali ndan ya Taasisi, mafuta ya gari, kurepair majengo na vifaa n.k
Kama kuna faida wanapata hawa watu basi tambua kuwa sio kubwa sana kifedha zaidi ya wao wenyewe kujitengenezea jina tu.
TP Mazembe Mose Katumbi angebaki na utajiri wake wa madini miaka ya karibuni wala asingekuwa tishio la siasa Congo.
Ila Brand alotengeneza ndani ya Congo kupitia Club ya TP Mazembe ndio ilimpa umaarufu zaidi.
Manji akaja akawa kiongozi Mbagala. Ushawahi kujiuliza kwanini watu kama Kimei wa CRDB licha ya fedha zote walizonazo lakini wanagombea Ubunge?
Matajiri wangapi wanajiingiza ktk siasa? Sitaki nitoe mifano ya mbali, mtazame Mheshimiwa Abood, Aboos ana shida gani na ela za ubunge? Kila baada ya lisaa limoja gari moja inatoka Dar kwenda Moro, na Moro kwenda Dar.
Kuna Shabiby, kuna akina Nimrod Mkono, Andy Chenge n.k hawa wote wana fedha chafu ila unawaona wanataka nafasi tu ili kujijengea heshima ndani ya jamii au kujibrand mwenyewe na kujitengenezea CV.
Hata huyo Abramovic wa Chelsea, wale Maboss wa Man City, PSG hizi club haziwaingizii fedha nyingi saaaana ila tu wameamua kuwekeza kwa ajili ya kutengeneza nafasi ktk jamii.