English Grammar: Benki ya Posta Tanzania ni TPB Bank au TPBank? Ni sahihi kwa neno "bank" kutumika mara mbili?

English Grammar: Benki ya Posta Tanzania ni TPB Bank au TPBank? Ni sahihi kwa neno "bank" kutumika mara mbili?

Wangeandika TP bank wangepata tabu sana kueleweka na watu, maana hiyo TPB Bank ndio watu walikuwa wakiita hivyo, na wenyewe wakaamua kunata na biti hivyo hivyo. Wangefanya rebranding kujiita TP bank wangechanganya watu, wangedhani ni bank mpya
Nina mashaka sana na jibu lako. Ila asante kwa mchango wako anyway
 
Branches nyingine za TPB kwakweli mnafifisha ustawi wa Bank, huwezi demand national identity card pekee katika kufanya forex, wakati benki nyingine hawafanyi hivyo?? Yaani mhudumu anakuambia bila National ID hakuna forex. huo ni uhujumu usio na maana.

Sasa na ww kwann huna National ID mpaka leo kwan ni shilling ngap kupata national ID!?
 
Sasa na ww kwann huna National ID mpaka leo kwan ni shilling ngap kupata national ID!?
Ninayo, ila sio kila anayetaka forex anayo National ID. Ukiweka hiyo condition unapunguza wateja wakati benki nyingine hazina hayo masharti.
 
Alafu nasikia hii hii logo ya bank ilitumia pesa nying sana kuwa designed.
 
Mwaka 1990 nilikuwa na Tshs 2,600 TPB ambazo sikuwahi kuzitumia baada ya kuwa nimemaliza chuo. Halafu mwaka 1996 niliacha Tshs 3,800,000 pale NBC Ubungo na TShs 2,700,000 pale THB Ohio. Leo ni zaidi ya miaka 20 tangu nimeziacha na nategemea thamani yake itakuwa imepanda sana kwani wakati huo Shilingi ilikuwa na thamani ya dola 1 kwa shilingi 250 tu.Je ninaweza kweli kuzipata au ndiyo hivyo wajanja wa benki wameshatia ndani.
 
Nina mashaka sana na jibu lako. Ila asante kwa mchango wako anyway
Hivi kwa mtanzania averaga tu, ambaye kazoea kusema Naenda benki ya TPB (hapo naye keshatumia neno bank mara mbili bila kujua)
Akisikia unamuambia karibu TP Bank ataelewa kuwa unamaanisha TPB? So inabidi watumie TPB Bank, na hawawezi kutumia TPB tu kwenye promotions kwa sababu mtu atajiuliza TPB ndio nini? Ni chuo cha fedha, microfinance au nini? So lazima atumie TPB na kisha na neno bank

TPB sababu ya brand kubwa (jina lililozoeleka na wateja)

Bank sababu ya kuitambulisha kama bank kwa ambao hawajawahi kuisikia
 
Hiko hivi kwa sasa TPB Bank inasimama kama jina linalojitegemea na sio Tanzania Postal Bank kama ilovyokuwa awali na jina lake kamili ni TPB Plc Bank ni sawa na NMB Plc Bank zamani ilikuwa ni National Microfinance Bank sasa kwa kuwa dhumuni lake sio kuwa benki ya makabwela tena wamehamua kubaki na jina ambalo ni brand yao kibiashara ambayo ni NMB na kuongeza neno benki mbele the same to CRDB, DCB na nyingine

Hamna kosa lolote hapo la grammar ni biashara ndio imetumika hapo
 
wamehamua kubaki na jina ambalo ni brand yao kibiashara ambayo ni NMB na kuongeza neno benki mbele
Kwenye logo ya NMB hakuna neno Bank kwa mbele
IMG_20190803_191012_232.jpg
 
Vifupipisho vinaweza maanisha chochote, ili kutilia mkazo kwenye unachotaka kumaanisha ukiwa unatumia kifupisho neno Bank ni muhimu kuliweka mwisho... Ukilitamka kwa urefu hupaswi kurudia Bank mara mbili...

TPB Bank ni sahihi... Tanzania Postal Bank ni sahihi...

TPB pekee inaweza maanisha chochote... Tanzania Postal Bank Bank yaweza kua Tanzania Postal Bank's...



Cc: mahondaw
 
Vifupipisho vinaweza maanisha chochote, ili kutilia mkazo kwenye unachotaka kumaanisha ukiwa unatumia kifupisho neno Bank ni muhimu kuliweka mwisho
Kwenye Logo ya Diamond Trust Bank neno DTB lipo pekee. Hakuna neno Bank lililowekwa mwisho
 
Back
Top Bottom