ENOKO: Duniani mpaka mbingu ya 10

ENOKO: Duniani mpaka mbingu ya 10

Ukisoma kwenye Biblia, ni watu wawili tu ndiyo ambao hawakuwahi kuonja mauti, nao ni Nabii Eliya na Enoko. Mungu hakutaka kuwaua, aliwatwaa na kuwapeleka mbinguni.

Sasa kama ilivyo kwa manabii, wafalme wa zamani na watumishi wengine kuandika vitabu vyao, basi naye Enoko aliandika kitabu chake kiitwacho Enoko.

Okay! Ngoja turudi kidogo kupeana somo. Unapoiona Biblia, jua ni mkusanyiko wa vitabu mbalimbali, kuanzia vile vya zamani sana mpaka vilivyofuatia, yaani vimebeba stori inayoendelea mpaka mwisho wa kila kitu.

Yaani kitabu cha Mwanzo kinazungumzia mwanzo wa dunia hii na kitabu cha Ufunuo ambacho ni cha mwisho kinaelezea mwisho wa dunia hii. Nadhani umenipata.

Biblia ilikuwa ni mkusanyiko wa vitabu zaidi ya hivi unavyoviona ila baadaye mtawala Costantine aliyekuwa akitawala Nicaea akaamua kukitoa kitabu cha Enoko kwenye Biblia, hiyo ilikuwa mwaka 325 Baada ya Kristo.
Hii inamaanisha nini?

Kabla ya hapo, Biblia ilikuwa na vitabu vingi lakini baada ya huyu mtawala kuingia, akaamua kuvitoa baadhi yake, na miongoni mwa vile ambavyo vilitolewa kilikuwemo hiki cha Enoko.

Kwa nini kitabu hiki kilitolewa? Hilo ni jambo jingine ambalo nitakuja kulielezea humu baadaye, iwe mitandaoni ama kwenye App yangu ambayo ipo njiani.

Humo kutakuwa na stori hizi nyingi sana za kuupa mwanga ubongo wako.

Ukisoma kitabu cha Enoko, anasimulia kuanzia mwanzo mpaka mwisho, jinsi alivyotokewa na malaika wawili, na kama ilivyo kwa malaika wote wanapowatokea wanadamu huanza na neno “Usiogope”.
Kwa nini?

Ni kwa sababu malaika ana muonekano wa kutisha, kwa binadamu, huwezi kuwa kawaida tu unapomuona malaika ametokea mbele yako, ndiyo maana husema usiogope.

Aliambiwa Mariamu Magdalena pia.

Enoko alianza kuwaelezea malaika ambao walikwenda chumbani kwake wakati amelala. Kwanza walikuwa wakubwa, wenye mbawa lakini sura zao zilikuwa na mng’ao mkubwa kama jua lakini macho yao yalikuwa yanawaka kama taa. Katika maisha yake, anasema hakuwahi kuwaona viumbe wakubwa namna hiyo.
Lipsi zao zilikuwa na moto, mbawa zao zilikuwa na mchanganyiko wa rangi mbili, zambarau na dhahabu inayong’aa kupita kawaida, mikono yao ilikuwa ni meupe kama theluji.

Hebu fikiria unakutana na kiumbe kama hicho, hutoogopa? Ndiyo maana walimwambia kwanza, usiogope.

Anasema malaika hao walisimama pembeni ya kitanda chake na kumuita kwa jina lake, Enoko akainuka na kuwaangalia.
Enoko aliogopa, anasema uso wake ulitetemeka mno lakini malaika mmoja akamwambia: “Usiogope”.

Walimwambia walitumwa na Mungu kumchukua na kumpeleka mbinguni, kwa yote ambayo angekutana nayo huko basi angewaambia watoto wake, wajukuu na vizazi vyote mbeleni.

Anasema hakutaka kuwapinga, akatoka na kwenda kuonana na watoto wake, Mathusal, Regim na Gaidad, akawaambia kuhusu malaika hao na kile walichomwambia, baada ya hapo, wakamchukua na kuanza kupaa naye kwa kumbeba kwenye mbawa zao.

Malaika wale walimchukua mpaka juu kabisa, na tazama akaanza kuingia kwenye mbingu ya kwanza. Hapa akakutana na bahari kubwa, anasema ukubwa wa bahari ile ni tofauti na bahari ambayo sisi tunayo hapa duniani.

Okay acha turudi nyuma.
Niliwaambia hii dunia imezungukwa na kioo kikubwa sana kinachoitwa firmament ambapo juu yake kuna maji mengi. Ukisoma kitabu cha Mwanzo, kinasema kipindi cha Nuhu milango ya mbinguni ikafunguliwa na maji kujaa duniani.

So hiyo milango ipo wapi? Ndiyo kwenye hiyo firmament ambayo wanasayansi walijaribu kuivunja kwenye mission za mbalimbali ili watoke nje waone kuna nini, ila hawakufanikiwa.

So juu ya hiyo firmament, kwenye hayo maji mengi aliyoyaona Enoko ndiyo mbingu ya kwanza.

Anasema ilikuwa ni bahari kubwa ambayo hakuna mfano wake.

Anasema baada ya kuiona hiyo bahari kubwa, akashangaa kuwaona malaika mia mbili wakija kule walipokuwa, malaika hawa ndiyo ambayo wanazitawala nyota zote.

Hapa kuna malaika wa aina mbili, wale wanaopaa juu ya bahari na wale ambao wanapita hata ndani ya bahari lakini kwa pamoja kuna wakati unafika na kuungana pamoja.

Wakati anaangalia mbele, macho yake yakatua kwenye nyumba moja kubwa ambayo imetengenezwa kwa barafu tu, malaika wengine walikuwa wakiruka na kwenda kwenye nyumba hiyo ambayo ilikuwa ni ya kupendeza mno machoni mwake.

Pia akaonyeshwa nyumba nyingine nzuri, ilikuwa ni ya kumeremeta kana kwamba ilijengwa kwa kutumia mafuta. Nyumba hii ilikuwa na maua mengi mazuri ambayo hata mengine hayapo hapa duniani.

Mbali na hilo, pia kulikuwa na malaika wakubwa waliokuwa wakiilinda nyumba hiyo.
Mimi kama Nyemo mnajiuliza: “Malaika hao wanailinda nyumba hiyo dhidi ya nani? Sijui”.

Baada ya hapo Enoko anasema baada ya kuyaona hayo yaliyokuwepo kwenye mbingu ya kwanza, sasa malaika hao wawili wakamchukua na kumpeleka kwenye mbingu ya pili.

Itaendelea....

View attachment 3064183View attachment 3064184View attachment 3064185View attachment 3064186View attachment 3064187View attachment 3064188View attachment 3064189View attachment 3064190
Uzi mzuri...
 
Fiksi mwanzo, kati na mwisho.

Eric Shigongo naye akiandika kuhusu miungu, si ajabu akaitwa nabii na watu wakasema neno lake ni la mungu.
 
Chai kama chai nyingine nying za jf
 
SEHEMU YA 02

Enoko anaendelea kusema kwamba malaika wale wawili wakamchukua na kumpeleka kwenye mbingu ya pili na huko akakutana na haya mambo.

Kwanza kulikuwa na giza kubwa, giza ambalo duniani hakuna lakini pia akawaona malaika wakiwa wamening’inizwa kwa staili ya kunyongwa, kufungwa na minyororo huku wakitazamwa na wengine waliokuwa wamesimama.

Hapa ngoja nikwambie kitu kimoja. Hao malaika hawakuwa kama hawa tunaowasoma sehemu mbalimbali, hawa ni malaika ambao kwa kuwaangalia walionekana kuchoka sana, weusi, na muda wote walikuwa wakilia machozi meusi tii, na wanalia kila dakika. Yaani pamoja na kunyongwa huko, hawakuwa wamekufa.

Enoko akauliza hawa ni akina nani? Akajibiwa kwamba ni baadhi ya wale malaika waliotaka kupambana na Mungu, wamechukuliwa na kuning’inizwa hapo wakisubiri hukumu siku ya mwisho.

Okay! Sasa hapa mimi kama Nyemo najiuliza kitu. Hawa malaika wataonekana tena mbingu ya tano, na wengine watatu walishushwa duniani. Swali ninalojiuliza ni moja. Kwa nini Mungu aliamua wengine kuwaacha mbinguni wakiteseka na wengine kuwashusha duniani? Ngoja tuendelee kwanza.

Wengine walikuwa wakimwambia Enoko: “Mtu wa Mungu, tuombee kwa Mungu atusamehe!”

Enoko akawa anawajibu: “Mimi ni nani mpaka niwaombee? Ni binadamu, nisiyekuwa na lolote lile. Kama nikiwaombea ninyi, nani ataniombea mimi?”

Baada ya hapo malaika hao wakamchukua na kumpeleka mbingu ya tatu. Huko akakutana na sehemu iliyotawaliwa na miti mingi mizuri iliyokuwa inamea matunda mazuri, ni kama bustani kubwa sana. Ilipendeza machoni mwake, ilikuwa ni sehemu ambayo ilimvutia kila alipokuwa akiiangalia.

Katikati ya bustani hiyo kulikuwa na mti mkubwa wa uhai, ni kama ule ambao uliwekwa kwenye bustani ya Eden ambapo kama Adam na Hawa wangekula hakika wasingekufa.

Mti huo ulikuwa na muonekano wa tofauti na miti yetu ya duniani. Ulikuwa kama umetengenezwa kwa mafuta yanayoteleza lakini pia ulionekana kuwa na muonekano wa dhahabu.

Mti huo ulikuwa na uwezo wa kuotesha kila aina ya tunda unalolijua wewe na usilolijua katika maisha yako. Pia katika bustani hiyo kulikuwa na mito, si ya maji, bali ilikuwa ni ya asali na maziwa.

Na pia kulikuwa na mingine ambayo ilikuwa inatiririsha mafuta na mvinyo (wine). Ukiachana na hiyo, pia kulikuwa na malaika mia tatu ambao walikuwa wanaitunza bustani hiyo kubwa huku wakiimba kila wakati.

Kwa namna walivyokuwa wakiimba, Enoko anasema hakuwahi kuona ama kusikia mtu duniani akiimba kama hivyo.

Hiyo ndiyo sehemu ambayo watakatifu watakwenda na kuishi. Yaani kama wewe unatenda mema duniani, utakwenda kuishi kwenye bustani hiyo milele na milele.

Baada ya hapo, malaika wale wakamchukua na kumpeleka upande wa Kaskazini mwa mbingu ile ya tatu. Sasa huko ndipo wale wasiokuwa watakatifu walipokuwa wanahifadhiwa, ndipo jehanamu ilipo.

Enoko anasema alipopelekwa huko, aliogopa kwa kuwa ilionekana kuwa sehemu iliyojaa mateso makubwa ambayo hakuwahi kuyaona. Mwanga pekee uliokuwa ukipatikana ni wa moto ambao ulikuwa unaunguza kila kilicho humo.

Pia kulikuwa na mto, huu haukuwa wa maji bali mto wa moto. Kulikuwa na moto kila kona. Ila mbali na moto huo, pia kulikuwa na barafu kila sehemu. Yaani kulikuwa na mateso ya aina mbili ambayo watu walikuwa wakiyapata. Ya kuunguzwa sana na moto lakini pia ya kupigwa na baridi kali kiasi cha kuganda kabisa.

Moto haukuwa ukiyeyusha barafu zile, watu walipigwa na vitu vyote hivyo viwili kwa wakati mmoja. Watu walikuwa wakilia kwa majuto lakini pia walilia kwa sababu ya kiu kali waliyokuwanayo.

Pia kulikuwa na malaika asiyekuwa na huruma hata kidogo, aliyeogopwa, mwenye hasira na alishika silaha kubwa kwa ajili ya kuwatesea watu.

Enoko akasema: “Hii sehemu imejaa mateso makubwa mno” na malaika akamwambia: “Hii ni sehemu ya watu waliotenda maovu duniani, watu ambao hawakumuheshimu Mungu sehemu ya wachawi, waovu, wabakaji, wala rushwa, matapeli na wengineo.”

Baada ya kuyaona hayo yote, malaika wale wakanichukua na kunipeleka mbingu ya nne.

Itaendelea kesho.
Kuamini hizi story inakubidi uwe na akiri hatarishi
 
tazama akaanza kuingia kwenye mbingu ya kwanza. Hapa akakutana na bahari kubwa, anasema ukubwa wa bahari ile ni tofauti na bahari ambayo sisi tun
Kwa wale wafuatiliaji wa science , Kuna hii microscope yenye kuitwa Nini sijui ambayo ndiyo imeleta mapinduzi kuhusu idadi ya sayari,juzi wamekuja na jipya kwamba angani Kuna bahari kubwa sana kuliko hizi tulizonazo Duniani, so Kuna kitu hapa ila tungoje mda,Bado Kuna Siri nyingi sana
 
Tuwekee chanzo cha hiyo habari yako usijekuta umeitoa tbc 😁
 
KWA hekima YA wanadamu ndiyo; kwa hekima YAKE HAPANA. MUNGU si MWANADAMU hata aseme uongo
Hili jibu lako ni la kisiasa sana, hebu kua direct aisee achana na mambo ya hekima ambayo haina kipimo maalum
 
This Mungu story is what we call "manufactured reality".

Ni uongo fulani tulioukuza wenyewe mpaka ukaonekana kama ukweli.
Mkuu shukrani sana kwa kitabu cha James kugel how to ready a bible

Nimekisoma na nimejifunza mengi sana, kama utakuwa unafaham vitabu vyengine vyenye mfanana na hicho unaweza kunitajia nikavitafita 🙏
 
Hili jibu lako ni la kisiasa sana, hebu kua direct aisee achana na mambo ya hekima ambayo haina kipimo maalum
Mshana jr nampenda sana ; ni BINADAMU YUKO WAZI sana. Nyie mnatumia NGUVU NYINGI mno KWA SABABU hamko WAZI. HAKUNA watu ninaowachukia KAMA WATU wanafiki, AU wachawi
 
Mkuu shukrani sana kwa kitabu cha James kugel how to ready a bible

Nimekisoma na nimejifunza mengi sana, kama utakuwa unafaham vitabu vyengine vyenye mfanana na hicho unaweza kunitajia nikavitafita 🙏
Asante mkuu,

Umesoma "Philosophy of Religion: An Anthology"?

Kama hujasoma naki attach hapa.

Mimi napenda sana chapter ya "The Problem of Evil"

PART IV The Problem of Evil page 276
 
Attachments

Back
Top Bottom