Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shukrani sana mkuuAsante mkuu,
Umesoma "Philosophy of Religion: An Anthology"?
Kama hujasoma naki attach hapa.
Mimi napenda sana chapter ya "The Problem of Evil"
PART IV The Problem of Evil page 276
Anytime.Shukrani sana mkuu
Kijana uko sawa??Mshana jr nampenda sana ; ni BINADAMU YUKO WAZI sana. Nyie mnatumia NGUVU NYINGI mno KWA SABABU hamko WAZI. HAKUNA watu ninaowachukia KAMA WATU wanafiki, AU wachawi
Hivyo kuna kitu nyuma yake kwanini isiwe chekundu?Chochote cheusi kishakuwa ni alama mbaya. Iwe kwa VIUMBE hai,mimea na vingine vingi. Nimesomea wanyama pori. Kila kiumbe kizuri,kinaanza na neno white.
laSEHEMU YA 02
Enoko anaendelea kusema kwamba malaika wale wawili wakamchukua na kumpeleka kwenye mbingu ya pili na huko akakutana na haya mambo.
Kwanza kulikuwa na giza kubwa, giza ambalo duniani hakuna lakini pia akawaona malaika wakiwa wamening’inizwa kwa staili ya kunyongwa, kufungwa na minyororo huku wakitazamwa na wengine waliokuwa wamesimama.
Hapa ngoja nikwambie kitu kimoja. Hao malaika hawakuwa kama hawa tunaowasoma sehemu mbalimbali, hawa ni malaika ambao kwa kuwaangalia walionekana kuchoka sana, weusi, na muda wote walikuwa wakilia machozi meusi tii, na wanalia kila dakika. Yaani pamoja na kunyongwa huko, hawakuwa wamekufa.
Enoko akauliza hawa ni akina nani? Akajibiwa kwamba ni baadhi ya wale malaika waliotaka kupambana na Mungu, wamechukuliwa na kuning’inizwa hapo wakisubiri hukumu siku ya mwisho.
Okay! Sasa hapa mimi kama Nyemo najiuliza kitu. Hawa malaika wataonekana tena mbingu ya tano, na wengine watatu walishushwa duniani. Swali ninalojiuliza ni moja. Kwa nini Mungu aliamua wengine kuwaacha mbinguni wakiteseka na wengine kuwashusha duniani? Ngoja tuendelee kwanza.
Wengine walikuwa wakimwambia Enoko: “Mtu wa Mungu, tuombee kwa Mungu atusamehe!”
Enoko akawa anawajibu: “Mimi ni nani mpaka niwaombee? Ni binadamu, nisiyekuwa na lolote lile. Kama nikiwaombea ninyi, nani ataniombea mimi?”
Baada ya hapo malaika hao wakamchukua na kumpeleka mbingu ya tatu. Huko akakutana na sehemu iliyotawaliwa na miti mingi mizuri iliyokuwa inamea matunda mazuri, ni kama bustani kubwa sana. Ilipendeza machoni mwake, ilikuwa ni sehemu ambayo ilimvutia kila alipokuwa akiiangalia.
Katikati ya bustani hiyo kulikuwa na mti mkubwa wa uhai, ni kama ule ambao uliwekwa kwenye bustani ya Eden ambapo kama Adam na Hawa wangekula hakika wasingekufa.
Mti huo ulikuwa na muonekano wa tofauti na miti yetu ya duniani. Ulikuwa kama umetengenezwa kwa mafuta yanayoteleza lakini pia ulionekana kuwa na muonekano wa dhahabu.
Mti huo ulikuwa na uwezo wa kuotesha kila aina ya tunda unalolijua wewe na usilolijua katika maisha yako. Pia katika bustani hiyo kulikuwa na mito, si ya maji, bali ilikuwa ni ya asali na maziwa.
Na pia kulikuwa na mingine ambayo ilikuwa inatiririsha mafuta na mvinyo (wine). Ukiachana na hiyo, pia kulikuwa na malaika mia tatu ambao walikuwa wanaitunza bustani hiyo kubwa huku wakiimba kila wakati.
Kwa namna walivyokuwa wakiimba, Enoko anasema hakuwahi kuona ama kusikia mtu duniani akiimba kama hivyo.
Hiyo ndiyo sehemu ambayo watakatifu watakwenda na kuishi. Yaani kama wewe unatenda mema duniani, utakwenda kuishi kwenye bustani hiyo milele na milele.
Baada ya hapo, malaika wale wakamchukua na kumpeleka upande wa Kaskazini mwa mbingu ile ya tatu. Sasa huko ndipo wale wasiokuwa watakatifu walipokuwa wanahifadhiwa, ndipo jehanamu ilipo.
Enoko anasema alipopelekwa huko, aliogopa kwa kuwa ilionekana kuwa sehemu iliyojaa mateso makubwa ambayo hakuwahi kuyaona. Mwanga pekee uliokuwa ukipatikana ni wa moto ambao ulikuwa unaunguza kila kilicho humo.
Pia kulikuwa na mto, huu haukuwa wa maji bali mto wa moto. Kulikuwa na moto kila kona. Ila mbali na moto huo, pia kulikuwa na barafu kila sehemu. Yaani kulikuwa na mateso ya aina mbili ambayo watu walikuwa wakiyapata. Ya kuunguzwa sana na moto lakini pia ya kupigwa na baridi kali kiasi cha kuganda kabisa.
Moto haukuwa ukiyeyusha barafu zile, watu walipigwa na vitu vyote hivyo viwili kwa wakati mmoja. Watu walikuwa wakilia kwa majuto lakini pia walilia kwa sababu ya kiu kali waliyokuwanayo.
Pia kulikuwa na malaika asiyekuwa na huruma hata kidogo, aliyeogopwa, mwenye hasira na alishika silaha kubwa kwa ajili ya kuwatesea watu.
Enoko akasema: “Hii sehemu imejaa mateso makubwa mno” na malaika akamwambia: “Hii ni sehemu ya watu waliotenda maovu duniani, watu ambao hawakumuheshimu Mungu sehemu ya wachawi, waovu, wabakaji, wala rushwa, matapeli na wengineo.”
Baada ya kuyaona hayo yote, malaika wale wakanichukua na kunipeleka mbingu ya nne.
Itaendelea kesho.
Watu weusi tuna shida. Kila kilicholaaniwa na kibaya ni cheusi. Duh!hawa ni malaika ambao kwa kuwaangalia walionekana kuchoka sana, weusi, na muda wote walikuwa wakilia machozi meusi tii, na wanalia kila dakika. Yaani pamoja na kunyongwa huko, hawakuwa wamekufa.
Hivi wanatuchukuliaje?Na Shetani ni mweusi
Hivi wanatuchukuliaje?
Kumbukumbu zangu ni kwamba bikra maria ndo alitokewa na malaika hyo ipo kwenye kitabu cha luka toka sura ya kwanza, kuhusu magdalena labda nimesahauMkuu,naomba unikumbushe mistari ya bibie ambayo inaeleza jinsi Maria Magdalena alivyotokewa na malaika.Amen mtumishi. 🙏
Unawatofautishaje Maria Magdalena na Maria mama wa Yesu?Au ni mmoja?Kumbukumbu zangu ni kwamba bikra maria ndo alitokewa na malaika hyo ipo kwenye kitabu cha luka toka sura ya kwanza, kuhusu magdalena labda nimesahau
Jamaa amekwambia subiri app yake. Andaa mchuuuziHicho kitabu cha Henoko kinapatikana wapi siku hizi
Ni watu wawili tofauti, mariam Magdalena ana historia ndefu lkn kwa kifup ndo yule mwanamke kahaba aliemfuta yesu miguu kwa machozi yake, na ndie aliekutana na yesu wakwanza baada ya kufufuka, na ndie aliepamba kaburi la yesu kwa manemane. Hayo yote yalitokea baada ya historia ndefu nyuma yakeUnawatofautishaje Maria Magdalena na Maria mama wa Yesu?Au ni mmoja?
Unadai kuwa hiki kitabu kiliondolewa mnamo mwaka 325 K.K., sasa wewe ulikipataje na kukisoma?Ukisoma kwenye Biblia, ni watu wawili tu ndiyo ambao hawakuwahi kuonja mauti, nao ni Nabii Eliya na Enoko. Mungu hakutaka kuwaua, aliwatwaa na kuwapeleka mbinguni.
Sasa kama ilivyo kwa manabii, wafalme wa zamani na watumishi wengine kuandika vitabu vyao, basi naye Enoko aliandika kitabu chake kiitwacho Enoko.
Okay! Ngoja turudi kidogo kupeana somo. Unapoiona Biblia, jua ni mkusanyiko wa vitabu mbalimbali, kuanzia vile vya zamani sana mpaka vilivyofuatia, yaani vimebeba stori inayoendelea mpaka mwisho wa kila kitu.
Yaani kitabu cha Mwanzo kinazungumzia mwanzo wa dunia hii na kitabu cha Ufunuo ambacho ni cha mwisho kinaelezea mwisho wa dunia hii. Nadhani umenipata.
Biblia ilikuwa ni mkusanyiko wa vitabu zaidi ya hivi unavyoviona ila baadaye mtawala Costantine aliyekuwa akitawala Nicaea akaamua kukitoa kitabu cha Enoko kwenye Biblia, hiyo ilikuwa mwaka 325 Baada ya Kristo.
Hii inamaanisha nini?
Kabla ya hapo, Biblia ilikuwa na vitabu vingi lakini baada ya huyu mtawala kuingia, akaamua kuvitoa baadhi yake, na miongoni mwa vile ambavyo vilitolewa kilikuwemo hiki cha Enoko.
Kwa nini kitabu hiki kilitolewa? Hilo ni jambo jingine ambalo nitakuja kulielezea humu baadaye, iwe mitandaoni ama kwenye App yangu ambayo ipo njiani.
Humo kutakuwa na stori hizi nyingi sana za kuupa mwanga ubongo wako.
Ukisoma kitabu cha Enoko, anasimulia kuanzia mwanzo mpaka mwisho, jinsi alivyotokewa na malaika wawili, na kama ilivyo kwa malaika wote wanapowatokea wanadamu huanza na neno “Usiogope”.
Kwa nini?
Kiliondolewa kwenye biblia na kuhifadhiwa(tuite kufichwa?).Kipo.Unadai kuwa hiki kitabu kiliondolewa mnamo mwaka 325 K.K., sasa wewe ulikipataje na kukisoma?
Tutumie na sisi soft copy tukisome.
Nitumie basi soft copyKiliondolewa kwenye biblia na kuhifadhiwa(tuite kufichwa?).Kipo.
NB:Kila niionapo id yako inanikumbusha mikoa ya Tabora,Mwanza na Shinyanga enzi hizo za jeshi la sungusungu lilipokua linawasensemya wahalifu/wakosaji.
Mimi sina mkuu.Nitumie basi soft copy
Watu walijuaje kama ni musa na eliyaUkiangalia kwa jicho la ndani, uwezekano mkubwa ni kwamba hata Mussa naye pia hakufa bali alichukuliwa akiwa mzima na Mungu mwenyewe, huku Mungu akiwa na sababu zake maalumu za kuwaambia Waisrael kuwa "Mussa mtumishi wangu amekufa"
Ndiyo maana pale kilimani walipokuwa wapo na Yesu, Petro aliwaona Musa na Eliya
Karama ya rohoni; Petro aliwatambuaWatu walijuaje kama ni musa na eliya