Enyi Manabii wa kizazi kipya ni kweli mmepewa nguvu na Mwenyezi Mungu, au ni ushirikina tu?

Badala yake, hii ni taswira au lugha ya kiroho inayoelezea huruma na kusikiliza kwa upendo wa Mungu kuelekea wale wanaomngojea kwa subira
Kwa hiyo kuna jinsi mungu huyo anasikiliza kwa upendo?
Kitendo cha kusema kusikiliza kwa upendo kinatoa ishara ya kusikiliza kwa makini!
Kama unasikiliza kwa makini ina maana at first place ulikosa kusikiliza kwa makini.
Huoni unatoa sifa ya mungu kuwa anasikia kila kitu?
Tuendelee kukaa hapo hapo kwenye angle ya lugha ya taswira.
 
Mungu angekuwepo, kila mtu angemjua bila utata.

Ukishaona Mungu anaanza kuelezewa, kuhubiriwa, kutangazwa, ujue hizo ni siasa na hadithi za watu tu.
• Kutoamini uwepo wa Mungu ni mtazamo wako binafsi, na inaweza kutokana na sababu mbalimbali kama vile uzoefu wako wa maisha, elimu yako, au mitazamo yako ya kitamaduni. Kwa hiyo siwezi nikakulazimisha umwamini mungu.

• Lakini Hapa kuna mifano michache:
Yohana 14:1 (Biblia Takatifu): "Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, mwaminini mimi."

Marko 11:22 (Biblia ya King James Version): "Yesu akawajibu, akawaambia, Mwaminini Mungu."

Waefeso 1:12 (Neno: "ili sisi tuwe za sifa za utukufu wake, sisi tuliotangulia kutumaini katika Kristo.")
 
Ni matapeli wa kimtandao wengi wakiwa ni raia wa Nigeria.

Walikuwa wanatumia account fake za yahoo zenye majina mbali mbali kutapeli watu kwa mtandao huo.
Okay mkuu, hapo nimekuelewa ✍️✍️.
 
Manabii wa zamani walishindana
Wewe Nabii wa uongo pia. Nabii wa ukweli aliwashinda manabii wa uongo wa Baali Wewe kama Nabii wa Ukweli inakuwaje manabii wa uongo Wana wafuasi wengi kuliko kikanisa chako au mikutano Yao ya nje wanajaza watu wengi kuliko wewe ukiitisha kimkutano chako Cha nje ? Manabii wa uongo wamekuzidi nguvu? inakuwaje mfano.manabii wa uongo wanajaza watu kibao mikutano Yao wakati nyie mnajiite wa ukweli mnajaza tu mikutano yenu watu wanasali dini yenu ndio wanakuwa wengi kuliko wageni? Hivi mjiulize Mungu wa Eliya Yuko wapi aliyeshinda washirikina manabii wa Baali?

Mungu wa Musa yoko wapi aliyewashinda wachawi na waganga wa Misri

Wewe huna nguvu za Mungu za kuwashibda wachawi na washirikina wa Tanzania umejaa mifundisho ya kibwege ya kitheolojia ya vyuo vya Kichungaji nk nguvu za Mungu huna mjinga wewe
Ndio maana unalia Lia humu .Ni aibu kwako kuwa washirikina na wachawi Wana wafuasi wengi kuliko wewe na huna nguvu ya kuwafanyia waje kwako
 
akainama

Nani akainama? Binadamu? Embu soma hiyo sentensi vzuri, nalimngoja bwana kwa saburi; akainama.
Mkuu hii nimesha fafanua tayari, ( angalia thread nime ku quote)

akainama" katika muktadha wa Zaburi 40:1 hayatafsiriwi moja kwa moja kama kitendo cha kimwili cha Mungu kuinama. Badala yake, hii ni taswira au lugha ya kiroho inayoelezea huruma na kusikiliza kwa upendo wa Mungu kuelekea wale wanaomngojea kwa subira.
 
Tuendelee hii nilishaiona mkuu wangu.
 
1......……. Hapa kuna wa "WADAI WA MUNGU" na "KUTUMWA KWAKO ." Ikiwa unarejelea msaada wa Mungu kwa binadamu, kuna mitazamo mingi kutoka kwa dini tofauti. Hapa kuna maoni kadhaa:

• Mitume na Manabii, Katika imani ya Kikristo, Wakristo wanafundishwa kwamba Mungu ametuma mitume na manabii kutoa mwongozo, mafundisho, na ufunuo wa mapenzi yake.

• Wakala wa Mungu, Mara nyingine, watu huamini kwamba malaika ni wajumbe wa Mungu wanaosaidia kuleta ujumbe, ulinzi, na mwongozo kwa binadamu.

•Kazi ya Roho Mtakatifu, Wakristo wengine wanafundishwa kuamini kwamba Roho Mtakatifu, ambaye anachukuliwa kama mmoja wa utatu wa Mungu, ni mwongozo na msaidizi anayeishi ndani ya waumini.

• Viongozi wa Kidini, Kulingana na dini, viongozi wa kidini wanaweza kuwa wajumbe wa Mungu wanaotumwa kufundisha na kuongoza waumini. ( lakini si manabii wa kizazi kipya)





2........….. kwa nini Mungu asifanye kazi yeye mwenyewe, tunaweza kugundua sababu kadhaa zinazotolewa:

• Kupitia Binadamu na Viumbe, Katika imani, Mungu anachagua kufanya kazi yake kupitia binadamu au viumbe vyake ili kuonyesha upendo wake na kuweka msisitizo wa ushirikiano kati yake na mwanadamu.

• Utekelezaji wa Mpango wa Mungu, ikiwa tunachukulia Mungu kuwa ni mwenye hekima na mwenye mpango, kuna dhana kwamba kufanya kazi kupitia viumbe ni sehemu ya mpango wake mkamilifu.

• Kuimarisha Imani, Kwa mujibu wa mafundisho ya kidini, Mungu anaweza kuchagua kufanya kazi kupitia binadamu ili kuimarisha imani yao na kuwapa fursa ya kujitolea kwa hiari.

• Uwezo wa Kuchagua, Mungu anaamini katika uhuru wa kuchagua, basi kutoa nafasi kwa viumbe wake kufanya kazi ni njia ya kuheshimu uhuru na utashi wao.
 

Mwenyezi mungu anasema, nitajibu hoja ya kila mtu, Kwa mda muafaka na ulio sahihi...
 
Kutoamini uwepo wa Mungu si mtazamo wangu mimi binafsi. Kuna watu walikuwepo maelfu na maelfu ya miaka hawakuamini uwepo wa Mungu. Ukisema huu ni mtazamo wangu binafsi, unaniambia kwamba hujaelimika katika haya mambo, hujamsikia hata Epicurus aliyezaliwa miaka 342 BCE. Miaka hiyo mimi sikuwepo, lakini watu walipinga imani ya Mungu.

Hiyo mistari uliyoiweka ni mistari ya imani, haithibitishi Mungu yupo na haiondoi cintradictions katika dhana ya kuwepo Mungu.

Hivyo, mimi hainiambii kitu chochote cha maana kipya.

Ukitaka kunipa kitu cha maana na kipya.

1. Thibitisha Mungu yupo, kimantiki.

2. Ondoa contradictions za kwenye Biblia.

3. Ondoa contradictions kwenye dhana ya kuwepo Mungu.
 
kwamba kufanya kazi kupitia viumbe ni sehemu ya mpango wake mkamilifu
Hii dhana ya mpango wake mkamilifu inatokea wapi?

Kwanini kufanya kazi na viumbe visivyo vikamilifu kufanye mpango wake kuwa mkamilifu?

Kwanini iwe ni sehemu ya mpango wake mkamilifu? Je hajitoshelezi mpak useme kufanya kazi na viumbe ni sehemu ya mpango wake kukamilika?
 
• Mkuu mimi siyo nabii, mimi siyo Mchungaji, mimi siyo mashii, Mimi siyo shetani wala siyo wakala wa shetani, wala sijishughulishi na vikao vya kidini au utafunaji wa hela za waumini...

• Swali langu fikirishi ni kwamba katika vitabu vya kidini vinasema nabii/masihi wa mwisho ni yesu, Mathayo sura ya 3 anaelezea huduma ya Yohana Mbatizaji, Pia ukitazama kitabu Qur'an, sura ya 4 (An-Nisa - Wanawake) na sura ya 61 (As-Saff - Safu). Sasa kutokana na vipengele tajwa hapo juu, Je hawa manabii wa kizazi kipya, hizo nguvu wanapewa na mungu...!! Au wametengenenza za kwao?
 
Wewe unaweza kuthibitisha kuwa hayupo?
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwapo, ulimwengu wenye kuwezekana kuwa na mabaya usingekuwapo.

Huyu Mungu sifa zake zinamfanya asiwe mchoyo wa mazuri kiasi cha kuruhusu ulimwengu ambao unaweza kuwa na mabaya uweze kuwapo wakati angeweza kirahisi tu kuufanya usiwezekane kuwapo.

Kwa hivyo, ama Mungu huyu yupo, na ulimwengu unaoweza kuwa na mabaya haupo, ama ulimwengu unaoruhusu mabaya upo, na Mungu huyu hayupo. Viwili hivi ni mutually exclusive. Kikiwapo kimoja, kingine hakipo.

Tunaona ulimwengu unaoruhusu mabaya upo.

Hivyo, Mungu huyo hayupo.

Ni wa hadithi za kutungwa na watu tu.
 
• Kukushawishi imani(mungu) ni jambo lenye changamoto, Kwa maana mungu anasema mimi ni roho, mimi ni nafsi niliyopo mioyoni mwenu hamta niona kwa macho yenu ya damu. kwani imani mara nyingi ni suala la kibinafsi, kiroho, Kumbuka, kila mtu ana safari yake ya kiroho,(Waamini mungu yupo)

1.....….…. Binadamu wanaweza kujisifia kuhusu uwepo wa Mungu kwa njia mbalimbali, kulingana na imani zao na uzoefu wa kibinafsi. Baadhi ya mambo ambayo watu wanaweza kujisifia ni pamoja na:-

• Kuona Miujiza, Baadhi wanaweza kuelezea matukio ya kipekee au miujiza ambayo wanahisi ni ishara ya uwepo wa Mungu katika maisha yao.

• Kutambua Njia za Mungu, Wengine wanaweza kujisifia kwa kutambua na kuelewa miongozo na njia wanazohisi zinaongozwa na Mungu katika maamuzi yao.

• Uhusiano wa Kibinafsi na Mungu, Watu wanaweza kujisifia kwa kuwa na uhusiano wa kibinafsi na Mungu kupitia sala, ibada, na kusoma maandiko.

• Mabadiliko ya Kiroho, Kujisifia kwa mabadiliko chanya katika tabia na maisha wanayoyaona kama matokeo ya uwepo wa Mungu.

• Imani katika Maana na Madhumuni, Baadhi wanaweza kujisifia kwa kuwa na imani ya kwamba uwepo wa Mungu unawapa maana na madhumuni katika maisha yao.

• Haya ni baadhi ya maneno au matamko ya binadamu mbali mbali, yakitoa ushuhuda baada ya kuomba kupitia neno la mungu, baba, uliye juu, ibariki kazi ya mikono yangu.. Na mambo yao yakaenda vizuri 🙏🙏.
 
Kama umesoma vipande vyote vitatu nilivyo Andika, mungu anasema Nimeamua kugawa majukumu, Haijalishi najitosheleza au sijitoshelezi, Ameamua kugawa majukumu ili binadamu wawe Karibu zaidi na neno la mungu, hivyo aliamua kufanya hivyo ili kuwakumbusha zaidi binadamu kuhusu ufalme wa mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…