Enyi wachambuzi wa mpira, mbona hampazi sauti juu ya uhuni uliofanywa na TFF kuwadhurumu watoto haki yao?

Enyi wachambuzi wa mpira, mbona hampazi sauti juu ya uhuni uliofanywa na TFF kuwadhurumu watoto haki yao?

Mtoto wa chini ya miaka 15 anataka kulipwa?
Sidhani hata kama sheria za FIFA zinaruhusu hii.
Tangu lini kuichezea team ya Taifa ilikuwa ni kuhusu malipo.
Kwamba wamepokonywa Jezi? Au wamerudisha jezi. Waliambiwa hizo jezi ni mali yao?
Kuna vitu vya kulalamika, ila sio hili la kutaka kuanza kuwalipa watoto wa miaka 15 wakilichezea Taifa.
Hio jezi ni kumbukumbu kwa mchezaji unapo wapokonyonya wakati mashindano yamefika mwisho unazipeleka wapi? in addition kila tournament hua zinatengenezwa kits mpya
 
MBONA UNATETEA UJINGA MZEE KWA HIYO ZAWADI ANAPEWA NANI??

ACHA KUTETEA UJINGA
Zawadi linapewa Taifa mshindi.......
Kwa maana ya Shirikisho la mpira la nchi husika, na kama zawadi haina limitation za matumizi ni wao ndio wataamua inaenda wapi.
Wachezaji hawachezi Team za Taifa ili walipwe, ukiona mtoto wa miaka 15 analilia hela kuna shida pahala.
 
NALIA NGWENA huwa nashangazwa sana na wachambuzi wa kibongo wanaojiita wanaharakati na uchambuzi wao umejikita juu ya Simba sc na Yanga Sc utadhani hii nchi Kuna timu mbili tu ndiyo zinacheza.

Kuna bwana mdogo kaandika kwenye mitandao anaituhumu TFF kuwa imewadhurumu haki Yao hawajalipwa lakini wachambuzi MAANDAZI wapo kimya tu.

Mbona Suala la Feisal salum Wachambuzi mliongea sana na harambee ya kumchangia mlipitisha bakuli??

Wachambuzi wa Kitanzania mnachambua football gani na mnaangalia/mnapigania harakati gani ili mpira ukue??

Hao watoto wa Under 15 ndiyo taifa la kesho Sasa Kama wanafanyiwa Madudu Kama haya na wakaamua kuachana na mpira mnadhani kuwa tutapata wapi wakina John Bocco, Mbwana Samata N.k??

Maoni Yangu: Enyi wachambuzi wa Mpira ACHENI kupaza sauti kwa Simba SC na Yanga Sc tu, Pazeni sauti juu ya haki na kudhurumiwa kwa watoto/wadogo zetu kwani ndiyo wachezaji wetu wa baadae lakini tukikaa kimya kizazi Cha football kitakufa kwa Tamaa za watu wachache.

NALIA NGWENA natumia jukwaa hili la michezo na mtandao wetu Pendwa Jamii forum kuwaambia @cloudsfm @efmradio vipindi vya michezo na redio zingine kuwa acheni kuangalia Simba na Yanga tu Pazeni sauti juu ya huu uhuni na dhuruma kwa watoto wadogo.
Washaokulaa bahashaaa haoo
 
Kwani hawana wazazi??
Kwahiyo walipwe wazazi? Tsh ngapi kila mmoja unapendekeza.
Vipi Gharama za kuwatunza wakiwa kule walitoa wazazi?
Vipi gharama za watoto mwakani watatoa wazazi?
Hivi nyie watu huwa mnawaza Namna gani?
 
Hayo
Walichokifanya TFF siyo haki.

Na uzuri nimemuona na kumsikia Wallace Karia akiliongelea jambo hilo kwa kutoa sababu ambazo hazijajitosheleza.

Mfano anasema eti waliwanyang'anya jezi hao watoto kwa sababu hizo jezi zimetengenezwa kwa gharama kubwa!! Kweli ndiyo sababu yenye mashiko hii kutolewa na rais wa shirikisho!!

Halafu sababu ya kutowapa mgao wa fedha walizopewa kwenye hayo mashindano baada ya kuwa washindi wa 2, 3, nk ni kwa sababu mdhamini (Motsepe) alitaka zitumike kujengea miundombinu!!! Sawa!!

Sasa imekuwaje washindwe kuwapa hata posho hao watoto? Je, hawakustahili kupewa chochote, isipokuwa chakula na malazi waliyopata wakati wa mashindano, na nauli tu ya shilingi elfu 20-50 ya kurejea makwao?

Yaani rais Wallace Karia anataka kutuambia Shirikisho halikuwa na fedha ya motisha kwa hao watoto ili na wenyewe wapate moyo wa kulipambania Taifa lao wakati mwingine?

Je, Karia anataka kutuambia hata maafisa wake na benchi la ufundi walioambatana na hao watoto kwenye hayo mashindano, walilipwa nauli tu za kurejea majumbani kwao!!

This is unfair!! Na cha kuhuzunisha, wakati anajibu hizi tuhuma; alijikita zaidi kwenye zile kauli zake zilizo zoeleka za nyodo, dharau na kejeli. Huwa hapendi mawazo mbadala! Hapendi kukosolewa!! Huyu jamaa anatakiwa kubadilika.
Hayo ni miongoni mwa maajabu yanayopatikana Tanganyika ndio maana wageni hawaishi kuja kushangaa mkuu.
Na mengi mno sema tu wengi huwa wanaambiwa wakiyasema hawataitwa tena na vipaji vyao vitateketea.
 
Hio jezi ni kumbukumbu kwa mchezaji unapo wapokonyonya wakati mashindano yamefika mwisho unazipeleka wapi? in addition kila tournament hua zinatengenezwa kits mpya
Kupokonywa una maanisha nini?
Wachezaji wamerudisha Jezi.
Hawajapokonywa......
Na sioni hoja hapa, ni lini Jezi mtu anaondoka nazo Bongo hii?
Kwani hamfahamu Jezi zinafuliwa......

Ni vizuri kama jezi wangeondoka nazo, ila kuambiwa wazirudishe haipaswi kuwa hoja ya malalamiko.
 
Hio jezi ni kumbukumbu kwa mchezaji unapo wapokonyonya wakati mashindano yamefika mwisho unazipeleka wapi? in addition kila tournament hua zinatengenezwa kits mpya
Uonevu tu. Mbaya zaidi hilo shirikisho lina mkataba na Sandaland kwa ajili ya kudhamini jezi, nk!! Halafu watoto baada ya kutumia jezi, eti wanatakiwa kuzirejesha!!

Wizi mtupu!! 😁
 
Kw
Mtoto wa chini ya miaka 15 anataka kulipwa?
Sidhani hata kama sheria za FIFA zinaruhusu hii.
Tangu lini kuichezea team ya Taifa ilikuwa ni kuhusu malipo.
Kwamba wamepokonywa Jezi? Au wamerudisha jezi. Waliambiwa hizo jezi ni mali yao?
Kuna vitu vya kulalamika, ila sio hili la kutaka kuanza kuwalipa watoto wa miaka 15 wakilichezea Taifa.
Kwa hiyo walikuwa wanajitolea na hivyo hawapaswi kupewa hamasa?
 
Kuzing'ang'ania unamaanisha nini?
Uliwahi kuuliza hata Timu za wakubwa kama huwa wanaondoka na jezi?
Unanilimit nanmna ya kufikiri? Kwamba jibu liwe ndio au hapana?
Kwani watu mkiskia timu ya Taifa mnaelewa nini kwani? Pahala pa kwenda Kugawana posho na Kucheza ili uondoke na Jezi?

Ukiona mtu yoyote anampa motisha ya Fedha mtoto jua anashida pahala.
Miaka 15 anadai hela? Sijawahi skia hii.......
Endelea kuchelewa kusikia.
Kwani TFF wamepewa fedha zitokanazo na hayo mashindano ama hawaiupewa?

Km wamepewa,ni kwa nini?
 
Kw

Kwa hiyo walikuwa wanajitolea na hivyo hawapaswi kupewa hamasa?
Mtoto wa miaka 15?
Analipwa? Ni nchi gani inawalipa watoto wa miaka 15.
Mpira wa team ya Taifa haijawahi kuwa ni kuhusu Fedha, ni Pride ya Kuwa Mtanzania.
Pandikiza mawazo ya malipo kwa watoto wa miaka 15.
Miaka 10 mbele utaona unakuwa na team ya taifa ya namna gani.
 
Kupokonywa una maanisha nini?
Wachezaji wamerudisha Jezi.
Hawajapokonywa......
Na sioni hoja hapa, ni lini Jezi mtu anaondoka nazo Bongo hii?
Kwani hamfahamu Jezi zinafuliwa......

Ni vizuri kama jezi wangeondoka nazo, ila kuambiwa wazirudishe haipaswi kuwa hoja ya malalamiko.
Kwa hiyo baada ya kuzirejesha hizo jezi, mnazipeleka wapi? Mnaenda kuziuza, kuzigawa kwa wajumbe wenu wa TFF! Au mnaenda kuzihifadhi kwa ajili ya mashindano yajayo?

Mlichokifanya kwa hao watoto siyo poa hata kidogo. Yaani nyinyi ambao hata kupiga danadana tu hamuwezi, mnajilipa posho za kila aina!! Halafu watoto waliohangaika kuwapatia hayo mafanikio, mnaishia kuwapa tu nauli ya kurejea makwao!! Eti kwa sababu ni watoto!!

Mlishindwa hata kuwanunulia zawadi zinazoendana na umri wao kama motisha, kutokana na hicho walichokifanya!! Acheni ubabaishaji nyinyi.
 
Kupokonywa una maanisha nini?
Wachezaji wamerudisha Jezi.
Hawajapokonywa......
Na sioni hoja hapa, ni lini Jezi mtu anaondoka nazo Bongo hii?
Kwani hamfahamu Jezi zinafuliwa......

Ni vizuri kama jezi wangeondoka nazo, ila kuambiwa wazirudishe haipaswi kuwa hoja ya malalamiko.
Jezi inarudishwa kama mashindano yana endelea yakifika mwisho jezi inarudishwa kufanya nini? Kila shindano lina bajeti yake na kits zake hao watoto wanahitaji hivyo vifaa kuendeleza careers zao tena ingependeza baada ya mashindano wapewe zaidi kumbuka wengi wao wanatoka familia duni
 
Back
Top Bottom