Enyi wachambuzi wa mpira, mbona hampazi sauti juu ya uhuni uliofanywa na TFF kuwadhurumu watoto haki yao?

NALIA NGWENA huwa nashangazwa sana na wachambuzi wa kibongo wanaojiita wanaharakati na uchambuzi wao umejikita juu ya Simba sc na Yanga Sc utadhani hii nchi Kuna timu mbili tu ndiyo zinacheza.

Kuna bwana mdogo kaandika kwenye mitandao anaituhumu TFF kuwa imewadhurumu haki Yao hawajalipwa lakini wachambuzi MAANDAZI wapo kimya tu.

Mbona Suala la Feisal salum Wachambuzi mliongea sana na harambee ya kumchangia mlipitisha bakuli??

Wachambuzi wa Kitanzania mnachambua football gani na mnaangalia/mnapigania harakati gani ili mpira ukue??

Hao watoto wa Under 15 ndiyo taifa la kesho Sasa Kama wanafanyiwa Madudu Kama haya na wakaamua kuachana na mpira mnadhani kuwa tutapata wapi wakina John Bocco, Mbwana Samata N.k??

Maoni Yangu: Enyi wachambuzi wa Mpira ACHENI kupaza sauti kwa Simba SC na Yanga Sc tu, Pazeni sauti juu ya haki na kudhurumiwa kwa watoto/wadogo zetu kwani ndiyo wachezaji wetu wa baadae lakini tukikaa kimya kizazi Cha football kitakufa kwa Tamaa za watu wachache.

NALIA NGWENA natumia jukwaa hili la michezo na mtandao wetu Pendwa Jamii forum kuwaambia @cloudsfm @efmradio vipindi vya michezo na redio zingine kuwa acheni kuangalia Simba na Yanga tu Pazeni sauti juu ya huu uhuni na dhuruma kwa watoto wadogo.
watoto wanapaswa kushukuru kupewa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao , lengo la mashindano ya under 18 ni kutoa platform ya watoto kucheza mpira sio kujiingizia kipato , mtoto halipwi ,washukuru kupewa nauli na nafasi ya kuonyesha vipaji kati ya maelfu ya watoto wa umri wao
 
Wanafundishwa uzalendo,
Sio kila kitu kulalamika tu nyie kenge
unamlipa vipi mtoto? watoto wanapaswa kufurahi kupatiwa nafasi kati ya ma Elfu , watoto wanahitaji basic needs wakiwa kambini , kiufupi kambini pawe Bora kuliko nyumbani , kama hawajawarudisha nyumbani kwao (nauli)ni sahihi TFF kuliangalia hili sio mtoto kulilia malipo .
 
NALIA NGWENA huwa nashangazwa sana na wachambuzi wa kibongo wanaojiita wanaharakati na uchambuzi wao umejikita juu ya Simba sc na Yanga Sc utadhani hii nchi Kuna timu mbili tu ndiyo zinacheza.

Kuna bwana mdogo kaandika kwenye mitandao anaituhumu TFF kuwa imewadhurumu haki Yao hawajalipwa lakini wachambuzi MAANDAZI wapo kimya tu.

Mbona Suala la Feisal salum Wachambuzi mliongea sana na harambee ya kumchangia mlipitisha bakuli??

Wachambuzi wa Kitanzania mnachambua football gani na mnaangalia/mnapigania harakati gani ili mpira ukue??

Hao watoto wa Under 15 ndiyo taifa la kesho Sasa Kama wanafanyiwa Madudu Kama haya na wakaamua kuachana na mpira mnadhani kuwa tutapata wapi wakina John Bocco, Mbwana Samata N.k??

Maoni Yangu: Enyi wachambuzi wa Mpira ACHENI kupaza sauti kwa Simba SC na Yanga Sc tu, Pazeni sauti juu ya haki na kudhurumiwa kwa watoto/wadogo zetu kwani ndiyo wachezaji wetu wa baadae lakini tukikaa kimya kizazi Cha football kitakufa kwa Tamaa za watu wachache.

NALIA NGWENA natumia jukwaa hili la michezo na mtandao wetu Pendwa Jamii forum kuwaambia @cloudsfm @efmradio vipindi vya michezo na redio zingine kuwa acheni kuangalia Simba na Yanga tu Pazeni sauti juu ya huu uhuni na dhuruma kwa watoto wadogo.
Hakuna mtu anaetaka kudeal na kitu asichokuwa na uhakika nacho
 
Jezi si mali ya tff ni mali ya mchezaji akishakabidhiwa, ndo maana ana uhuru wa kubadilishana na mchezaji pinzani baada ya mechi kuwalizika au hata kumpa shabiki. hayo mambo ya kufua jezi yalishapitwa na wakati, na kama kuna kiongozi anang'ang'ania jez huyo hatufai,

Watoto walitakiwa waachiwe jez kama kumbukumbu na kulipwa walipwe, mambo ya wanatumikia taifa kwa hyo wasilipwa huo ni uduanzi, taifa/tff halikuhusika katika kuwakuza mpaka wakawaona wanafaa na kuanza kuwatumia.
Hao vima wanapata laana za bure tu ukute wanachukua jezi wakawape watoto wao nyumbani huku waliofanikisha wakiwapokonya yaani Umasikini wa watu huwa hauwatoki hata wakifanikiwa maana upo kwenye damu...
 
Mtoto wa miaka 15?
Analipwa? Ni nchi gani inawalipa watoto wa miaka 15.
Mpira wa team ya Taifa haijawahi kuwa ni kuhusu Fedha, ni Pride ya Kuwa Mtanzania.
Pandikiza mawazo ya malipo kwa watoto wa miaka 15.
Miaka 10 mbele utaona unakuwa na team ya taifa ya namna gani.
Wanalipwa... Sijui kuhusu football lakini watoto wanalipwa. Waigizaji watoto wanalipwa kwa mfano. Yule dogo wa home alone alikuwa akilipwa na alikuwa chini ya umri wa miaka 15. Mtoto wa will smith baada ya kusainiwa na lebo ya jay z alikuwa akilipwa.
Kwa hiyo si kweli kuwa mtoto wa moaka 15 hafai kulipwa, hicho si kigezo.
 
Ni mpira, tena Specific national team.
 
Hili binafsi hata mimi limenishangaza mtoto wa miaka 15 bado ni mdogo sana hata interest na hela huwa hawana kiivo huwa wanapenda kucheza mpira na kufurahi hayo mambo ya pesa nadhani kuna vijeba kwenye timu wanawashawishi vibaya madogo

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Mkumbuke wanapambana kwa ajili ya familia zao kuku nyie.
 
NALIA NGWENA huwa nashangazwa sana na wachambuzi wa kibongo wanaojiita wanaharakati na uchambuzi wao umejikita juu ya Simba sc na Yanga Sc utadhani hii nchi Kuna timu mbili tu ndiyo zinacheza.

Kuna bwana mdogo kaandika kwenye mitandao anaituhumu TFF kuwa imewadhurumu haki Yao hawajalipwa lakini wachambuzi MAANDAZI wapo kimya tu.

Mbona Suala la Feisal salum Wachambuzi mliongea sana na harambee ya kumchangia mlipitisha bakuli??

Wachambuzi wa Kitanzania mnachambua football gani na mnaangalia/mnapigania harakati gani ili mpira ukue??

Hao watoto wa Under 15 ndiyo taifa la kesho Sasa Kama wanafanyiwa Madudu Kama haya na wakaamua kuachana na mpira mnadhani kuwa tutapata wapi wakina John Bocco, Mbwana Samata N.k??

Maoni Yangu: Enyi wachambuzi wa Mpira ACHENI kupaza sauti kwa Simba SC na Yanga Sc tu, Pazeni sauti juu ya haki na kudhurumiwa kwa watoto/wadogo zetu kwani ndiyo wachezaji wetu wa baadae lakini tukikaa kimya kizazi Cha football kitakufa kwa Tamaa za watu wachache.

NALIA NGWENA natumia jukwaa hili la michezo na mtandao wetu Pendwa Jamii forum kuwaambia @cloudsfm @efmradio vipindi vya michezo na redio zingine kuwa acheni kuangalia Simba na Yanga tu Pazeni sauti juu ya huu uhuni na dhuruma kwa watoto wadogo.
= kuwadhulumu
= dhuluma / dhulma.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Mzazi unapaswa kuona aibu kama unamtegemea dogo wa miaka 15 atunze familia....
Hao watoto wanatakiwa wafunzwe maana ya haki kwa vitendo,na wasifunzwe uhuni kwa vitendo kama baadhi ya viongozi wa TFF wanavyotaka kuwaaminisha hao watoto kwa kutowapa stahki zao.
 
Jezi si mali ya tff ni mali ya mchezaji akishakabidhiwa, ndo maana ana uhuru wa kubadilishana na mchezaji pinzani baada ya mechi kuwalizika au hata kumpa shabiki. hayo mambo ya kufua jezi yalishapitwa na wakati, na kama kuna kiongozi anang'ang'ania jez huyo hatufai,

Watoto walitakiwa waachiwe jez kama kumbukumbu na kulipwa walipwe, mambo ya wanatumikia taifa kwa hyo wasilipwa huo ni uduanzi, taifa/tff halikuhusika katika kuwakuza mpaka wakawaona wanafaa na kuanza kuwatumia.
Ni lini Jezi ilikuwa mali ya mchezaji Bongo hii?
Jezi zinafuliwa na kutumika tena.
 
So, linapokuja suala la jezi tutumie uzoefu wa bongk wa jezi si mali ya mchezaji tofauti na wenzetu tunafua na kutumika tena.
Ila likija suala la kuwapa pesa, japo sasa tutumie uzoefu wa kimataifa watoto hawapewi pesa.
Typical Tanzanian, kuchagua mifano ya kile kinachomnufaisha. Kama hakimnufaishi utasikia kwanimi tuwaige wao. Kama kinamnufaisha utasikia, hata UK wanafanya hivi hivi.
 
Basi wangewapa hata motisha.
Haiwezekani useme mmeshinda halafu ushindi si wao wala wazazi wanaouona. Wangewanunulia hata kitu kinachoendana na umri wao na hizo jezi wakawaachia. Ndio maana hata watoto wanaofaulu wanawapa vitu vya kuwamotivate wazidi kufanya bora zaidi.
Kuwapa motisha ni jambo zuri, zawadi mbali mbali nakubaliana na wewe.
Vifaa vya Shule, vifaa vya michezo etc.
Lakini Hakutakiwi kuwa na mentality ya tukishinda hela tutagawana.
Hichi ndio nachokikataa, Wanacheza kwa ajili ya Taifa sio ili kupata pesa.
Shida inaanza si watoto wa chini ya 15 ni vijeba, ndio maana unaona wanalalamika.
 
Sasa kumbe wanajua kuwa wamepeleka vijeba? Kama wanajua basi wameanza wao kuvunja sheria basi inabidi tu wavilipe.
Maana huwezi kupanda mbaazi mwisho utake kuvuna mahindi. Soka la TZ lina mambo mengi ya ajabu
 
Back
Top Bottom