Enyi wapambanaji, "Kama kazi yako, hujawahi kutana na polisi au vyombo vya usalama" kuwa tajiri Ni ndoto!

Enyi wapambanaji, "Kama kazi yako, hujawahi kutana na polisi au vyombo vya usalama" kuwa tajiri Ni ndoto!

Makonda wa daladala wangekuwa mabilionea.

Kila gari likipigwa mkono anayeenda ku-negotiate ni konda na ni choka mbaya.

Au kukutana kupi kunaongelewa? Kulala "selo"?
 
Niliwaza zamani sana hivi nikasema niwe jambakuzi wa kutisha ila sasa yaliyonikuta ni mfadhaiko wa moyo baada ya kuwa na vitendea kazi vyote ila shida ikaja niliposoma uzi wa UMUGHAKA nikajikuta siitaki tena hiyo kazi wacha niendelee kula hela za tarehe 23
 
Kha! Hebu tofautisha kati ya polisi na Vyombo vya Usalama?!

Hivi nyinyi Usalama mnawachukuliaje?! 😃
 
Enyi wapambanaji, "Kama kazi yako,hujawahi kutana na polisi au vyombo vya usalama" kuwa tajiri Ni ndoto!

Utakuwa na maisha ya kawaida Sana, shida ZITAKUWA nawe kila siku, lakini kamwe hutoweza kuwa tajiri ktk maisha haya.

"Lakini Kama kazi yako unayoifanya una misuko suko ya kukutana na polisi,kamatia hapohapo,lazima utoboe"
Kuwa "tajiri" ni zaidi ya kupata hekaheka ma polisi..
 
bila kusahau wanaofanya biashara halali bila kukwepa kodi.
Hatukwepi kodi... tunalipa kidogo. Hakuna kitu ngumu kama kukata % kwenye mapato yako. Zaka inatushinda ndo izo 30% za serikali?
 
Niliwaza zamani sana hivi nikasema niwe jambakuzi wa kutisha ila sasa yaliyonikuta ni mfadhaiko wa moyo baada ya kuwa na vitendea kazi vyote ila shida ikaja niliposoma uzi wa UMUGHAKA nikajikuta siitaki tena hiyo kazi wacha niendelee kula hela za tarehe 23
KAZI ipi iyo Mkuu
 
Sio lazima uandamwe na polisi ndo utusue kimaisha.Wapo watu wengi Sana waliotoka kimaisha kwa kutumia mbinu halali kutafuta Mali zao.
 
Unawachukulia machinga poa? Machinga Ameshika mabegi na vitu vya kuzugia begi moja jipya ana mrungi na kete za bangi unamuona machinga anazurura kwa magufuli bus terminal lakini kila jioni hesabu anayofunga wewe kaote ndio utaipata
Huyo sasa sio machinga, huyo ni pusha anatumia umachinga kama cover.
 
Sio kila tajiri ametajirika kwa kupitia njia za haramu,
Watu masikini ndio huamini kua kila tajiri katajirika kwa kupitia njia za haramu,

Siku ukiingia Jela ndio utajua thamani ya uhuru wako,enjoy life na ridhika na ulichonacho huku ukiendelea kutafuta kwa njia za halali,
Life is very short,usipoteze muda wako kwa kukaa jela.
 
Back
Top Bottom