Enzi hizo kwenye mitihani ilikuwa akili kidogo, ujanja mwingi

Enzi hizo kwenye mitihani ilikuwa akili kidogo, ujanja mwingi

666 chata

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2013
Posts
1,700
Reaction score
3,921
Unakumbuka enzi izo za vibomu? wengine wakiita nondo, uangaliziaji na makamati ya kimkakati wakati wa mitihani mashuleni? ujanja ujanja wa kila namna ilimradi tu watu wafaulu mitihani.
Baadhi ya matukio
Tuko necta ya fomu 6 kuna demu mmoja aka kamatwa na ki karatasi kimekunjwa kwa ustadi mkubwa sana ndani yake kuna topic karibia zote za ilo somo, msimamizi akapiga kelele wakaja wenzake, kiboom kina urefu wa kama rula iv, shule ikaishia hapo.

Sasa mitihani ya ndani ya shule ndio ilikua noma, kuna mademu hao walikuaga hawajisumbui kusoma, siku za mitihani wanajichora kwenye mapaja topic za muhimu tu.

Wengine walikua wanaandika nondo za muhimu kwenye madawati wanayo kaa kwa ustadi mkubwa na kwa kifupi sana, hauwezi kujua ila yeye ndio anajua tu, ilo dawati akikuta kesho kwenye chumba cha mtihani halipo anaanza kuchanganyikiwa.

Kulikua na wataalam wanaandika vibomu, ka karatasi kadogo ila ndani kamejazwa topics zote na anakaweka nyuma ya booklet anateleza tu😂😂

Daah zamani kufaulu ilikua mbinu, unakuta jamaa wana akili sana darasani ila kila necta lazima wafeli. Kuna wahuni walikua wanakaa kamati, kila mtihani unafanyiwa mkakati mzito sana, jibu linaanzia kwa wa 1 ila linafika mpaka kwa 7.

kuna watu walikuaga wanaanza kusoma hesabu ile rasmi kabisa wiki moja kabla ya necta, baada ya kua wameiacha kama miaka miwili iv😂😂 Sijui wewe unakumbuka nini enzi izo!
 
Haahahha hapana, mie nimekumbushia tu elimu zetu zamani na wale wahuni wasiokua wanataka kusoma, sio kwa ubaya.
kwa ile mikazo ya enzi zenu unafkiri wazee wa Bibliography hawapo humu.
Wapo Sana Sema wanajikaza TU.🤣
 
Sisi tulikua hatujisumbui kuingia na vibomu tulikua tunakwangua rula tunaandika majibu ilikua noma sana ni mwendo wa kutembeza rula tu[emoji28]
 
Ila bado naamini watu bora kiakili na kiuwezo waliishia 2012 rudi nyuma.
Unaongelea level gani mkuu?? Chuo, advance au o-level.
Kama ni o level si ndo hazo wa
2012 waliorekebishiwa matokeo??
Tokeo limetoka, watu wamefeli serikali ikawapa wanafunzi maksi za bure wakafaulu kibao.

Ila kwa vyuo, walau.
 
Miaka hii wanaibia na hawana hata uelewa wa kutosha baada ya kumaliza shule, ukute huyo dada aliyefukuzwa shule kwa kibomu kipindi hicho sasa ni don
 
Mimi ni aina ya watu kitabia kama Joh wa kwenye American Ninja....

Mwanzon kabisa form one kwenye mtiani mtian ukaniwia mgumu baadhi ya maswali na Am 4 real huwaga sipendi acha swali nikaomba Tag Kwa salva for sure salva alinikazia alikua na chance ya kunisaidia swali lakini akaninyima makusudi

Tulipo Toka kwenye mtiani nilipo muuliza akajib Am 4 real
"UNAONA MIMI SIPATI SHIDA KWENY MITIANI HUWAGA NASOMA" akanambia Am 4 real uwe unasoma
"MWANAJESHI MWENYE AKILI HUPIGANA WAKATI WA AMANI"
for sure kwenye safar yangu ya elimu baada ya salva kuniambia ivyo sijawai pata wakati mgum kwenye mitiani
 
Miaka hii wanaibia na hawana hata uelewa wa kutosha baada ya kumaliza shule, ukute huyo dada aliyefukuzwa shule kwa kibomu kipindi hicho sasa ni don
Yeah sure, enzi zile unakuta watu hawasomi lakini vitu basics wanavijua.
 
Unaongelea level gani mkuu?? Chuo, advance au o-level.
Kama ni o level si ndo hazo wa
2012 waliorekebishiwa matokeo??
Tokeo limetoka, watu wamefeli serikali ikawapa wanafunzi maksi za bure wakafaulu kibao.

Ila kwa vyuo, walau.
Ngazi zote tu
 
Binafsi Mambo ya kupiga chabo , vibomu Nondo nk Mimi nilikua naona upuuzi tu nilichokuwa nafanya nawekeza katika harakati za Mtu mweusi najipanga Kuanzia A to Z .

wengi waliofeli shule ni kwasababu ya kutegemea chabo
So siku msimamizi akikaza lazima mambo yaharibike
 
Kuna wale wasiopenda kuvaa saa lakini siku za mitihani utakuta mtu kavaa saa mkanda wa ngoz mpana..muangalie Sasa namna anavyochomoa vibomu kwenye chumba Cha mtihani😂😂🙌
 
Miaka hii wanaibia na hawana hata uelewa wa kutosha baada ya kumaliza shule, ukute huyo dada aliyefukuzwa shule kwa kibomu kipindi hicho sasa ni don
Duuh!! Kwahyo waliosoma "zamani hiyo" wote wamefanikiwa, sio?
 
Kuna wale wasiopenda kuvaa saa lakini siku za mitihani utakuta mtu kavaa saa mkanda wa ngoz mpana..muangalie Sasa namna anavyochomoa vibomu kwenye chumba Cha mtihani😂😂🙌
Kweli mwaka ujao 2023 nikisimamia mitihani , Wajiandae kunyooshwa ntawakazia Sana , sio Kama mwaka huu.
 
swahiba wangu nilimpa paper yangu akopi, akakopi kila kitu mpaka jina...hahaaaa alirudia darasa masikini
 
Sasa rula unaikwanguq vp? dooh [emoji23][emoji23]
Rula unaikwangua na kiwembe ile layer ya juu kabla ya kuingia chumba cha mtihani

Kwahyo ukiingia kwenye paper kama swali hulielewi unaandika tu kwenye rula na penseli namba ya swali unampa mwenzako anakujazia kwenye rula anakurudishia unacopy majibu kilaini


Uzuri wa rula unatumia penseli Kwahyo hata msimamizi akikuona,unaweza ukafuta fasta ukapoteza ushahidi
 
Back
Top Bottom