Enzi hizo...

Naanza:
Enzi hizo mzazi akitaka kukuadhibu kwanza anakuagiza mwenyewe ukalete fimbo, sasa kalete fimbo ya kizembe uone. Fimbo pendwa ilikua mpera....Hebu tukumbishie na wewe enzi hizo [emoji2][emoji2][emoji2]
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ wengine Tulikuwa hatuambiwi hivyo.. Bse ukinambia hivyo sirudii nahamia kwa shangazi,Bibi mkubwa Kijiji Cha tatu huku nakaa wiki nasema bibi/baba au mama ataniua ... Siku ya kurudishwa narudishwa kishujaaa...πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Ulitaka unichape nimefanya kosa yapasa uvizie au unidanganye..
Like hey embu ingia ndani angalia hayo maziwa Kama yameshaganda uje nayo na kibiriti Tuwashe Moto ..Nkupikie ugali...
(Ugali maziwa dah ...ulinifanya niwe zuzu ..nkifanya kosa nakamatika kiulaini Sana)
Ila siku moja nilipigwa ..mnoo ...nilimchungulia mwalimu mkuu then nkapikiwa huo ugali aaargh Toka siku hiyo ndoa ilikufa ...maana kipigo kilikuwa heavy...
 
Team kuogelea mpo?
Team Kujipikilisha maporini pro?
Team Kombolela?
Team Wadokozi?
Team chandimu?
Team rede kina dada?
Ongezeeni ...aseh
 
Aisee we kiboko
 
Hahaham. Jusi cola juzi tu mkuu enzi hizo tulikua na super dip
 
Enzi hizo Yale magari ya mbao na matairi ya kandambili. Unatengeneza gari yako halafu unakuta Kuna jamaa mmoja maarufu mtaani kwa kutengeneza Kona, basi unaenda anakusukia Kona fresh. Wapo waliokua wataalam wa kutengeneza vipago vya manati. Halafu ukiua ndege unachkua damu unapaka kwenye kipago ili iwe inaua sana [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hahahah, ilikuaje ukamchungulia mkuu?
 
Wewe ya kitambo hii hizo dip mnajua nyie
Jusi cola naikumbuka mkuu ikiwa kwenye kipakti kama cheusi hivi. Uliza legends enzi za Super dip, soda Aina ya Fahari. Pipi cola za kitambo, toffie za zamani. Na zile pipi pundamilia. Naongelea 1995-1997 era
 
Mtaalamu wa kuyaiba magari yenu nipo hapa ...πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Sijawahi tengeneza gari ...
Kilikuwa pia kuna wataalamu wa Kuchonga pia /ndera...
Dah una kumbukumbu nzuri bro..
 
Hahhahahah nimecheka sana
 
Nilikuwa snitch balaa unitume nkuitie dada yangu ...teh teh unanipa hela sh kumi ama sh ishirini...
Nakuitia Bibi yangu au baba mkubwa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kaka umenikumbusha mbali auntie alikua anafungia deki pamoja na mikanda chumbani mpka kazi ifanyike aisee haoo watu watajituma fasta fasta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…