Enzi zetu haikuitajika Peugeot, Nissan Wala Datsun ila ukiwa na Phoenix, Swala, frying pegeou au Raleigh unang'oa walimbwende na ndoa zilidumu sana

Nilikuwa nna baskeli inaitwa bugati enzi hizo.siku hiyo nikaipiga pedeli hivyo hivyo kwa nyuma cheni ikachomoka ikazama kwenye freewili inanivuta asee nilipiga mzinga moja hioo na vumbi la kutosha.
Kuna ile unanyonga Pedels ila mnyororo hauleti ushirikiano,Baiskeli inakua haiendi,walikua wanaita Mbwa zimelala.
πŸ˜€πŸ˜€
 
Mnyama phoenix alileta mapinduzi makubwa sana. Kabla ya hapo turbo ndio ilikuwa tishio kijijini kwetu.
Phoenex Moja ya ubunifu Bora sana kuwai kutokea tangu Dunia iumbwe....Hawa wachina walileta mapinduzi ya baiskeli πŸ€“πŸ€ 
 
Ni kweli. Ila kuipata hio Phoenix walikua wanasota sawa tu na kupata crown sasa hivi. Atalima pamba hata misim mitatu akiweka akiba ya Phoenix [emoji1787][emoji1787]
 
Ni kweli. Ila kuipata hio Phoenix walikua wanasota sawa tu na kupata crown sasa hivi. Atalima pamba hata misim mitatu akiweka akiba ya Phoenix [emoji1787][emoji1787]
Haahaa, πŸ˜‚
Miaka ya nyuma mzee wangu alianzisha mradi wa kufuga Ng'ombe wa maziwa...
Kuna jamaa akaja kuomba kazi ya kukatia Ngo'mbe majani....
kumbe target yake kuiba Ile baiskeli...
true
alifanikiwa kutoroka na Ile baiskeli ya MZEE
hakupatikanaga tena...
 
Zile za gia alafu ukute zina kitenga kwa mbele zilipo ingia ndio zilikua hizi SUBARU FORESTER za vijana wa sasa.... Ukiishika unapiga gia tuu .unajiona mjanja sana

Na ukienda kusalimia ndugu na maragiki jua likizama kagiza kakiingia unaiacha huko huko utoki nayo usiku maana watakuteka uibiwe. Unarudi nyumbani kwa mguu utairudia kesho yake kuchukua ndinga yako
 
πŸ€“πŸ€“πŸ€“

Nimecheka hapo kwenye SUBARU FORESTER

Na kesho kuchukua ndinga yako....
 
Kuna ile unanyonga Pedels ila mnyororo hauleti ushirikiano,Baiskeli inakua haiendi,walikua wanaita Mbwa zimelala.
[emoji3][emoji3]
[emoji3][emoji3][emoji3] umenikumbusha mbali, eti mbwa zikilala inatakiwa ukojolee ile freewill , sasa ukiona mkojo huna inabidi umwombe mtu akujoe kwa kukusaidia.....daah.. [emoji12]
 
Mbwa zimelala nimecheka kama mtoto mdogo....
Sisi tuli ita ku trade....

Kuna watu wali lisha familia Kwa ufundi baiskeli [emoji851]
Zama zimebadilika...
Mi nilikuwa na nakorokochoa mwenyewe, fundi akila hela hapo labda ya kunyosha ringi tu na krispoko nampa mwenyewe, hapo kuna spana mojaa ilikuwa haikosi kwenye kibegi inaitwa "spana malaya" ilikuwa na matundo mengiiii.....[emoji3][emoji3]
 
[emoji3][emoji3][emoji3] umenikumbusha mbali, eti mbwa zikilala inatakiwa ukojolee ile freewill , sasa ukiona mkojo huna inabidi umwombe mtu akujoe kwa kukusaidia.....daah.. [emoji12]
Halafu kuna ile mnaitumia Kengele ya Baiskeli kujitizama kama kioo,basi ukijiona uso umekua mrefu au pua kubwa mnachekana.
πŸ˜€πŸ˜€
 
Au ilikua Baiskeli ikichanganya Speed,unakua unanyonga zile pedals kwa kurudisha nyuma,basi ule mlio wa ile Bearing ya tairi la nyuma unajiona mjanja.
[emoji3][emoji3]
[emoji23][emoji23][emoji23] una kumbukumbu sana

Namkumbuka jamaa mmoja kila asubuhi tukiwa primary atapita hivyo kwa kasi namchungulia dirishani tu
 
Sikuhizi hata kutembelea ndugu na jamaa hakupo tena kwsbb ya smartphones
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…