Tunakumbushana tu, ndivo ilivokuwa.
Shule private maarufu enzi zetu kulikuwa Jitegemee, Vituka na sait Antony Mbagala
huku tarime kulikuwa na Shirati sec school.
Je wewe unakumbuka lipi? Gen Z mtupishe.
Waliokuwa wanasoma shule private ni wale waliofeli mitihani ya kuingia kidato cha kwanza na kidato cha tano, enzi hizo walikuwa takataka, wengi wao walikimbilia shule za seminari, pale Mbeya tulikuwa na Sangu Secondary School, na Darisalama palikuwa na Kinondoni Muslim, kule Kilimanjaro boys' enzi zile private school walichokuwa wanakiweza ni michezo tu,mashindano ya UMISETA, pia wengi walikuwa wanyonge wanyonge watemi walikuwa shule za serikali, ukienda kule Ruvuma utakuta Kaigo,Box 2 pale Mbeya utakuta Rungwe na Iyunga, Pwani utakuta Kibaha Sec, Kagera Ihungo, Kigoma Sec, Ndanda, Masasi girls,Mazengo,Ilboru,Mzumbe,Mazengo n,k ilikuwa raha sana, kila kitu bure,tunakatiwa tiketi kwenda na kurudi nyumbani kwa treni au mabasi ya Relwe unachagua tu wapi uende wakati wa likizo. Ukiwa kiranja mkuu unakuwa kama raisi, unakuwa na menu yako na chumba chako binafsi cha kulala. Ukikosea unalambwa bakora au unapewa adhabu ya kuchimba visiki, tuliosma wengi tulikuwa watoto wa masikini, utakuta una kaptula moja na shati moja, suruali unaazima. Wengine walikuwa wanaamua kubaki mashuleni wakati wa likizo na kufanya vibarua vya kulima ili waweze kujikimu,makwao hali ilikuwa ni tete kimaisha, wengi wao hivi sasa ndio wanatupangia maisha na kutoa maamuzi ya hovyo hovyo wamesahau walikotoka.